Uchaguzi 2020 Je, unafahamu majukumu ya Tume ya Uchaguzi ni yapi kwa mujibu wa Katiba?

Uchaguzi 2020 Je, unafahamu majukumu ya Tume ya Uchaguzi ni yapi kwa mujibu wa Katiba?

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Kwa mujibu wa Ibara ya 74 (6) ya Katiba, majukumu ya Tume ni:-

(i) Kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura
katika uchaguzi wa Rais na Wabunge katika Jamhuri ya
Muungano;

(ii) Kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi wa Rais na Wabunge;
(iii) Kuchunguza mipaka na kuigawa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya uchaguzi wa Wabunge;

(iv) Kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura na uendeshaji wa uchaguzi wa Madiwani; na
(v) Kutekeleza majukumu mengine yoyote kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.

Majukumu mengine ya Tume kwa mujibu wa sheria ni pamoja na yaliyotajwa katika kifungu cha 4C cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi,

Sura ya 343, na kifungu cha 86A cha Sheria ya Uchaguzi ya
Serikali za Mitaa, Sura ya 292, ambayo ni:-

(i) Kutoa elimu ya mpiga kura kwa nchi nzima, kuratibu na
kusimamia watu wanaotoa elimu hiyo; na
(ii) Kuteua na kuwatangaza Madiwani wanawake wa viti
maalum.
 
Hahaha kumbe viti maalum huwa ni vya wanawake, Kabudi alichukua kiti cha nani?!
 
Back
Top Bottom