Je, umewahi kukataa kutoa rushwa ili kupata stahiki yako?

Je, umewahi kukataa kutoa rushwa ili kupata stahiki yako?

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
UMEWAHI KUKATAA KUTOA RUSHWA.jpg


Kupata stahiki yako kwa njia ya haki na bila kutumia njia za udanganyifu ni msingi wa maadili na utawala bora katika jamii yoyote ile.

Katika dunia iliyojaa changamoto na mizani tata ya kimaadili, kukataa kutoa rushwa kunaweza kuonekana kama jaribio la “kuwakazia” wenye mamlaka, na mara nyingine tunajikuta tukikabiliana na changamoto kadhaa.

Kukataa kutoa rushwa kunaweza kusababisha athari tofauti kutegemea na jamii husika. Katika baadhi ya kesi, kukataa kutoa rushwa kunaweza kuleta matokeo mazuri kama vile kujijengea heshima binafsi na kuendeleza mabadiliko chanya ndani ya mfumo. Lakini pia, msimamo huo unaweza kusababisha kutengwa, kupoteza fursa, au hata “kuadhibiwa” kwa kwenda kinyume na mfumo uliopo.

Historia imejawa na mifano ya watu mashuhuri waliokataa kutoa rushwa licha ya mazingira magumu. Kwa mfano, Mahatma Gandhi aliendeleza amani na kutetea ukweli dhidi ya mfumo wa ukoloni, akipinga utaratibu wa rushwa ulioendelea kuzoeleka. Vilevile, wanaharakati wengi wa haki za kiraia wameonesha ujasiri wa kukataa kushiriki katika vitendo vya rushwa, wakiamini kuwa kufanya hivyo ndiyo njia pekee ya kuleta mabadiliko ya kweli.

Rushwa.PNG

Kukataa kutoa rushwa, hata hivyo, si uamuzi rahisi. Watu wengi wanaweza kujikuta katika hali ngumu ya kuchagua kati ya kukataa rushwa na mahitaji yao ya msingi au fursa za kuboresha maisha yao. Lakini pia, mfumo wa sheria na utawala katika nchi unaweza kuwa na mapungufu, hivyo kufanya kuwa changamoto kubwa kwa watu kushikilia msimamo wa kukataa kutoa rushwa.

Katika jamii inayoelewa umuhimu wa maadili na uwajibikaji, watu wanaokataa kutoa rushwa wanaweza kuchukuliwa kama waanzilishi wa mabadiliko chanya. Kwa kushikilia maadili yao na kusimama imara dhidi ya mfumo wa rushwa, wanaweza kuwa mfano bora kwa wengine na hata kuchangia kubadilisha mfumo wa kijamii kwa ujumla.

Inaeleweka kuwa kukabiliana na rushwa kunaweza kuhitaji ujasiri mkubwa na msimamo thabiti. Hata hivyo, hata kama athari zinaweza kuwa ngumu mwanzoni, uamuzi wa kuwa mwaminifu unaweza kuleta mabadiliko chanya ambayo yanazidi thamani ya faida za haraka.

Swali linalobaki ni: Je, umewahi kukataa kutoa rushwa kupata stahiki yako? Nini kilitokea baada ya kufanya hivyo? Unadhani wewe binafsi una mchango katika mabadiliko unayotamani kuyaona dhidi ya tatizo la Rushwa?
 
Niliwakatalia TANESCO na umeme wao, waliweka mazingira.. nikawaambia siku wakijisikia wenyewe kuja kufunga umeme waje
 
Kukataa kutoa rushwa ni gharama kubwa kuliko kutoa rushwa.

Ukikataa kutoa rushwa kujiokoa nchi hii ni upumbavu.

Ukikamatwa na Traffic, fine ni elfu 30 wakati rushwa hata Elfu 5 anachukua.

Ukikamatwa na mirungi, jela miaka 20 wakati unaweza kutoa rushwa elfu 50 ukawa huru.

Mifano ni mingi
 
Kukataa kutoa rushwa ni gharama kubwa kuliko kutoa rushwa.

Ukikataa kutoa rushwa kujiokoa nchi hii ni upumbavu.


Ukikamatwa na Traffic, fine ni elfu 50 wakati rushwa hata Elfu 5 anachukua.

Ukikamatwa na mirungi, jela miaka 20 wakati unaweza kutoa rushwa elfu 50 ukawa huru.


Mifano ni mingi
Hapo ni kweli una kosa unataka kujinasua. Sasa kuna ile situation kwamba inabidi upewe huduma ambayo ni haki yako ila unahitajika kutoa chochote kitu kwanza uhudumiwe. Mfano kumshtaki mtu polisi ni kweli mtu kakufanyia uhalifu ila ukienda kituoni polisi hawatoki hapo bila kuwapa hela ya mafuta ya gari
 
Nilishakataa kutoa rushwa, na Nilishaikataa rushwa. Kumbuka tu: Usikubali rushwa, wala kutoa rushwa.

