Je, unafahamu maajabu yaliyokuwa yakitokea katika daraja la Mto Kirumi?

Je, unafahamu maajabu yaliyokuwa yakitokea katika daraja la Mto Kirumi?

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
20,561
Reaction score
24,428
Kama ulikua hujui kuwa Duniani kuna Daraja ambalo wakandarasi liliwatoa jasho na wengine kukimbia wacha nikufamishe.

Daraja hilo lipo barani Afrika upande wa Afrika Mashariki nchini TANZANIA, Ndio, lipo TANZANIA mkoa wa MARA wilaya ya BUTIAMA kata ya BUKABWA Kijiji kiitwacho KIRUMI.

Daraja hilo linaitwa DARAJA LA KIRUMI, Lipo katika Kijiji kiitwacho KIRUMI katika mto MARA. Hili daraja brother katika ujenzi wake palitokea mambo mengi ya ajabu ajabu.

Mambo ambayo yaliwafanya wakandarasi kukiona cha mtema kuni, Daraja hilo la KIRUMI lina urefu wa mita 223.3.

Lilianza kujengwa Mwaka 1978 na Kampuni ya kichina ya H Ang. Mto huo ni mpana na una kina kirefu sana, Sasa kampuni hiyo ilikuja na wazo la kuangusha mlima Kwani pembezoni mwa huo mto kuna mlima unaitwa mlima KIRUMI.

Lengo lao udongo na mawe ya mlima huo wayatumbukize kwenye mto, Ili kupunguza upana na kina cha Mto MARA lakini walishindwa.

Ilipofika mwaka 1979, zabuni ilichukuliwa na Wakaburu. Kampuni ya Morem kutoka AFRIKA KUSINI pia nao walishindwa. Hawakuweza kuendelea kutokana kila siku walikuta vifaa vyao vinaelea kwenye maji alievipeleka hawamjui.

Wakienda kuvichukua usiku wakilala vinarudi tena kwenye maji. Wakiamka asubuhi wanavikuta kwenye maji wakaamua kusepa.

Mwaka 1980 Zabuni ikawaangukia Wahindi Kampuni ya Mauradadi. Hawa walianza ujenzi kwa kuchimbia nguzo karibu na kwenye maji.

Walikiona cha moto maana kulitokea tetemeko kubwa lililosikika hapo Mlima KIRUMI. Tetemeko ambalo lilipelekea kuvunjwa vunjwa nguzo zote.

Na kusukumwa mpaka Ziwa Victoria Wilaya ya Musoma. Kwasababu mto huo unamwaga maji yake katika Ziwa Victoria. Mwaka huo huo, wakaingia Kampuni ya lenari (COWIconsult) kutoka nchini Italia.

Hawa jamaa nao walikumbana na chamoto mbili kama ifuatavyo;-

Ya kwanza wakati wanajenga jiwe la msingi, Kila siku wakiamka walikuta wamemwagiwa shahawa kwenye makalio.

Walivumilia na kutunza siri mpaka wakafanikisha kujenga Jiwe la Msingi ili rais aje kuzindua ujenzi uanze. Rais Mwl. Julius Kambarage Nyerere ndiye aliyekuwa Mgeni Rasmi katika Uwekaji wa Jiwe la Msingi.

Hata hivyo siku moja kabla ya hafla uzinduzi wa jiwe la msingi ili ujenzi uanze changamoto ya pili ikajitokeza.

Tetemeko la ardhi likapita na kusababisha kupasuka na kuanguka kwa Msingi wote. Pamoja na Tukio hilo Rais akafika siku iliyopangwa kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi.

Lakini ilishindikana ilibidi waahirishe na Rais Nyerere hakuweza kushuka hata Kwenye gari. Waitaliano baada ya kuona mambo yanazidi kuwa magumu.

Waliona ni bora wayaweke wazi mambo wanayofanyiwa usiku. Halafu wakaomba likizo wakakubaliwa wakaenda kwao. Baada ya mwezi Mmoja walirudi ujenzi uliendelea bila shida hadi kukamilisha.

Mwezi Novemba, Mwaka 1985 Daraja la KIRUMI lilifunguliwa na Rais wa Awamu ya Kwanza Mwl. Julius K. Nyerere. Mpaka sasa daraja hilo lipo na linatumika hadi leo.

Hakuna tena cha matetemeko wala Maajabu mengine.
 
Aisee ule mdaraja maji unayaona yanapita karibu kbsa na daraja mto u atisha balaa na Ile milima ukipita kipindi Cha masika acha kbsa
 
Utaalamu wa kisayansi na kimazingara walioutumia wataliano pale kirumi sio wa nchi hii! Lile daraja huwa linanesa ukipita na gari kwa kasi ukiwa mdadisi ila ndipo balance yake ilipo miaka nenda miaka rudi na bado liko nga! Nga! Ngah!!!!
 
Utaalamu wa kisayansi na kimazingara walioutumia wataliano pale kirumi sio wa nchi hii! Lile daraja huwa linanesa ukipita na gari kwa kasi ukiwa mdadisi ila ndipo balance yake ilipo miaka nenda miaka rudi na bado liko nga! Nga! Ngah!!!!
Duuuh, hicho ni kivutio, lazima nitie timu huko!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilipita hapo mwaka 1989 nikitokea Mwanza kuelekea Tanga, wakati huo njia rahisi ni kupitia Nairobi.

Nilikuta kuna askali wakilinda pale na ukweli hilo daraja ni la kipekee maana ile kona yake kwenda upande wa pili unavutia na pale katikati lina nesa flani hivi.

Kuna siku nitarudi tena eneo hilo nifanye utalii wa ndani na mapicha juu kwa juu!.
 
Wataliano ilibidi Warudi kwanza kwao kwa muda🤔 waliporudi kila kitu kilikua sawa 👏😃 walienda kujifua upya
 
Kumbe wataliano nao wako vzuri eeh, had wahind na uchawi wao walisanda asee [emoji1][emoji1][emoji1]
 
Ndoo apo tunapojua kwamba kuna kuzidia
Kumbe wataliano nao wako vzuri eeh, had wahind na uchawi wao walisanda asee [emoji1][emoji1][emoji1]
Wazee walikua hawataki pajengwe au!?
 
Back
Top Bottom