Je, unafahamu namna ya kugundua kama gari imeshushwa kilometer katika dash board?

Je, unafahamu namna ya kugundua kama gari imeshushwa kilometer katika dash board?

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,409
Reaction score
13,262
Kuna michezo mingi watu huifanya hasa wanapotaka kuuza gari ,hapa wengi hufanya mchezo wa kushusha km ilinwaweze kuliuza garinkwa haraka, na kwa pesa ndefu. Wengi hufanikiwa kasheshe inakuja kwa aliyelinunua unakuta linamzingua vibaya kutokana na kuchengana kwa data za service.

Technolojia ina mengi na inaumiza wengi wasio kuwa na uelewa nayo. Kumbe kuna wimbi kubwa sana la watu wana agiza magari kutoka nje na hata kununua kwenye show room za hapa Bongo kwa kigezo cha kuangalia kilomita zilizotembewa na kufanya ndio kipimo cha ubora na ubora wa gari, wanajikuta wanangukia pua.

Hapo wengi wanaingia sana mkenge kwa kuwa kilomita za gari zinashushwa ili kukuvutia mnunuaji kwa nchi za wenzetu ni kosa kisheria. Hasa ujerumani nimekaa sana Na ninapafahamu vyema yaani ukigundulika umefanya hivyo ni sawa na muuaji ila sijajua kwa Bongo imekaaje

Lengo la mada hii la kuiweka hapa ni kuwa hapa ni sehemu sahihi sababu kuna wataalam wa IT. Swali l kubwa watu hujiuliza, je haiwezekani kutambua kuwa gari hii iliwahi kushushwa kilomita? Nimeshawishika kufikiria hivi baada ya kukumbuka kuwa kwenye hard disc au memory card vitu vikifutwa unaweza kufanya back up na ukavipata tena.

Sasa kwa kuwa kwenye dash board za magari/cluster kilomita zilizotembewa na gari huwa zinahifadhiwa kwenye EEPROM,
Ipo namna ya kutambua kwamba data zilizomo kwenye eeprom zilisha wahi editiwa? Japo mchakato wale ni mrefu kidogo na unahitaji mtu makini mwenye vifaa iwe kwa kutambua mwanzo ilikuwa na km ngapi au hata kwa kutambua tu kuwa eeprom hii ishawahi fanyiwa ujanja?

Japo kushusha ni rahisi sana kama ukiwa na mshine ya OBD ZILE KUBWA au ukiwa na laptop yenye softwear za magari kwa ajili ya EEPROM japo watengenezaji wa magari kama Toyota, Nissan, Honda hiki ni kitu wana ki-burn sana japo bongo watu wanafanya.

JE, WEWE UNADHANI NJIA GANI INAWEZA KUTUMIKA KWA HARAKA KUTAMBUA KUWA KM ZIMESHWA TUSHIRIKISHE KARIBU KWA MJADALA

No photo description available.

Source😀ominique Maguhwa - TANZANIA USED CARS MARKET(THE TOP GEAR)
 
Kwa mtu kama mimi kwa uzoefu wangu wa kijijini,huwa naangalia oil silly,pedel ,usukani ,sit na hub maana vyote hivyo vina uwiano na kilometer,wakipunguza tu kwa hapo lazima ntajua tu,labda wabadilishe vyote ambayo itakuwa hasara kwao,kibongo bongo sana sana wataliosha tu vizuri tu
 
Wewe omba Mungu tu na lifanyie inspection gari kuanzia kwenye body hadi engine ujiridhishe. Mengine utajitia presha bure.

Unaweza kuekewa gauge cluster yenye low milage tu na ukapigwa.
 
Kuna gari zinakaa Zanzibar miaka Kisha wanazileta bara (wanang'oa namba za Zanzibar) linaoshwa fresh unapigwa mchana peupe kumbe jamaa washakaa nalo Sana unguja hapo
Niheri litumike hapo n'gambo na liwe zima lisisumbue, kuliko kulitoa huko japan n.k halaf lije likusumbue hapa utajuta
 
Njia za kujua ni hizi

1. Muuzaji akupe file la gari wakati linaingia Tanzania maana kwenye file kuna kua ma documents za TBS walivyokagua gari likiwa bandarini

2. TRA kwenye mfumo wao wa TANCIS wanaweza kujua baada ya kupeleka namba ya gari husika kwao.

3. Kufungua ile cluster yenyewe utaona kwa nyuma kuna sehemu imekua soldered( hii niliwahi kuona kwenye IST) baada ya hio IST dashboard kuganda kwenye kilomita bila kupanda
 
Njia rahis ni hii" Hivi sasa hivi kwa mfano mtu anataka kukuuzia zile Benz za mjerumani za zamani halafu unakuta hiyo Benz,eti namba D!!
 
Ikiwa una chukua Showroom check kushoto kwako juu ya kioo cha mbele uwa kuna sticker imebandikwa ikionyesha INSPECTION KILOMETRE uwa zina andikwa kwa peni ukikosa pale check kwenye file kuna paper imeandikwa ivyo ukikosa napo jua iyo ime chachukuliwa
 
Kwa Uzoefu wangu kila Gari Inayotoka Japan lazima pale upande wa Kushoto kwenye Kioo cha mbele juu iwe ina Sticker mbili. Moja ni ya Duara ina rangi ya njano huwa inaandikwa "Inspected Mileages" huwa inaandikwa Mileages za gari zilizopo kwenye Odometer kabla haijasafirishwa kuja Tz. Na Chini Yake huwa kuna Sticker Nyingine imeandikwa "Radiation Free". Sign Ya Kwanza ya kujua Gari Imebadilishwa Mileages ni Ukiona Hako Ka Sticker ka juu kamebanduliwa na Mara nyingi huwa wanakabakiza Kale ka Sticker ka Chini ka "Radiation Free".

NB sio Kila gari Iliyobanduliwa hako ka Sticker Imechezewa Odometer, kuna Baadhi ya wamiliki huwa hawapendi Sticker Nyingi kwenye Kioo cha Mbele.

Angalizo Gari Nyingi Za Show Room huwa wanapunguza Kilometers kama huamini angalia kama zinakuwaga na Hicho ki Sticker!! Na aina ya Gari ninnazozijua zinaongoza Kupunguzwa Kms kwa Uchache ni Toyota Crown na Toyota Alphard japo Zipo aina nyingine Nyingi Tuu zinazoshushwa kms.
Kwa Hiyo wanunuzi Wa Crown na Alphard Kuweni Makini.

Nipo Tayari Kukosolewa kama kuna Sehemu Nimeenda Chaka.
 
Back
Top Bottom