Je, umewahi kupatwa na tukio lililohatatisha maisha yako ukiwa na miaka 0-3, ambalo baada ya kusimuliwa lilikupeleka mbali kihisia?

Stephen Ngalya Chelu

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2017
Posts
8,252
Reaction score
18,335
Hivi majuzi mama alinisimulia tukio ambalo hakuwa amewahi kunisimulia hapo kabla na likanifanya nishikwe na baridi ya huzuni na hofu na nikawaza mengi sana.

Iko hivi....

Nilikuwa nina mwezi mmoja tu tangu nizaliwe ambapo tukio hili likitokea. Siku hiyo ilikuwa siku ya kwanza mimi kutolewa nje (sebuleni) tangu nizaliwe. Mama alinichukua na kunipakata akiwa amekaa sebuleni. Katika hali isiyo tarajiwa, alikuja mwanamke mmoja akiwa anakimbia na kuingia sebuleni alipokuwa amekaa mama. Mwanamke huyo alikuwa anafukuzwa na mumewe ambaye walikuwa wanagombana muda huo.

Mwanaume huyo alikuwa ameshika kafimbo kanene kafupi wakati anamfukuza mwanamke wake. Sasa huyo mwanamke akawa anajizungusha alipokuwa amekaa mama ambaye alikuwa amenipakata mimi wakati huo. Wakawa wanazungushana hapo, mke anajikinga kwa kumzunguka mama, na mumewe anazunguka akiwa ameshika fimbo anataka ampige mkewe. Mama akawa amepanic, anajaribu kunyanyuka anashindwa kwa kuhofi a usalama wa mtoto(mimi) akabaki anapiga kelele tu huku akiwa anajaribu kunikinga nisidhurike.

Sasa kitu cha hatari ni kuwa, mzee alipoona kuwa hatimizi lengo lake la kumbutua mkewe, akaamua kurudha ile fimbo ili ampige mkewe. Kwa mstuko mama alinyanyua mkono kwa hamaki kunikinga maana ilikuwa imenilenga kabisa kichwani. Kwa kitendo cha yeye kunyanyua mkono aliiparaza ikapita sentimita chache sana kutoka usawa wa kichwa changu, na ikamkosa mlengwa pia(mke wa huyo mzee). Kwa maelezo ya mama, anadema laiti kama ile fimbo igemgonga sawasawa mkononi, mkono wake ungweza kuvunjika mara kadhaa, sasa imagine ingekipata kichwa cha mtoto wa mwezi mmoja!!

Baada ya tukio lile, yule mwanamke alikimbia nje na mumewe akamfuata huko na inadaiwa hawakusikia tena kelele za watu wakigombana tena. Ni kama ugomvi ulisha pale tu. Mama alilia sana siku hiyo, imagine first born anapitia katika hatari kubwa kama hiyo katika siku za awali tu za maisha yake!!!!

Kuna mengi sana ya kuhatarisha maisha nimeyapitia kitoka umri wa miaka 0-4, hadi wazazi hawaamini kama nimekua na nikiwa na afya njema kabisa.

Tuwapende na kuwaheshimu wote waliotupigania wakati sisi tukiwa hatujui hili wala lile.
 
Tulikuwa tuna mchezo wa kuogelea kwenye karo la kuhifazia maji.lilikuwa na kama futi7 mi na mwenzangu tulikuwa yapata miaka 10 tulikuwa nayo!!bwana wee siku hiyo tukakuta limejaa maji top na tuna ham ya kuogelea na hakuna noma.si nikadaivu ndani nilikunywa vikombe vya kutosha.kila nikipiga kelele narudishwa chini.yule mwenzangu akakimbia kwa hofu.mungu mkubwa nilipoibuka ya mwisho ambayo ningezama ndio mazima nikajiwahi kushika kingo.hadi leo nikikumbuka natetemeka
 
Nilipokua mdogo sikuwahi patwa na maswahibu

Ila nilipokua shule ya msingi najielewa nilitaka kuzama nilipokua naogelea mtoni
 
Kwa ujumla nimewahi kupata ajari kubwa tatu za Pikipiki, nikaona isiwe kesi, uza pikipiki nunua gari ambapo mpka sasa nshapatanalo ajari mara nne
(Adui pombe nahusika).
Thanks God mpaka sasa niko salama though mim na adui we have not yet divorced
 
Nilikuwa mchanga kabisa, Mama na baba yangu walikuwa kazini. Mama yangu aluvyokuja mchana nyumbani, akanikuta nimefunikwa makanga na nimeachwa kwenye kitanda changu, huku house girl kaacha kabandika maharagwe kwenye jiko la umeme. House girl aliniacha. Hii kitu Mama yangu kanisimulia juzi tu. I was shocked. Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu.
 
Ngoja nikienda home nikadadisi dadisi na mimi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…