SoC02 Je, umeanza kuwaandaa watoto wako na mwisho wa human labour?

SoC02 Je, umeanza kuwaandaa watoto wako na mwisho wa human labour?

Stories of Change - 2022 Competition

ANAUPIGA MWINGI

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2022
Posts
389
Reaction score
757
Kazi za binadamu au human labour ni kazi zimekuwepo miongo na miongo mingi sana hapa Duniani. Ila kuna dalili kwamba zinaelekea kufikia mwisho muda si mrefu sana kutoka sasa.

Katika mkutano wa World Economic Forum walikadiria kwamna hadi mwaka 2025 ajaira million 85 Duniani zitachukuliwa na mashine na huku hadi mwaka 2030 kazi Millioni 800 zikichukuliwa na mashine, hii mana yake ni kwamba kazi nyingi sana zitafanywa na mashine au roboti.

Africa inatarajia kwamba hadi kifikia mwaka 2030 kazi zaidi ya million 35 zitakuwa zimepotea na kuchukuliwa na mashine.

Nchi masikini hatutaachwa nyuma na hii misuko suko, na isha anza kuonekana ambako kwwmye taasisi nyingi sana tunaona mashine mbali mbali, tunaona mageti Utomatic, kuna CCTV Camera, kuna ATM hadi za ku deposite pesa, kuna mashine nyingi sana ambazo tunaona kabisa zinachukua nafasi za binadamu.

Je wewe hapo unawaandaa vipi watoto wako na hili swala? Make inaweza kuwa furusa kwao pia, Make usije sema ni kazi ya Serikali kipindi wanakulamu Serikali haitakuwepo, je unawaandaa watoto ni hili vuguvugu?

Tunaona hata nchini swala la ajira linazidi kuwa gumu sana,nafasi 10 wanaomba watu elfu 50, ukiachana na maswala ya misuko suko ya kiuchumi lakini pia swala la techinolojia linachukua nafasi kubwa sana.

Mfano usha ona siku za hivi karibuni tangazo la ajira la Bank telers? binafisi sijaona muda mrefu sana, au usha ingia benki? kwa sasa Bank hazina Jam kabisa na madirisha mengi yamefungwa, au usha ona wakiendelea na ile speed ya zamani ya kufungua matawi mapya?

Wakati wa kuwandaa watoto ni sasa hasa kisaikolojia na kiakili pia,

1. Anza kuwapa picha kamili ya hali ilivyo na kwamba kazi za kuajiriwa zinaelekea mwisho na hata kama zitakuwepo ni kidogo sana, waandae watoto wajue wanachukue muelekea gani.

2. Acha watoto wajikite kwenye vipaji vyao vya asili walivyo pewa ba Mungu, yaani talent zao, kama una mtoto ana kipaji na still una mpeleka au kumtafutia mwalimu wa tuiotion basi una mchimbia kabuli na atakuja kukulaumu sana. Mtoto wako ana kipaji? Wakati ni sasa.

3.Watoto wajikite sana kujifunza kutatua changamoto na hii ndo kazi inayo lipa kwa sasa, Je mtoto wako ana weza tatua changamoto zipi? Au ni yule wa Baba nimepata A?
Watoto wajifunze udadisi utawasaidia sana, wajifunze jinsi wanaweza tatua vitu vya kijamii na sio kushinda kushabikia mpira, mtoto ana miaka 7 ni shabiki wa EPL.

4.Wajengee networking, Exposure na confidence, hizi zitawasaidia sana na hapa dio sehemu tuna kwama sana, Exposure inaweza kuwa msaaada kwao.

5. Kama kuna vitu vya binafisi vya wao kujifunza basi ni sasa hivi, acha kuwatafutia watoto walimu wa Tuiotions labda kama hao walimu ni Expert fulani wanawasaidia kutatua changamoto, ila kama ni kuwafundisha CIVICS na History basi unawapoteza.

Kosa kubwa ni kwamba wazazi wengi wanajua triend inako elekea kwa sasa ila kwa makusudi kabisa hawataki kuanza kuwaandaa watoto wao, still una mrithisha mtoto mambo yanayo elekea mwisho, mtoto ana rithi Division.

Matatizo ya ajira tunayo yaona si kwamba yatapungua siku za usoni na ni vile Serikali yenyewe haitaki kusema ukweli make na yenyewe inapaswa kuandaa raia kisaikolojia, hili tatizo la ajira linaenda kuwa baya kuliko ilivyo sasa hivi, ukweli usemwe bila kuficha.

Tuwaandae watoto na zama za mwisho za ajira za binadamu, ili wajindae na zama za mashine au computer. Wajiandae kuwa sehemu ya watu watako tatua changamoto.

Time is now
 
Upvote 11
Umeandika mambo muhimu sana, hili jambo huwa kinanikosesha amani, huwa nikiwaanhakia watoto wangu na wahurumia sana
 
Elon musk kwenye interview yake moja alisema in the future people will be paid the universal basic income kwa hyo watu wajiandae maana Artificial intelligence itachukua nafasi kama Qatar tu wataanza kutest new technology itakayobeba mpira kupeleka uwanjani.
 
Crane na winchi zimechukua Kazi za wabeba zege siku hizi lile rundo la kupandisha zege juu hakuna tena.
Wala vibarua wa kuvuna miwa, au pamba hawahitajiki tena,wala wapandaji na wapaliliaji mazao ni mashine tu
 
Crane na winchi zimechukua Kazi za wabeba zege siku hizi lile rundo la kupandisha zege juu hakuna tena.
Wala vibarua wa kuvuna miwa, au pamba hawahitajiki tena,wala wapandaji na wapaliliaji mazao ni mashine tu
Umeona, bado hatukashituka tu
 
Unashauri wanetu wasome fan gan? Ambazo n problem solving?
 
hujajibu swali
Nimesema angalua kipaji cha mtoto wako ba sio kumforce, yeye anataka au anapenda nini? Walio gundua vitu Dunin wengi walifanya vile wanavyo penda na hii ni hata kwenye sanaaa pia, anagalia mtoto wako uelekeo wake kama hataki kusoma usimlazimishe
 
Back
Top Bottom