Je, ukiona jina la mwanao limeshamiri kutumiwa na makahaba sheria zinaruhusu kubadilisha?

Je, ukiona jina la mwanao limeshamiri kutumiwa na makahaba sheria zinaruhusu kubadilisha?

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Mfano mwanao umempa jina, mara paah! jina kama hilo lina-trend kimalaya kutumiwa na makahaba na mashoga.

Sheria zinasemaje kuhusu kubadili hasa akiwa kaanza shule?

Au ni namna gani waweza li-brand ili lisimwathiri mtoto ukubwani?
 
Nenda mahakamani watashughulikia. Hilo linawezekana.

Kama bado ni mdogo na hajasajiliwa popote unaweza kubadili mwenyewe.

Naona utakuwa ulimwita mwanao D-ASS mkuu! (lol)
 
dmkali,

Kuna familia moja mtoto wao alipewa jina la Fataki. Si unakumbuka ile kampeni ya anti-mafataki kwa vibinti vya shule.

Dogo akawa anataniwa sana na watoto wenzie mtaani kwao na hasa p/school kwao. Dogo akakosa furaha, so ikabidi wambadilishie jina tu, no way.

Kama imekuwa shida we mbadilishe jina.
 
Kuna familia moja mtoto wao alipewa jina la Fataki. Si unakumbuka ile kampeni ya anti-mafataki kwa vibinti vya shule, dogo akawa anataniwa sana na watoto wenzie mtaani kwao na hasa p/school kwao. Dogo akakosa furaha, so ikabidi wambadilishie jina tu, no way.

Kama imekuwa shida we mbadilishe jina
Procedures zikoje kwa mtoto wa shule
 
Waiteni wanenu majina ya kibantu huwezi kuta yakitumiwa hovyo
 
Procedures zikoje kwa mtoto wa shule
Utaratibu ninaoufahamu ni mtoto na mzazi/mlezi kufika kwa hakimu wa angalau Mahakama ya mwanzo kwa lengo la kula kiapo cha kubadilisha jina mkiwa na kadi ya clinic na/au cheti cha kuzaliwa vya mtoto.

Baada ya hapo nadhani mtaenda RITA kubadilisha cheti cha kuzaliwa na baadae shuleni kwa mtoto kubadilisha jina.

Nafikiri haitamsumbua kama tu hajajaza ile form wanayojaza darasa la saba kabla ya kufanya mtihani wa mwisho. Inaitwa, nadhani TCM9 au TSM9 kama nimepatia.
 
Back
Top Bottom