Je, una tatizo la Mimba kuharibika?

Je, una tatizo la Mimba kuharibika?

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
Hii Ni maalum kwa wanawake wote ambao wamekuwa wakishika ujauzito na huwa zinaharibika kabla ya muda wake.

Sasa Leo tumewaletea kaujanja ambako hakatumii gharama kubwa katika kulidhibiti tatizo Hilo.

Huu unaouona pichani Ni mchicha, lakini siyo tu mchicha Ila Ni mchicha bwasi.

Huu mchicha bwasi tumekuwa tukiutumia kila siku katiku katika vyakula vyetu, lakini Ni moja Kati ya mimea ambayo Ina kazi kubwa Sana katika kuulinda na kuukuza mwili wako.

Kwanza acha nikupe kaujanja kwanza Kisha tutaendelea kuuchambua kidogo.

Kama umekuwa na tatizo Hilo ambalo tumelielezea hapo juu ya kushuka mimba Kisha inaharibika Basi fanya haka kaujanja.

Chukua majani ya kijani ya huu mchicha bwasi, yajae kwenye kiganja chako Cha mkono, Kisha yachemshe na unywe asubuhi kabla ya kula chochote na usiku kabla ya kwenda kulala.

Lakini fanya hivi baada ya kuhisi au kutambua kwamba umebeba ujauzito, hapo utajionea maajabu.

Kwa Nini tumeuchagua huu mmea wa kuitwa mchicha bwasi katika tiba yetu hii, Ni kwa sababu hizi zifuazo.

Huu mchicha majani yake una wingi wa mkusanyiko wa vitamin B, mfano folates, riboflavin, niacin, thiamine, Vitamin B6, na nyinginezo zote zinapatikana kwenye majani ya huu mchicha.

Ambazo hizo zote zinamsaidia au zipo kwa ajili ya kumlinda mtoto aliye tumboni kiafya ya akili na kimwili.

Lakini pia huu mchicha una boost Kinga za mwili maana una vitamin C za kutosha pia.

Una vitamin A za kutosha kwa ajili ya kumlinda ngozi na afya ya macho kwenye kuona.

Pia una calories chache Sana kwa ajili ya kuzuia unene usio na faida.

Pia huu mmea una vitamin K, kwa ajili ya kulinda na kufanya mifupa iwe imara.

Pia una potassium za kutosha kwa ajili ya kudhibiti kiwango Cha mapigo ya moyo mwilini.

Pia una protein za kutosha, una calcium za kutosha, una lysine, na pia husaidia katika suala zima la mmeng'enyo mzuri wa chakula.
 
1716104579217.jpg
 
Back
Top Bottom