asiyetabirika
Member
- Oct 14, 2019
- 46
- 56
Kuna muda wamekuwa ni msaada ila kuna mda wanakuwa ni waumizaji hasa kwenye mazao ya kilimo, yaani mkulima unaweza pambana huko shambani halafu mazao yakifika sokoni dalali anakupangia bei huku na yeye atakwambia umlipe kiasi fulani cha pesa ambacho kimsingi huwa ni kikubwa kulingana na kifungashio mathalan gunia moja la vitunguu unaweza ambiwa kwenye kila gunia dalali atahitaji kati ya tshs 5000 hadi 7000 sasa hapa mkulima lazima aumie kwani muda mwingine ghalama za uzalishaji huko mashambani,kodi za mazao na usafirishaji huwa zipo juu.
Sasa naomba kujua uhalali wa hawa watu kwenye kupanga bei lakini uhalali wa ile pesa wanayoipata kwani muda mwingine unaweza kuta unamlipa 7000 na bado wakukuuzia kwa bei ya juu ila wewe ukapewa kalekale kahela ka mwanzo ,
Mfano watakwambia bei ya gunia ni tshs 70,000 ila utato 7000 ya dalali maana yake pesa yako hapo ni tshs 63,000, mkisha kubaliana hapo maana yake hata wakiuza kwa tshs 80,000 pesa yako itabaki ileile 63,000.
Kwanini mamlaka husika zisiweke mipaka kwa hawa majamaa namna ya kufanya kazi zao?