Usiwe mnyang'anyi na usikubali kunyang' anywa.
 
Hapo ni kweli una kosa unataka kujinasua. Sasa kuna ile situation kwamba inabidi upewe huduma ambayo ni haki yako ila unahitajika kutoa chochote kitu kwanza uhudumiwe. Mfano kumshtaki mtu polisi ni kweli mtu kakufanyia uhalifu ila ukienda kituoni polisi hawatoki hapo bila kuwapa hela ya mafuta ya gari
Kwa Mfano hawana Mafuta, unategemea watumie pesa zao kushughilia matatizo yako?

Vituo vya polisi havina bajeti, lakini wanatakiwa kulisha mahabusu, kulipa Migambo na kupeleka mahabusu Mahakamani hapo unategemea nini?
 
Kwa Mfano hawana Mafuta, unategemea watumie pesa zao kushughilia matatizo yako?

Vituo vya polisi havina bajeti, lakini wanatakiwa kulisha mahabusu, kulipa Migambo na kupeleka mahabusu Mahakamani hapo unategemea nini?
Sasa ile budget ya Wizara ya Mambo ya ndani wanayo ombaga Bugeni inaenda wapi!!??
 
Nimeshawahi kujaribu kutoa chochote kwenye ofisi moja ya umma ili nipatiwe huduma kwa haraka lakini kusema ukweli ukiwa mbishi jiandae kupitia machungu ikiwamo foleni kali pamoja na kucheleweshewa huduma.

Kukataa kutoa rushwa kunahitaji moyo sana. Hata barabarani ukiamua ukatae kutoa rushwa jiandae kulipa faini zamoto moto.
 
Sasa ile budget ya Wizara ya Mambo ya ndani wanayo ombaga Bugeni inaenda wapi!!??
Ulishawahi kuona serikali inapeleka pesa kwa ground huko?

Unajua hata mtendaji wa kata na vijiji, pesa za kufanya kazi, Migambo, kalamu na stationery nyingi wanatoa mfukoni au mpaka wakamate mtu.

Kuna chemba ya maji taka ilivunjika huku, akaja DC kwa mtendaji wa kata akamwambia afunike hiyo chemba.

Mtendaji akamwambia hana fungu, DC akajibu kamata mtu yeyote mhalifu mtoze
 
Ndiyo, imewahi kunitokea mara kadhaa, na niliathirika na kitendo changu cha kukataa kutoa rushwa kwa kuwa sikuhitaji kunuua haki yangu.

Umefanya nikumbuke tukio moja, Mwaka 2015 Kuna mama yangu mdogo mmoja alikuwa mgonjwa ambaye kwa sasa hayupo tea kwa duia hii, alilazwa sana hospitali akapoteza tumaini la kupona.

Kuna mtoto wake 1 ameolewa ujerumani, akawa ameagiza mama yake apelekwe huko ili angalau akatibiwe Kwenye hospitali za huko. Akatuma nauli ya watu 2, yaani mama yake na mtu 1 wa kumpeleka mgonjwa.

Mtu aliyechaguliwa kuambatana na mgonjwa ni mimi, nikaanza kutafuta hati ya kusafiria ya kwangu, mama mdogo alikuwa nayo, nisumbuliwa mno Uhamiaji, kila ukienda wanasema hakuna mtandao, hali ya kuwa wengine wanahudumiwa.

Mwisho ikamuuliza mmoja ya watu walihudumiwa inakuwaje, akasema hapa bila kunyoosha mkono utamaliza miezi hupati, hebu muone yule dada pale mwambie uko na haraka, nikamfata kumwambia tu niliombwa rushwa ya 200,000 ili nipate kwa haraka maana ilikuwa ya haraka, nikakataa kutoa rushwa.

Nikawaambia familia nimekwama kupata hati akatafutwa mtu mwingine mwenye hati ya kusafiria ili ampeleke mgonjwa, kwa bahati mbaya siku ya safari mgonjwa akafariki asubuhi.

Labda nigepata mapema mgojwa angefika Ujerumani akapata matibabu angeishi, japo kifo ni mipango ya Allah.

Rushwa inatesa sana watu.
 
View attachment 2734592

Kupata stahiki yako kwa njia ya haki na bila kutumia njia za udanganyifu ni msingi wa maadili na utawala bora katika jamii yoyote ile.

Katika dunia iliyojaa changamoto na mizani tata ya kimaadili, kukataa kutoa rushwa inaweza kuonekana kama jaribio la “kuwakazia” wenye mamlaka, na mara nyingine tunajikuta tukikabiliana na changamoto kadhaa.

