Nikiwa kwenye mtihani wa taifa kidato cha pili, baba alisafiri kwenda kijijini ambako mama yake ambaye ni bibi yangu alikuwa anaumwa sana.Huyu bibi alikuwa ananipenda sana.
Bahati mbaya wakati anaumwa sana na kuzidiwa alikua anahitaji anione kabla hajafa. Kama ujuavyo mabibi wanavyopenda wajukuu kiukweli alimsihi sana baba anataka anione. Hivyo baba alikuwa anavutavuta mda kwa kumfariji ili nikimaliza pepa tu niende kijijini nikamuone. Maskini, Mungu nae ana mipango yake akamchukua kabla sijamaliza mitihani.
Baada ya kumaliza pepa nilienda msibani tayari akiwa ameshazikwa siku kadhaa zilizopita. Hali ile ilinihuzunisha sana kwani nilikuwa nampenda sana bibi yangu.
Watu wanapokaribia kufa huomba wapendwa wao wafanyiwe vitu flani. Mwingine anaweza taka apikiwe chakula Fulani, mwingine ataomba aletewe juisi, mwingine atataka nguo flani anayoipendaga. Vipi wewe ulishawai kwa bahati mbaya ukashindwa kutimiza ulichoombwa na marehemu awe rafiki, ndugu au jamaa?
Unapomkumbuka unapata hisia gani?