JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Sheria ya Mikataba inabainisha kuwa wakati ambapo mkataba unakuwa umevunjika, mhusika ambaye ameathirika na uvunjwaji huo anastahili kupata fidia ya hasara iliyojitokeza kutoka kwa aliyesababisha ukiukwaji wa mkataba huo, au fidia iliyosababishwa na kujitokeza kwa mambo fulani ambayo ni ya kawaida katika uvunjaji wa mkataba, au ambayo wahusika walijua walipofanya mkataba kuwa yaweza kutokea iwapo mkataba utavunjwa.
Aidha iwapo mkataba umevunjika, kama kiwango cha fedha kimetajwa kwenye mkataba kuwa ndio malipo
yatakayofanywa kwa kuvunjwa kwa mkataba, au kama mkataba umeelekeza adhabu nyingine yoyote, mhusika anayelalamika kuhusu uvunjaji huo unastahili fidia inayoeleweka isiyozidi kiwango kilichotajwa au kama itakavyokuwa, adhabu iliyowekwa.
Upvote
2