Je, Ujasiriamali ni chaguo lako lakini mtaji umekuwa changamoto kwako? Jaribu kupitia fursa hizi tano

FAJES

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2017
Posts
720
Reaction score
644
Ujasiriamali ni shughuli inayohitaji ujasiri na uimara kiroho na kimwili. Kama unadhani kufanya biashara au Ujasiriamali ni shughuli yako ya pili au mbadala baada ya kukosa kazi unayoipenda basi hutafanikiwa.

Jambo muhimu la kuzingatia katika tasnia ya ujasiriamali ni kwamba, fursa za biashara hutokana na changamoto za upatikanaji wa huduma na bidhaa mbalimbali katika jamii inayoishi. Hivyo kanuni za kiujasiriamali ni kuwa, tunabadilisha hizo changamoto na kuwa fursa za kibiashara.

Je, umekutana na changamoto yoyote ya upatikanaji wa huduma katika eneo unaloishi.? Kama jibu ni ndiyo, changamoto hiyo ibadilishe na kuwa fursa ya biashara. Kama si rahisi kwako kutengeneza wazo la kibiashara usisite kuleta changamoto hizo katika jukwaa hili maana kuna wadau mbalimbali ambao wanaweza kukusaidia.

Nikijikita moja kwa moja kwenye mada: Huenda Ujasiriamali ni chaguo lako namba moja lakini mtaji umekuwa ni tatizo kwako.

Leo nimejaribu kukusogezea fursa ndogondogo unazoweza kuanza nazo kutokana na hali yako ya kifedha na vile vile kwa kuzingatia facilities katika eneo unakoishi. Hata hivyo, ni vema kuzingatia kwamba, japokuwa hautahitaji kuwa na mtaji mkubwa sana kufanya shughuli hizi lakini ukweli ni kwamba bado itakuhitaji kuwa na kiasi angalau kidogo cha kuanzia.

Fursa namba moja: Biashara ya Mahindi

Je, unaweza kuuvaa ujasiri na kuanza kuuza mahindi ya kuchoma?

Shughuli hii haitohitaji mtaji mkubwa zaidi ya Tshs. 70,000 kwa kuanzia. Kwa maana ya kununua jiko, mkaa, wavu na mahindi ya kuanzia.

Ukifanikiwa kuanza na mahindi 50 kwa siku ambayo Utayauza kwa Tsh. 500 @ moja maana yake utaweza kupata Tsh. 25,000 kwa siku. Ukiondoa gharama za kununua mahindi na mkaa kwa siku unaweza kutengeneza Tsh. 10,000 @ siku na 70,000 kwa wiki na 280,00 - 300,00 kwa wiki under Ceteris Paribus (When other factors are kept constant). Shabaha hapa si kuwa mchomaji wa mahindi mwaka mzima au siku zote za maisha yako. Lengo ni kukusanya fedha zitakazokuwezesha kupiga hatua kuelekea malengo yako uliyojiwekea hapo baadae.

Natambua kuwepo kwa changamoto za kila biashara, lakini kwa hatua ya mwanzo naomba tu-assume kama hazipo ili upate morale ya kuthubutu na kuanza kupiga hatua ya kuanza.

Biashara nyingine zinazofanana na hiyo ni zile za kuuza kahawa na uji . Yaani utatumia mtaji wa kama 70,000 hivi na kutengeneza faida ya Tshs. 10,000 kwa siku. Kama wewe ni +ve minded person, jaribu fursa hizi kwa vitendo kisha baada ya juma moja urudi hapa tupeane mrejesho.

Fursa namba 2: Huduma ya Maji Majumbani.

Hii Fursa zaidi ya sehemu zenye changamoto za upatikanaji wa maji laini yasiyokuwa na chumvi (soft water) hasa Kwa Dar es Salaam na maeneo mengine yenye changamoto kama hii.

Katika macho ya kiujasiriamali, kila changamoto inayojitokeza kwenye jamii huwa inabadilika na kuwa fursa.

