Dam55
JF-Expert Member
- Oct 8, 2015
- 5,641
- 11,958
ZITTO KABWE alifukuzwa CHADEMA kujiunga ACT Wazalendo.
MAALIM SEIF aliondoka CUF kujiunga ACT Wazalendo
BERNARD MEMBE alifukuzwa CCM kujiunga ACT Wazalendo
Je, majeruhi hawa wa kisiasa ndio chanzo cha umaarufu wa ACT Wazalendo?
Zitto Kabwe
Majina mawili ya wanasiasa ndani ya chama cha upinzani cha ACT Wazalendo, Bernard Kamilius Membe na Maalim Seif Sharrif Hamad yanatarajiwa kuidhinishwa na Kamati Kuu ya chama hicho kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano na Zanzibar leo Agosti 5 mwaka huu wa 2020 ili kushiriki Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba.
Majina hayo yana mvuto na haiba kisiasa nchini Tanzania, hali ambayo inaweka chama hicho katika mjadala wa taswira ya sasa na ile ya baada ya uchaguzi mkuu wa urais, ubunge na udiwani wa mwaka 2015 na kushuhudia kikiambulia nafasi moja ya kiti cha ubunge kutokana na ushindi wa Zitto Kabwe katika jimbo la Kigoma Mjini, pamoja na kupata madiwani na kuongoza Halmashauri ya Kigoma-Ujiji.
Hata hivyo kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka huu ACT Wazalendo kimeimarika kwa kiasi kikubwa na kuwa na wanasiasa wenye hadhi ya juu ambao wanaweza kutamba kwenye medani ya siasa na kuwashinda wapinzani wao badala ya kutegemea ushawishi na haiba ya mwanasiasa mmoja.
Mpaka mwaka 2014 ACT Wazalendo hakikuwa maarufu kisiasa nchini Tanzania. Taswira ya chama hicho ilibadilika mara baada ya kuwapata wanasiasa wawili wakubwa Zitto Kabwe na Profesa Kitila Mkumbo.
Upepo ukaanza kunukia uturi na kuwavutia baadhi ya wanasiasa wa ndani ya upinzani na chama tawala CCM kuelekea uchaguzi mkuu wa urais, ubunge na udiwani wa mwaka 2015.
ACT imetoka kuwa chama kichanga kilichokosa wanasiasa wenye majina makubwa na ndani ya miaka sita ya uhai wake katika siasa kimefanikiwa kuvutia wanasasa, wafuasi na wanachama.
Licha ya changamoto za ndani na nje zikiwemo kutojulikana, utata wa itikadi na falsafa ya chama ikihusishwa na CCM, wigo wa wafuasi kuwa hafifu na uhaba wa rasilimali hivyo kuwahitaji baadhi ya vijana kufanya kazi kwa kujitolea, hivi leo chama hicho kimepiga hatua mbele.