Je! Unadaiwa au unafikiria kukopa? Njoo tushauriane

DATAZ

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2012
Posts
3,799
Reaction score
10,196
Kwa hali ya maisha ya watanzania walio wengi ni VIGUMU sana kuishi bila kukopa. Vinavyokopwa ni vingi kianzia fedha, vyakula, nguo na bidhaa nyingine.

Ziko sababu kadhaa ambazo HUMLAZIMU mtu kukopa zikiwa ni pamoja na ufinyu wa kipato ukilinganisha na mahitaji ya kimaisha, dharura kama ugonjwa na masomo, sababu za kimaendeleo na nyinginezo.

Waswahili husema, "KUKOPA NI HARUSI NA KULIPA NI MATANGA". Msemo huu una mantiki kubwa na ndio maana mara nyingi tunashuhudia migogoro mingi katika jamii inayotokana na MADENI (kukopeshana).

Lengo la bandiko hili ni kushauriana kuhusu kufanya maamuzi sahihi ya kukopa na namna kukabiliana na maisha kipindi cha subsistence ya mkopo.

1. USIKOPE KABISA.

Ikiwezekana acha kabisa kukopa. Jibane kama vise kwa kidogo unachopata, utazoea tu.

2. UWE NA SABABU NZITO YA KUKOPA.

Ukikopa kwa sababu nzito ni rahisi sana kukumbuka kulipa na kupambana kutafuta ili ulipe kuliko kukopa kwa mfano ili ukatumbue bar.

3. ITATHMINI VIZURI BIASHARA UNAENDA KUKOPEA.

Usikope kwa ajili ya biashara ambayo hujaielewa vizuri kwa kufuata mkumbo.

4. KAMA UNA FAMILIA, ISHIRIKISHE.

Ieleze familia yako juu ya mpango wako wa kukopa ili kuondoa matatizo yasiyo ya lazima.

5. USIMKWEPE ANAYEKUDAI.

Inapotokea kuna jambo limeshindikana katika kulipa mkopo wako, usianze kumkimbia anayekudai na kuzima simu. Matendo hayo yatamghadhabisha sana mdai wako na anaweza kuchukua hatuaikiwezekana ambayo itakuumiza.

6. USIKOPE KWA WATU WAKOROFI.

Kuna mtu akikopa tu ujiandae kutangazwa na kudhalilishwa hata bila ulazima. Waogope sana watu hao.

7. DAWA YA DENI NI KULIPA.

Hakuna dawa nyingine. Hata kama matarajio yamekwnda ndivyo sivyo, kaa na mdai wako msihi akupe muda zaidi na ikibidi akupe utaratibu mwingine malipo kidokidogo.

LAMSNGI:
Usikope bila sababu ya MSINGI au ACHA KABISA KUKOPA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…