Maeneo mengi Dar yanachangamoto ya upatikanaji wa maji yasiyokuwa na chumvi. Hapa inategemea na uwezo wako kifedha. Kama unamtaji kidogo unaweza kutafuta mahala penye maji laini yasiyo na chumvi (soft Water) na kuyasafirisha hadi sehemu ambako changamoto ipo. Unaweza kujiwekea malengo ya kuuza ndoo za lita 20 kwa idadi kuanzia angalu 50 kwa siku. Endapo gharama za kuyatoa maji hayo yanakopatikana na kuyafikisha kwa Wateja wako Let's say ni Tsh. 200 na wewe kuuza ndoo hiyo kwa Tsh 500 au 400 hivyo unauhakika wa kutengeneza Tsh. 10,000 hadi Tsh 15, 000 kwa siku. Kwa mwezi utaweza kujitengenezea kipato chako hadi Tsh. 450,000. Kumbuka hii ni pesa ambayo haukuwa nayo na haukujuwa utaipataje, hivyo shukuru sana Mungu kwa kaisi hiki hata kama ni kidogo, safari kubwa katika ujasiriamali siku zote ilianzishwa na safari ndogo.

Fursa namba 3: Uwakala wa Usafiri wa Mabasi yaendayo Mikoani.

Je, wewe ni kijana unayeishi mitaa ya Kigamboni, Mbagala, Temeke, Gongo la Mboto, Chanika, Tegeta na maeneo mengine ambayo humuwia uvivu msafiri kufika Ubungo siku moja au mbili kabla ya safari ili kujipatia tiketi.?

Kama ulikuwa hujui basi ngoja nikueleze. Miongoni mwa changamoto Kubwa ambayo watu huwafika ni ile safari ya kutoka baadhi ya maeneo niliyoyataja na kufika Ubungo siku moja au mbili kabla ya safari kwa ajili tu ya kufanya booking au kukata tiketi.

Hivyo basi anza kuchangamikia fursa hii kwa kuzungumza na Wahusika wa Mabus ya Mikoani ambapo utakuwa ukitoa huduma ya kumuhakikishia mteja kupata ticket yake akiwa eneo lake bila kufika Ubungo maana itampuzia usumbufu, kuokoa muda na gharama za kufika Ubungo. Hapo sasa kulingana na makubalilo na wahusika unaweza kutengeneza commission ya angalu Tsh 2000 kwa kila Ticket. Inamana ukifanikiwa kuuza Ticket 10 tu kwa siku utakuwa na Tsh 20,000 kwa siku ambayo ni Tsh 140,000 kwa wiki na Tsh 600,000 kwa mwezi. Fursa iliyoje hii.? Hata kama itakiwa ni Ticket 5 kwa siku maana yake utapata Tsh 300,000 kwa mwezi. Je, hii ni sawa na kukaa bure?

Fursa namba 4: Biashara ya Icecream

Je, unaishi karibu na mazingira ya shule ya wanafunzi wa shule ya awali na shule ya msingi?

Kama upo mazingira haya basi wahi uchangamkie fursa hii bila kuchelewa. Itakuhitaji kuwa na fridge nyumbani na kuwa na mtaji pengine usiozidi hata Tsh. 10,000 ili kutengeneza iceream kuanzia 200 ambazo utaziuza kwa bei ya Tsh 100 kila moja. Ukiwa na uwezo wa kuuza icecrem 200 kwa siku maana yake ni sawa na Tsh. 20,000 na kupata faida ya Tsh 10,000 kwa siku sawa na Tsh 300,000 kwa mwezi.

Fursa namba 5: Kusindikiza Watoto wa shule ya Awali na Msingi shuleni.

Changamoto nyingine katika jamii tunayoishi hasa kwa Wananchi wa kawaida (simanishi wale wenye uwezo wa kupeleka watoto wao kwenye shule za English medium) ni ile ya kuwafikisha watoto wao wa Awali na Wanaoanza shule za Msingi. Kwa nini hii ni fursa? Kwa sababu watu wengi kutokana na kuwa busy wanakosa muda wa kuwafikisha watoto wao mashuleni hasa wale wa awali na wanaoanza shule za msingi kwa darasa la kwanza katika maeneo ambayo watoto hao wanasoma shule zenye umbali kidogo kutoka kwenye makazi yao na wanahitaji kusindikizwa asubuhi na mchana wanaporejea.

