Gudboy
JF-Expert Member
- Aug 14, 2009
- 867
- 82
Inapokuja katika swala la utayarishaji msosi majumbani kwetu hatuwezi kutoikubali kazi ya friji katika mpango mzima wa kuhifadhi chakula. Kwa kuhifadhi vyakula katika jokofu kunaokoa mda pale unapotaka kupika msosi wa haraka.
Swali la kujiuliza ni vyakula hivi tunavyoviweka katika majokofu yetu vinaweza kuwa salama kwa mahitaji ya mwanadamu ndani ya mda gani? wataalamu wanasema chakula chochote kitakacho hifadhiwa ndani ya nyuzi 0 za Fahrenheit kitakuwa salama kwa kuliwa kwa mda wote lakini ubora wa chakula hautakuwa uleule.
Tumekuorodeshea baadhi ya vyakula na mda wake unaoruhusu kuhifadhiwa kwenye jokofu.
Mkate: Miezi 2 mpaka 3
Nyama iliyopikwa: Miezi 2 mpaka 3
Matunda: Miezi 8 mpaka 12
Sausage: Mwezi 1 mpaka 2
Soupu: Miezi 2 mpaka 3
Vipande vya nyama ya kuku ambayo haija pikwa: Miezi 9
Kuku mzima ambae hajapikwa: Mwaka 1
Mboga za majan : Miezi 8 mpaka 12
Ni muhimu ukazingatia haya:
Kama chakula ni chamoto subiri kipoe kwanza ndio ukiweke kwenye jokofu,hiyo inasaidia kukifanya kipate ubaridi mapema ambapo ubora wake hautapotea kwa haraka. Usigandishe vyakula ambavyo vipo katika makopo au mayai hiyo itavifanya kupata nyufa na bacteria kuingia. Ni muhimu ukafuata maelezo kwa vyakula vilivyotengenezwa viwandani.