Je umri gani mzuri kwa watoto kutaihiriwa, nina mtoto wa miezi 4 anafaa?

Je umri gani mzuri kwa watoto kutaihiriwa, nina mtoto wa miezi 4 anafaa?

Tena umechelewa, sisi huwa tuna-watairi watoto zetu kabla ya kumaliza miezi miwili.

Kama upo Dar. Mtaa wa Swahili na Kariakoo kwenye jengo la club ya PAN Africa kuna Dr. Juma (hayuko kwenye mgomo). Huyu ni mtaalaam humchukuwa chini ya dakika moja tu kamaliza kazi.
 
Utamumiza bure bora hata afike mwaka mmoja kwa mtazamo wangu
 
Kaka hujachelewa sana, mtahiri haraka iwezekanavyo, na kidonda kikipona itabidi uwe unampiga massage kila asubuhi, nna uhakika akifika primary school watoto wenzake watamkimbia . nadhani umenielewa... Lol


Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD
 
nenda mapema maana ukichelewa ataanza utundu na atakua anajitonesha mara kwa mara. Ni kweli kabisa dokta jumaa ni mtaalam na mzoefu sana. Halafu ni vizuri kumfanyia kipindi hiki cha baridi maana atapona upesi.
 
Hayo ni matesy kwa mwanao subiri akue mpaka ajitambue na aweze kuwa na uvumilivu!
 
Mwanagu wa kwanza alikuwa na miaka miwili nilivyomtahiri. Wa pili sijamtahiri ingawa ameshatimia miaka miwili. Kitaalamu hakuna muda maalumu. Ila nilivyomtahiri mtoto wa kwanza nilimdadisi doctor kuhusu suala la muda akasema hakuna muda maalumu ila yeye watoto wake anasubiri wakue. Maana yake wangu wa miaka miwili alikuwa mdogo. Kumbuka kuwa mtoto atapigwa nusu kaputi.

Ila kuna pia imani kuwa mtoto akitahiriwa akiwa mchanga basi atakuwa na kibamia. Hii inazungumzwa sana ndio maana sikutaka ku risk nikasubiri mwanangu afike miaka miwili.

Na ukiangalia sana hii fashion ya kutahiri vichanga ni mpya hivyo atujuhi faida na hasara zake na wataalamu wenyewe hawaju wanaangalia maslahi; kaka zangu wote walitahiriwa wakiwa na akili zao timamu.
 
Back
Top Bottom