Je, unaamini kuwa uchawi upo?

Hapo kwenye elimu ni zimwi, una point lakini ni kama umeshindwa kuiweka bayana pointi yako, but I can feel it, you have something there meaningfully, labda ulitaka kuzungumzia mifumo mibovu ya elimu,labda, mifumo inayokaririsha tu watu na kutotoa fursa ya watu kuweza kufikiri, mifumo ya elimu ambayo inapima ufanisi wa elimu kwa kuangalia ni wangapi wamepata grade gani, bila kujali wanaelewa nini, labda unamaanisha hicho, lakini ukisema tu "elimu" ni zimwi, unakuwa umegeneralize sana.

Kuhusu uwepo wa imani za uchawi Ulaya na Marekani, naomba Nyani Ngabu na Kiranga au EMT watusaidie.
 
Last edited by a moderator:
Shida moja hapa ni kwamba watu wanachanganya uchawi, ulozi, mazingaombwe uganga wa kienyeji! hivi vyote ni vitu vinavyofanana lakini pia vikitofautiana
Msaada please;
Nisaidie tofauti kati ya uchawi, ulozi na uganga wa kienyeji.
 
Eiyer

Vyote ambavyo sayansi imeshindwa kuvithibitisha vipo?
 
Last edited by a moderator:
Msaada please;
Nisaidie tofauti kati ya uchawi, ulozi na uganga wa kienyeji.


Hakuna tofauti mkuu

vyote vinatumia nguvu za Giza zisizoonekana..

Na zinaweza kuthibitika kwawewe kuamua tu kushiriki kimojawapo
 
Msaada please;
Nisaidie tofauti kati ya uchawi, ulozi na uganga wa kienyeji.

Hebu andaa maswali yako yote halafu tukutane live hii mijadala inahitaji uwanja mpana nakaribisha na wengine watakaokuwa tayari nitaleta na zana halisi
 
Iwe vyovyote iwavyo bado elimu ni tatizo kwa jamii zetu

Pamoja na mzuri yake bado imeleta matatizo mengi sana

Unaweza kushangaa mtu ambae ni "msomi" anakwenda huko na huko sehemu mbali mbali duniani kusoma halafu akirudi kwao hataki hata kumsalimia mama yake kisa eti atamchafua

Hataki tena kuzungumza na watu wa kwao kisa hawajasoma

Hataki tena kuishi Tanzania kisa kuna wasio soma wengi

Matatizo ya kijinga ni mengi sana na unaweza kukaa mahali ukajiuliza kama hii inayoitwa elimu ni elimu au ni kitu kingine kabisa
Kuhusu uwepo wa imani za uchawi Ulaya na Marekani, naomba Nyani Ngabu na Kiranga au EMT watusaidie.
Unaweza kuishi Mwanza lakini bado ukawa hujui kama kuna watu wanaishi kwa mlo mmoja na ukaja kuambia ukadhani ni hadithi tu!
 
Mtu anakurupuka na kudai uchawi haupo kwa sababu sayansi imeshindwa kuthibitisha wakati anajua kabisa sayansi hiyo hiyo inakiri kuna isiyoweza kuyajua

Watu wengine wa ajabu sana!

Ulichoandika hapa ni a logical non-sequitur. You are concluding Z from A while A and Z have no logical connection.

Ni kama vile umeambiwa "Gari hili lililo Dar kuna barabara nyingine haliwezi kupita, kutokana na uimara wake". Halafu ukalikuta gari lile Kibaha na kusema "haiwezekani hili gari liwe Kibaha kwa sababu tushaambiwa lilivyokuwa Dar kuna barabara nyingine haliwezi kupita". Bila hata kuuliza barabara hizo lisiloweza kupita ni zipi na kutoka Dar mpaka Kibaha kuna barabara gani!

Kwamba sayansi kuna mengine imeshindwa kuthibitisha haina maana kwamba isitumike katika kupima uwezekano wa kimantiki wa uchawi kuwapo.

Sayansi pia imeshindwa kuthibitisha kwamba kuna kiumbe mwenye macho matatu anayekaa juu ya mlima Kilimanjaro na ku control ulimwengu wote.

Je, hilo linamaanisha kwamba kiumbe huyo yupo? Kwa sababu tu sayansi imekiri kuwa kuna mengine haijayajua?
 

Unavaa kiatu kimoja na kuacha kuvaa kingine makusudi

Tatizo langu mimi sio watu kuitumia sayansi kupimia mambo ikiwemo na uchawi

Tatizo langu ni kuhitimisha kuwa kitu fulani hakipo kwasababu tu sayansi imeshindwa kukithibitisha

Najua kuwa gari linaweza kupitia barabara nyingine kufika linakokwenda kwani barabara ambayo lilitarajiwa kupitia imeshindwa kuhimili uzito wa gari

Kwa upande mwingine tunaweza kusema gari ni uchawi kwa mfano na barabara ni kile ambacho kinaweza kuthibitisha uwepo wa uchawi,barabara ya kwanza ambayo tulitegemea gari kupita [sayansi] gari [uchawi] limeshindwa kupita,lakini hiyo haimaanishi gari hilo haliwezi kupitia njia nyingine kufika huko linakotaka kwenda

Kwa maana hiyo basi tunaweza kuthibitisha uwepo wa uchawi bila kutumia sayansi kwakuwa uchawi upo na tunaona matokeo ya uwepo wake!
 

Unathibitisha uchawi upo au haupo kwa kutumia nini?
 
Kila kitu kina side mbili. Uchawi ni side ya pili
 
Ukitaka kujuA Kama uchawi upo lazima ujue defn yake kwanza
Ukiangalia vizuri hata Simu Mabomu na computer ni uchawi
 
Kila kitu kina side mbili. Uchawi ni side ya pili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…