JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Unadhani ni nini kinasababisha tatizo la dawa za kupunguza na kuongeza mwili (Kujenga Shape) na vipodozi vyenye madhara kuendelea kuwepo nchini licha ya madhara yake kujulikana? Unapendekeza hatua gani zichukuliwe ili kuondoa changamoto hiyo nchini?
Pia soma: Umeshawahi kununua dawa za kupunguza tumbo, kuongeza shape au nguvu za kiume mtandaoni? Unajua dawa hizo zimechanganywa na nini?
Ili kufahamu zaidi, usikose kushiriki katika Mjadala ulioandaliwa na JamiiForums kupitia XSpaces, utakaohusu athari za Matumizi ya Vipodozi na Dawa za Kuongeza au Kupunguza Mwili zinazotengenezwa na kuuzwa kiholela
Ni Alhamisi Julai 18, 2024 Saa 12:00 Jioni hadi 2:00 Usiku
Kushiriki mjadala katika XSpaces bofya hapa x.com
===
Athumani Kissumo, TBS (Afisa Udhibiti Ubora - TBS) Vipodozi ni Kitu chochote kinachotumiwa kupaka, kunyunyiza, kufukiza au kutumika mwilini kwa lengo la kusafisha, kujiremba au kubadili mwonekano kwa kung'aa au kuonesha taswira ya kuvutia kwa ngozi bila kukusudia kutibu au kuzuia ugonjwa. Lengo kubwa ni kujiremba bila kubadili maumbile ya mwili, kutibu au kuzuia magonjwa.
Kuna mifumo mingi ya Udhibiti wa Vipodozi ambayo imewekwa na Shirika kwa Mujibu wa Sheria
Majukumu ya Shirika katika Udhibiti yanahusisha Kupanga Viwango, kudhibiti Ubora (Ukaguzi wa Bidhaa kwenye Mipaka, Nchi zinapotoka na zinapoingia) lakini pia lazima Vipodozi viwe vimesajiliwa. Hii ni kwa Vipodozi vinavyotoka nje.
Kwa vipodozi vinavyotengenezwa nchini huwa tunatembelea Viwanda, ambapo tunakagua na pia kama bidhaa zinakidhi vigezo tunatoa Leseni
Pia, tunatembelea masokoni, kule tunafanya ukaguzi ambapo tukikuta bidhaa hazijakidhi viwango zinaondolewa sokoni na kuteketezwa.
Dkt. Mashili (Mtaalamu wa Fiziolojia ya Homoni na Mazoezi - MUHAS): Katika Dawa ambazo zinatumika vibaya ni 'Steroids' na vipodozi vyenye 'Steroids' vinaongoza kwa kutumika vibaya
'Steroid' ni homoni muhimu katika mambo ya Uzazi na 'sexuality'. Matumizi yaliyozidi ya vipodozi vyenye 'Steroids' husababisha mwili kushindwa kutengeneza 'Steroids' wenyewe.
Kuna Dawa mtu anapaka anafikiri anaongeza Makalio kumbe anaongeza Mafuta
Tunajua athari za Mafuta Mwilini, sawa matokeo yanaweza kuonekana lakini huko ni kuzidiwa na Mafuta Mwilini hali inayoweza kuongeza Magonjwa kama ya Kisukari.
Ukizungumzia Changamoto za Uzito uliokithiri Tanzania, kati ya Watu 10, Wanne wanauzito uliokithiri. Kati ya Watu 100, Watu 30 hadi 40 wanauzito uliokithiri
Pia, Wanawake wanakuwa na tatizo la Uzito uliokithiri kwasababu ya Homoni n.k
Emmanuel Alphonce (Meneja Ukaguzi na Udhibiti wa Dawa - TMDA): Mtu akisema ametumia Dawa fulani akapata madhara tunafuatilia na tunapobaini ni kweli tunafanya utafiti kujua ni Watu watu wangapi wameathirika na Dawa hiyo, huwa kuna fomu tunawapa wanajaza ili kujua ukubwa wa athari
Pia, kuna maamuzi ya kiutawala kama kufanya uchunguzi wa kimaabara au kuzuia matumizi ya Dawa husika.
Kama Mtu ameathirika Mwili kutokana na Vipodozi, tunashirikiana na TBS kujua ni kipodozi gani kimetumika na pia ni athari gani Mtu amepata.
Glory Benjamin, Afisa Lishe/Mtafiti – TFNC): Takwimu kuhusu dawa za kupunguza uzito kiholela bado ni changamoto Nchini lakini inashauriwa kuwa unapotaka kutumia Dawa za kupunguza uzito ni vizuri ukazingatia ushauri wa kitaalamu
Kuna changamoto ambazo zinaweza kujitokeza bila kujali umetumia Dawa iliyosajiliwa au ambayo haijasajiliwa, hiyo ni kwa kuwa ni matumizi ya Dawa yanahitaji mwongozo wa Kitaalamu.
Matumizi mengi ya Dawa za kupunguza uzito huwa yanakuwa ya muda mfupi kutokana na changamoto kama za watumiaji wengi kutozingatia ushauri wa Kitaalamu.
Pro. Willbroad Kalala, Mkuu wa Kitivo cha Famasi – KIU): Niliwahi kufanya utafiti kuhusu vipodozi vya kung’arisha Ngozi
'Steroids' ni viambata vinavyotumika katika kung’arisha Mwili, moja ya madhara yake ikitokea mhusika akatakiwa kufanyiwa oparesheni inakuwa ngumu kwa kuwa ngozi inakuwa nyembamba kutokana na Dawa zilizotumika.
Wakati tunafanya utafiti kuhusu matumizi ya vipodozi tuligundua kuwa tatizo ni ushawishi wa Wanaume.
Wanaume wengi wanapenda Wanawake weupe na hali hiyo imekuwa ikisababisha Wanawake wengi kutaka kutumia nguvu kubwa ya kujichubua bila kujua madhara ya kile wanachokifanya.
Kuna umuhimu mkubwa wa kutoa elimu kwa Jamii kuhusu matumizi ya vipodozi vya kuongeza weupe mwilini.
Wananchi wanatakiwa kuelezwa na ikiwezekana Wanaume waambiwe weupe sio urembo, ili wapunguze presha kwa Wanawake.
Inatakiwa kutambulika kuwa Binadamu sio kama model ya Gari, kitu ulichotumia wewe sio lazima kimfae Mtu mwingine.
Kila Mtu anakuwa na vitu vyake mwilini, unaweza kutumia kwa kumuiga Mtu lakini kumbe unajiharibia.