ndo maanake!NO FUND AVAILABLEHivi Tanzania kuna mpango wa kuwapatia wananchi walio nje ya nchi nafasi ya kupiga kura? Nchi nyingi wanafanya hili. Au siye ndiyo "no funds available" ?
Duuuh, ila kweli nilishajisahau! Hebu ngoja nikachungulie kwenye sanduku langu kama bado ipo!Je, una hati ya kupiga kura 2010?
Hati ya kupigia kura tunayo. Bahati mbaya wakati wa uchaguzi wengi wetu huwa tuko huku ughaibuni 'tunabeba maboksi' na hakuna utaratibu wa kuwawezesha walio nje kutimiza haki yao kidemokrasia, matokea yake tumewaachia watu wengine watuchagulie viongozi na imebidi tuwakubali kwani 'anayemuoa mama ndiye baba'Kama unayo:
1. Ihifadhi vizuri kwenye sefu!
2. Katu usikubali kuwauzia mafisadi!
Na kama huna:
1. Jiandikishe upate hati yako!
2. Kamwe usikubali kutojiandikisha!
---------------------------------
Rejea 'Waraka wa Uchaguzi wa Kuli: Yana Mwisho Haya'!
Zingatia Wito wa Mwanakijiji: '2010 - Ni Mwaka wa Uhuru Wetu'!
Wabeba maboksi rudini nyumbani mjiunge na makuli wenzenu kupiga Kura ya Uhuru!
Hivi Tanzania kuna mpango wa kuwapatia wananchi walio nje ya nchi nafasi ya kupiga kura? Nchi nyingi wanafanya hili. Au siye ndiyo "no funds available" ?
Mkuu Campanero, hii avatar yako inafanana sana na Mzee wa 'Vijisenti' vipi mnaweza kuwa na uhusiano?Awamu ya kwanza ya uandikishaji ilipita. Walisema watakuja kwenye pango langu kunipangia siku ya kwenda kujiandikisha. Ila sikuwaona. Awamu ya pili nasikia inakaribia. Tusikubali itupite hivi hivi. Kupiga kura ni haki yako. Pia ni wajibu wako. Piga kura. Na usimpigie fisadi.
Mkuu Campanero, hii avatar yako inafanana sana na Mzee wa 'Vijisenti' vipi mnaweza kuwa na uhusiano?
Nimefurahishwa sana na mwamko huu wa wana JF na kura ya UHURU 2010. Mie ninakoishi nimefanikiwa kuwahamasisha wananchi wenzangu kuandaa kabisa kadi zao kwa ajili ya uchaguzi huu. Nimewasisitizia kwamba itakuwa kura ya UHURU wa kweli ili wasije wakarudia makosa na kujitia kitanzi cha mafisadi. Hamasa ni kubwa kwa kweli...
kama unayo:
Na kama huna:
1. Jiandikishe upate hati yako!
2. Kamwe usikubali kutojiandikisha!
---------------------------------
rejea 'waraka wa uchaguzi wa kuli: Yana mwisho haya'!
zingatia wito wa mwanakijiji: '2010 - ni mwaka wa uhuru wetu'!
Samahani kuuliza siyo ujinga.
Hivi kuna tofauti gani kati ya hati na shada ya kupiga kura?? Maana navyofikiria ni kuwa hati ni voters registration card. Lakini huwa nachanganyikiwa ninaposikia kuwa CCM wamenunua shahada za kupiga kura hiyo jamaa hawawezi kpiga kura.
Narudia tena kuuliza siyo ujinga. Mambo ya daftari la kudumu wakati linaanza nilikuwa nje na sijaweza kupiga kura chaguzi tatu zilizopita kwa vile hawataki kutuwekea utaratibu na sisi wabeba mabox tupate haki yetu ya kuchagua.