Je, Una Hofu na Kifo? Je, unahisi Roho huumiza mwili itenganapo na Mwili?

Je, Una Hofu na Kifo? Je, unahisi Roho huumiza mwili itenganapo na Mwili?

Kazetela

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2016
Posts
1,714
Reaction score
1,642
Kifo ni kitendo cha kutokwa na uhai yani (kufariki) kwa kiumbe hai. Ni mechanism ambayo kiumbe hai yeyoye lazima akipitie. Kiumbe yeyote aliye 'hai' basi siku moja uhai utamuondoka nae atapoteza maisha yake. Mwili wake utakuwa si kitu tena na kila kiungo kifanyacho kazi mwilini husimama(hukoma) maramoja na ndio mwanzo wa kuoza,kuliwa na wadudu na kuishilia udongoni.

Kifo ni ahadi ya kweli ambayo Mwenyezi Mungu aliitoa kwetu Sisi wanadamu na ilinukuliwa katika maadiko matakatifu Yani Qur'an na Biblia, Sisi wanadamu lazima tufe, lakini hii haituhusu Sisi wanadamu peke yetu Bali kila kiumbe hai lazima aipate na ni hakika tupu. Kiumbe hai si matakwa yake kukizuia bali hii Hali hutokea tu kwa nguvu ya asilia na huwa ghafla been' vuu ama unakiona kabisa kwamba hiki hapa hii inatokana na aina ya kifo chenyewe na mazingira.

Kiumbe hai huwa hana ujanja ikiwa kifo kimemkaribia na kama kipo mbele yake.
Kwahiyo kabla ya kifo kukukumba basi kuna Hali ya kukubaliana nacho dhahili kama negotiation Flani hivi, nafsi inakuwa haijuti na unakuwa umeridhia kabisa kwamba, “sasa naondoka” ndio unakubali na maramoja shwaaa unaaga dunia.

Hakuna maumivu yoyote ambayo hutokea katika Ile harakati ya roho kutengana na Mwili ni kama vile unavuta hewa na kuitoa tu. Kuna Yale maumivu mfano umekatwa na kitu hivyo hupelekea maumivu lakini kwa kifo hicho kitu hakuna.

Huwa zinaonekana picha za video zikiwaonyesha watu wakihangaika wakati wa kukata roho kanakwamba Yani anaekata roho anaumia, hiyo siyo kweli, watu hao huwa hawaumii bali hutapatapa kwasababu ya roho kuondoka.

Kifo ni kitu Flani soft Sana na ni njia ya kwenda mahala pengine kwaajili ya maisha mengine kiroho zaidi,Ndio maana kuna msemo usemwao,"duniani tunapita" ndio 'tunapita' ikimaanisha endapo ukitaka kuufungua mlango mwingine wa ulimwengu mpya, basi sharti ufe kimwili.

Basi ndipo mlango wa ulimwengu mpya hufunguka nakujikuta huko, na ndio sehemu ya maisha mengine mapya tofauti na hapa Duniani.

Kifo ni soft mno ni kama kushika usingizi unapotaka kulala. Je ni Nani anaejua muda wa kushika usingizi? Hakuna Bali huwa tunautengenezea mazingira tu ili uje utupitie.

Basi kama usingizi utuijiapo, ndivyo hivyo hata kifo hututokea. Jiulize je ukishikwa na usingizi hukuumiza? Je kimwili, ama kinafsi? Jibu ni hapana Yani ni mtelezo tu shwaaaaa unajikuta umeshalala.

Ndivyohivyo hata kifo kilivyo, Yani ni soft mechanism tu ambayo kufumba na kufumbua, unajikuta upo mahala pengine katika ulimwengu mpya mwingine wa kiroho. Unajitambua lakini hujigusi ukagusika, unalia machozi hayatoki, unatembea pasina hatua kuvuta, Yani kilakitu kinakuwa kipya, hakuna uchafu, hakuna njaa, wala kuhisi joto. Naam huo ndio utakuwa ulimwengu mpya mwingine ambao utaishi nao milele mpaka Yule aliyeiumba roho yako afanye kulingana na mapenzi yake.

images%20-%202023-03-17T130119.549.jpg
 
Kifo ni kitendo cha kutokwa na uhai yani (kufariki) kwa kiumbe hai. Ni mechanism ambayo kiumbe hai yeyoye lazima akipitie. Kiumbe yeyote aliye 'hai' basi siku moja uhai utamuondoka nae atapoteza maisha yake. Mwili wake utakuwa si kitu tena na kila kiungo kifanyacho kazi mwilini husimama(hukoma) maramoja na ndio mwanzo wa kuoza,kuliwa na wadudu
Habari
Ulishawahi kufa?
 
Binadamu wengi hatuogopi kifo bali tunatamani tuwe na mwisho mwema na sio mwisho wa mateso makali
 
Back
Top Bottom