Ufanye nini.? Jitambulishe kwa Mjumbe wako kisha Serikali za mitaa, uwe na makazi yanayoeleweka ikiwezekana uwe Mwenyeji wa maeneo hayo kisha chagua nyumba ishirini katika mtaa wako ambazo unadhani hii ni fursa kwako. Zungumza na Wanafamilia hao kuhusiana na adhma yako, thibitisha kwamba wewe ni Mwananchi mwaminifu na utafanya kazi hiyo kwa uaminifu wote. Katika hizo nyumba ishirini unaweza kupata nyumba 7 au 10 ambazo zitakubali na kubaliana nao malipo ya Tsh. 5000 tu kwa wiki hivyo kwa mwezi kwa kila familia ni Tsh 20,000 na ukiwa na familia 10 inamanisha utakuwa na Tsh. 200,000/= Je, hii si fursa unayoweza kuanza nayo mtaani kwako.?


Kumbuka nachojaribu hapa ni kuibua mawazo ya kibiashara ambayo mtu mwingine ameshindwa kuyaona na hivyo yakamwezesha kuchangamkia fursa hizi. Wakati huo tuki -asssume factors nyingine ni constant.
 
i know..fursa ndogo ndogo kwa baadhi ya mikoa hamna kulingana na nature ya jiografia ya eneo husika. mfano baadhi ya sehemu ya mkoa wa dodoma, tabora mbali na kilimo hamna fursa za namna hiyo, maeneo ya kanda ya ziwa kama geita, muleba, chato fursa iliokua inawezesha vijana wengi ni uvuvi haijalishi una mtaji au hauna ila uhakika wa kupamba na kifanikiwa ulikua mkubwa sana ila kwasasa sekta hyo imekuwa na vikwazo vingi kwa vijana, unapozingatia viwango na sera zilizo wekwa na wizara husika
 
Tunashukuru kwa Mchango wako. Ilitakiwa tangu mwanzo utoe mchango wa namna hii na siyyo tu kukomea kusema mambo yaliyosemwa hayawezekani. Kwa kujibu hoja zako ni kwamba, ni kweli unachosema ni logical lakini kilichoandikwa hakimanishi kitakuwa sawa kwa watu wote kwa mazingira yote. Zinafaa kwa hali ya eneo husika. Hata hivyo, kilichosemwa kwa kiasi kikubwa kinaweza kufanywa na watu wanaoendana na mazingira hayo. Hizo sehemu nyingine tuendelee kuzitafutia fursa kulingana na maeneo husika.Mchango wako pia ni muhimu, ni vema ukatueleza changamoto zilizoko huko ili tuzibadili na kuwa fursa. Karibu Jukwaani.
 
Fulsa ndogo ndogo zipo popote pale. Dodoma hakuna wachoma mahindi? Hakuna wauza zabibu? Vipi Masai wanao uza sime na sendos?

Mimi naishi geita nakupinga kua uvuvi ndio fulsa rahisi pekeake HAPANA KUBWA!!
kama kuna secta iliyoajiri vijana wengi geita, kahama, mara basi ni kilimo na madini (dhahabu). Mimi mwenyewe ni mchimbaji mdogo mdogo!

Mkoa wa geita asilimia kubwa hauna maji ya uhakika kwenye baadhi ya sehemu.
Kupitia maada hii tayari nimepata wazo la kuchimba kisima cha kudril. Lakini hapo hapo nikakumbuka vipo viwili na wenye navyo wanauza sio chini ya laki1 kwa siku na bei yenyewe ni sh 100 kwa ndoo ya Lita 20!!!

Pili najua mtaji sina!! Ila haraka nimepata wazo hapa sio lazima namimi nichimbe kisima changu bali naweza kununua hata sim tank kubwaa nikaliweka mtaa wa tatu kutoka kilipo kisima kisha nikawa naletewa maji kwa "water boozer".

Hiyo hela ya kununua tank bado sina!!! Lakini naweza kumtafta mwenye kisima ama ndg jamaa na hata rafiki nikamshauri anunue tank / matank nakuyaweka mitaa iliyo mbali na kisima kisha anilipe kama tukavyoelewana au anipe hata usimamizi.
 
Vyakuandika vibakie kuwa vya kuandika na uhalisia ubaki kuwa uhalisia.

Ulichokiandika ni sehemu ndogo sana kuna uhalisia.
 
Vyakuandika vibakie kuwa vya kuandika na uhalisia ubaki kuwa uhalisia.

Ulichokiandika ni sehemu ndogo sana kuna uhalisia.
Naona unachanganya vitu viwili, kuna fursa za biashara na changamoto za biashara. Fursa zinabaki kuwa fursa, na changamoto zinabaki kuwa changamoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…