SoC01 Je, UKIMWI sio janga tena kama ilivyokua mwanzo?

SoC01 Je, UKIMWI sio janga tena kama ilivyokua mwanzo?

Stories of Change - 2021 Competition

Dyran

New Member
Joined
Sep 16, 2021
Posts
4
Reaction score
4
UKIMWI sio neno geni kwa watu wengi Tanzania. Watu wengi wameufahamu ugonjwa huu kutoka mashuleni, kwa ndugu au jamii kiujumla. Hali hii imefanya hofu juu ya ugonjwa wa UKIMWI kupungua kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na miaka ya 1980 ambapo ugonjwa huu ndio ulikua unaingia nchini na watu hawakua na uelewa wa kutosha juu ya ugonjwa huu.

Kupungua kwa hofu juu ya ugonjwa huu, kunawafanya vijana ambao ndio kundi tegemezi katika ujenzi wa taifa kuwa katika hatari zaidi ya kupata maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI. Ripoti ya hali ya maambukizi nchini kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ya 2020: Karibia watu 72000 wanapata maambukizi mapya kwa mwaka, na kati ya hao, 40% ni vijana kuanznia miaka 15 hadi 25.

Niliongea na Wanchuo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ili kujua ni kwanini hasa bado vijana wanaongoza kwa maambukizi mapya? Vijana wote walionesha kuwa na uelewa juu ya nini hasa neno UKIMWI unamaanisha, na njia za kujikinga na ugonjwa huu wanazijua. Hivyo sababu zilijikita katika Nyanja zifuatazo;

Matumizi ya Kinga
Vijana wengi wanaelewa kuwa kinga zinasaidia kujikinga na virusi vya ukimwi lakini bado kwa kiasi kikubwa hawatumii. Zipo sababu nyingi za kutotumia, ikijumuisha kuaminiana; hapa vijana hawatumii kabisa kinga au wanatumia siku za mwanzo, pia wakitumia ni kwaajili ya kujikinga na mimba. Na dhana mbaya zilizojengeka katika makundi mengi ya vijana; Vijana wengi wamezungukwa na dhana kuwa wakitumia kinga zinapunguza radha ya tendo, hii inapelekea kuwapo kwa hatari ya maambukizi zaidi kwa vijana.

Kupima Afya
Vijana wengi wamekua wazito kwenda kupima afya zao. Hii inatokana na uoga ambao vijana wamekuanao, watu wengi wamekua wakigopa kupima kwani wanakosa ujasiri wa kuyakubali majibu endapo watakuta wameathirika. Sio hivyo tuu, bali pia vijana wengi hawapimi afya zao pamoja na wapenzi wao wapya, pia hawana utaratibu wa kupima mara kwa mara na wapenzi wao wa kila siku. Hii inapelekea vijana wengi kuwa katika hatari ya kupata maambukizi.

Michepuko
Kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja nayo ni sababu kubwa inayowaweka vijana kuwa katika hatari ya kupata maambukizi mapya. Vijana wa kiume wanajiingiza katika michepuko kutokana na tamaa za kimwili, migogoro katika mahusiano yao na ili kuonesha “UMWAMBA” (kutaka sifa kwa wenzao). Wakati huo vijana wa kike wakijiingiza katika michepuko kutokana na migogoro katika mahusiano yao, pamoja na tamaa ya mali na fedha. Hivi vyote kwa ujumla vinawaingiza vijana kwenye michepuko na kuwafanya kuwa katika hatari ya maambikizi mapya.

Elimu rika kutoka kwa wazazi.
Wahenga walisema “mototo umleavyo ndivyo akuavyo”. Vijana wengi wanakosa wasaa wa kukaa na wazazi wao na kujadili juu ya tabia za kingono na maambukizi ya UKIMWI. Hii ni kutokana na sababu mbalimbali ikiweo wazazi wanaamini sio vizuri kukaa na motto kujadili kuhusu mahusiano na watoto wao. Pia wazazi wanakosa muda wakutosha kukaa na wototo wao kwani wanatmia muda mwingi katika kutafuta pesa.

Sio kwamba watu wamesahahu athari zitokanazo na UKIMWI bali wanapuuzia tuu. Katika mahojiano ya jarida la TIME, Bwana Paul Slovic, Mwanasaikolojia kutoka Chuo kikuu cha Oregon alisema “linapokuja suala la kushughulikia tatizo, msukumo wa furaha yetu ya sasa na urahisi, hufanya sisi kutenda kinyume na kile tunachopaswa kufanya.”

Hili linaendana na hali halisi ya Watanzania kwani watu wengi wamekua wakipuuza umuhimu wa kujikinga na maambukizi ya UKIMWI kwani wanawaona waathirika wakiendelea kuishi kwa muda mrefu, hivyo hata uog juu ya Ugojwa huu unapungua. Tofauti na uoga uliopo sasa juu ya janga la UJIKO19 (COVID19) ambapo watu wanashuhudia nduguzao wakipoteza maisha, hivyo wanaweka kipaumbele katika kujikinga.

Kutokana hili ni muhimu kuwepo kwa vipindi vingi na matangazo kwenye njia zote za mawasiliano ( televisheni, Radio, mitandao ya kijamii na magazeti) ili kuendelea kukumbusha madhara na umuhimu wa kujikinga. Pia kuwepo kwa semina na warsha mbalimbali kwa makundi rika ili kuhakkikisha mitazamo inarekebishwa na kutengeneza jamii iliyo salama.
 
Upvote 7
Back
Top Bottom