Je ulishawahi kuingia hasra kati shughuli gani ya ujasiriamali?

Je ulishawahi kuingia hasra kati shughuli gani ya ujasiriamali?

Nyamgluu

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
3,160
Reaction score
1,726
Habari wakuu.
Pamoja na kuongelea mafanikio na mikakati yetu ya kujikomboa kimaisha kwa njia halali nimefikiri ni vyema pia tuhadisiane na kuelezeana kuwa ni biashara gani ulishawahi fanya na ilikupeje hasara?
Nafikiri hii itakua kama fundisho kwa wengine watakao taka kufanya biashara kama hio wajue kuchukua tahadhari ya nini chakufanya na nini sio cha kufanya.
Tukumbuke kujaribu na kupata hasara sio kushindwa bali ni kupata fundisho.
Lets share our experiences.
Mimi ntakuja na zangu lukuki tu.
 
si kila biashara ambayo mtu fulani alipata hasara kwamba kila mmoja atapata hasara.
 
Hata mimi naamini mafanikio mazuri ni yale ambayo awali yaligubikwa na misukosuko,shida na karaa...
acha nishuhudie hasara iliyomkuta mteja wetu mmoja katika biashara ya kuu...

Mwaka 2009 kuna mama mmoja alikodi pango (banda) kwa ajili ya ufugaji wa kuku wa layers....
Kiukweli aliwekeza pesa nyingi almost 7M,akaingiza kuku 900.Aliwahudumia vizuri kwa miezi mitano (laying period)..
Kuku walipoanza kuangusha mayai ya mwanzo,yule mama akabweteka na pesa,akasahau kuwa kuku wanahitaji huduma ya karibu...
Bahati mbaya pesa za kuwalisha zikamuishia,kuku wakapata magonjwa,hata kununua dawa ikawa shida..
Basi kuku wakaanza kufa polepole,yule mama akashindwa kudhibiti yale magonjwa kabisa,kuku wakaanza kufa kwa pupa;

Amini usiamini kuku walikufa mpaka wakabakia 56 tu...hao wsliobaki wote waligeuzwa qibrs
 
Habari wakuu.
Pamoja na kuongelea mafanikio na mikakati yetu ya kujikomboa kimaisha kwa njia halali nimefikiri ni vyema pia tuhadisiane na kuelezeana kuwa ni biashara gani ulishawahi fanya na ilikupeje hasara?
Nafikiri hii itakua kama fundisho kwa wengine watakao taka kufanya biashara kama hio wajue kuchukua tahadhari ya nini chakufanya na nini sio cha kufanya.
Tukumbuke kujaribu na kupata hasara sio kushindwa bali ni kupata fundisho.
Lets share our experiences.
Mimi ntakuja na zangu lukuki tu.

Yani maumivu tu mwana, usikumbushe unaweza fanya wengine wasithubutu
 
Ngoja nitulie nitaanza story moja baada ya ingine.
 
Nilishawahi pia kufanya biashara ya kuku wa kisasa wa nyama na hakika biashara ilikuwa nzuri kwelikweli yaani jinsi walivyokuwa wazuri mtaani nilikuwa nawafunika wafugaji wenzangu hauzi mtu mpaka wangu waishe wanunuzi wa masoko kuanzia kisutu, stereo mpaka mabucha ya namanga kote walinifahamu sasa siku ya siku nikaingizwa mjini na kijana wa kazi hamu sina kabisa nilipata hasara isiyo mfano
 
Katika safari ya ujasiriamali kuna changamoto nyingi sana na hazina mwisho ingawa zina mwanzo, that is why some time tunashauriwa kuwekea biashara zetu bima, kwa sababu kuna mambo mengi sana yanaweza kuhapen na kukurudisha mwanzo wa safari, na risk ziko za aina nyingi kuanzia za kushindwa kuuza, wizi, moto, ushindani kuwa mkubwa na kazalika.
Na hazina mwisho, ila kinacho wezekana huwa ni kuzi minmize tu

Na wewe kama mjasiriamali unajifunza kutokana na hayo unayo yapata, bila kufail huwezi grow, na hakuna mahali pengine popote pale pa kujifunza biashara kama kupitia fail zako, wakina SONY waliweza kusimama baada tu ya kijifunza kupitia kwenye kushindwa kwao,

Hivyo kufaile katika biashara kupo sana na ndo sehemu pekee ya wewe kujifunza, hili la sijui semina za ujasiriamali ni kudanganyana, utaweza kujifunza ujasiriamali kutoka kwako pekee
 
umenibarikije bestito
Nilikuwa nafanya biashara ya kuuza vikoi, vitenge, na kutengeneza batik,
ile biashara mwanzoni ilikwenda vizuri na nikapata faida ila baadaye likaja
wimbi la kuharibika na kukosa soko kabisa mjini hata kule nilikokuwa napeleka
soko likawa halipo niliingia hasara kubwa sana kwani vitenge nilinunua na vikoi
na batik nilitengeneza na malighafi ziliaharibika sana yaani nikikumbuka hivyo
nabaki nasikitika sana nimeshakubali kuwa kwenye biashara kuna kupata na kukosa pia (loss & profit)

Back
Top Bottom