flashback
New Member
- Jul 16, 2013
- 2
- 2
Wote wasioogopa kufeli katika ndoto zao ndio wale wafanikiwao, na wale wanaopanga vikali juu ya kukwepa hasara au kupunguza hasara za biashara zao ndio wenye mafanikio ambayo hata yawe machache lakini watakuwa na mwanya mkubwa wa kufahamu ni wapi hasa walichemka na waparekebishe ili msimu ujao wasianguke, lakini pia siri kubwa ya kushinda ni kujiamini, hebu jiulize ni kwanini leo umeweza kuielezea bidhaa yako vizuuri sana eti kisa sababu umependeza tu? hii ni kuonesha kumbe hata kama hujaoga lakini nguo ni nzuri na safi zinaweza kukupa kujiamini, sasa sipati picha mtu ambaye ana imani ya dini yake na anaifata kiukweli na ni imani ambayo inamfanya awe msafi nje hadi ndani ya mwili wake halafu isimpe ujasiri na kujiamini zaidi katika biashara yake. mwisho wa wan yooote haya nadhani wote tunaamini ya kuwa M/mungu ndiye mmiliki wa mali zote za ulimwengu huu na nikisema hivi namaanisha hadi hiyo akili yako.