Kukataa kutoa rushwa kunaweza kusababisha athari tofauti, kutegemea na jamii husika. Katika baadhi ya kesi, kukataa kutoa rushwa kunaweza kuleta matokeo mazuri kama vile kujijengea heshima ya binafsi na kuendeleza mabadiliko chanya ndani ya mfumo. Lakini pia, msimamo huo unaweza kusababisha kutengwa, kupoteza fursa, au hata “kuadhibiwa” kwa kwenda kinyume na mfumo uliopo.

Historia imejawa na mifano ya watu mashuhuri waliokataa kutoa rushwa licha ya mazingira magumu. Kwa mfano, Mahatma Gandhi aliendeleza mwendo wa amani na kutetea ukweli dhidi ya mfumo wa ukoloni, akipinga utaratibu wa rushwa ulioendelea kuzoeleka. Vilevile, wanaharakati wengi wa haki za kiraia wameonesha ujasiri wa kukataa kushiriki katika vitendo vya rushwa, wakiamini kuwa kufanya hivyo ndiyo njia pekee ya kuleta mabadiliko ya kweli.

Kukataa kutoa rushwa, hata hivyo, si uamuzi rahisi. Watu wengi wanaweza kujikuta katika hali ngumu ya uchaguzi kati ya kukataa rushwa na mahitaji yao ya msingi au fursa za kuboresha maisha yao. Pia, mfumo wa sheria na utawala katika nchi mbalimbali unaweza kuwa na mapungufu, hivyo kufanya kuwa changamoto kubwa kwa watu kushikilia msimamo wa kukataa kutoa rushwa.

Katika jamii inayoelekea kuelewa umuhimu wa maadili na uwajibikaji, watu wanaokataa kutoa rushwa wanaweza kuchukuliwa kama waanzilishi wa mabadiliko. Kwa kushikilia maadili yao na kusimama imara dhidi ya mfumo wa rushwa, wanaweza kuwa mfano bora kwa wengine na hata kuchangia kubadilisha mfumo wa kijamii kwa ujumla.

Inaeleweka kuwa kukabiliana na rushwa kunaweza kuhitaji ujasiri mkubwa na msimamo thabiti. Hata hivyo, hata kama athari zinaweza kuwa ngumu mwanzoni, uamuzi wa kuwa mwaminifu kwa maadili yako unaweza kuleta mabadiliko chanya ambayo yanazidi thamani ya faida za haraka.

Swali linalobaki ni: Je, umewahi kukataa kutoa rushwa kupata stahiki yako? Nini kilitokea baada ya kufanya hivyo? Unadhani wewe binafsi una mchango katika mabadiliko unayotamani kuyaona dhidi ya tatizo la Rushwa?
Pongezi ziende kwa bwana YUDA ESKARIOTI
 
Niliwahi kuombwa rushwa ya ngono na TT kwenye treni ili anitoe third class anipeleke First class, hapo i baada ya kugonganishwa tiketi watu 2, nikawa nimekaa chini.

Alipopita kukagua tiketi akanikuta chini nikamwambia yule mtu kakalia siti yangu hataki kunipa alipokagua tiketi yake akakuta naye aayo kama yangu.

Akaniuliza una mizigo nikamwambia nina mkoba tu akasema nifate kuna behewa liko wazi ukakae.

Kufika mbele akasimama kwenye maungio ya treni akasema pole sana binti ngoja nikutafutie sehemu nzuri ukae ufurahie safari, nikasema loh Mungu kaniona mweee,

Tukaenda mpaka kufika kwenye mabehewa ya first kwaza nikastuka kidogo kimoyo moyo nikasema kutoka third hadi first kweli nina bahati.

Akafungua chumba akasema nakupa hiki chumba cha first ila inabidi tulale wote mpaka tukifika Dodoma nitakuacha peke yako.

Nikamwambia siwezi, akasema sasa uadhani anaruhusiwa mtu kuja huku kutoka kule kwa walalahoi, kwani unaogopa nini nimekupa hadhi halafu unakataa nikamwambia mie nipe siti tu ya kawaida akajibu umeiona tangu tumepita kule, akawa mkali ghafla.

Akasema nitaita askari wakukamate kwa kufika huku kwa kuwa huruhusiwi, akaanza kunitisha, nikachomoka mbio na woga wa kuruka kwenye maungio ukaisha nilikuwa navuka maungio kama napita ndani ya behewa, nikatafuta kauvungu kazuri nikalala zangu chini ya siti za watu hadi nikafika.
 
Kuna hakimu Mmoja wa mahakama ya mwanzo alinionba nimpe laki tatu nilipokataa akatoa hukumu ya Mimi kushindwa kesi! Nikamwabia nakata rufaa kimbembe ikawa kutoa nakala ya hukumu alinisumbua japo mwisho wa siku nikasaidiwa na hakimu wa wilaya na nikashinda Ile kesi.
 
Back
Top Bottom