Je, Unahitaji Mbegu bora (Hybrid seeds) kwa ajili ya Greenhouse au bustani yako?

Je, Unahitaji Mbegu bora (Hybrid seeds) kwa ajili ya Greenhouse au bustani yako?

George Upina

Member
Joined
Feb 26, 2011
Posts
10
Reaction score
27
RIJK ZWAAN ni kampuni iliyobobea kwenye utengenezaji wa mbegu bora za mboga mboga. Kwa tanzania tuna matawi mawili Arusha (Q SEM na AFRISEM). Pia tuna tawi jipya Mwanza na sasa Bagamoyo. Kutoka kwetu utapata mbegu za Nyanya (Round to Oval and Cherry) utakazoweza kuvuna kwa muda wa miezi mpaka 7 ndani ya greenhouse na miezi minne nje (ukiwa na system nzuri ya umwagiliaji kama Drip irrigation). Tuna hoho za rangi (Green, Yellow, Orange na Red) tuna paplikas,Matangomafupi na marefu, tuna Matikiti, Sweet melon, Beet roots, Ngogwe (Nyanya chungu), Bilinganya, Lettuce, Cauliflower, na nyingine nyingi isipokuwa kitunguu.

Siyo kama makampuni mengine, RIJK ZWAAN baada ya kukuuzia mbegu inakupa ushauri popote pale ulipo bureeee.
Greenhouse ni technologia mpya hivyo anayeumia ni mkulima maana kila makampuni yanataka kumfaidi hivyo mkulima asipokuwa makini anajikuta ameijiingiza kwenye kampuni isiyo sahihi. Tunajivunia kwamba wakulima wakubwa tanzania kama Ngongoseke Farms (Magu Mwanza), Lusana Farms (Geita) nawakulima wengine wa Arusha, Moshi, Lushoto, Bagamoyo hadi Zanzibar wanatumia Mbegu kutoka RIJK ZWAAN.

Utakutana na wtaalamu waliobobea kwenye kilimo cha mboga mboga na watakuhudumia popote pale ulipo.
Like page yetu pia ya Rijk zwaan Tanzania kwenye Facebook na pia unaweza pitia web site yetu Homepage - Rijk Zwaan.

Kwa Mawasiliano mengine piga 0762 682 824 au 0713 888 913 email g.upina@rijkzwaan.com
 

Attachments

  • 10647075_668814613264595_8937321443624717412_n.jpg
    10647075_668814613264595_8937321443624717412_n.jpg
    25.4 KB · Views: 388
  • 1897026_668818249930898_3562141440120574374_n(1).jpg
    1897026_668818249930898_3562141440120574374_n(1).jpg
    22.2 KB · Views: 421
  • 10690078_665263930286330_7555636523153893351_n.jpg
    10690078_665263930286330_7555636523153893351_n.jpg
    14.3 KB · Views: 322
  • 11024603_665263926952997_9222679027510762858_n.jpg
    11024603_665263926952997_9222679027510762858_n.jpg
    12.3 KB · Views: 309
Heikki Niskala Hajambo? Micho je? Alphonce yupo? Salimia sana......
 
  • Thanks
Reactions: ral
Safi sana hii kitu ila samahani mkuu naomba nisaidie nahitaji kujua duka au maeneo gani ntapata dawa ya kuua maguu inaitwa ROUNDUP na pia nasikia kuna dawa nayo naweza kuitumia wakati wa majani ya palizi nikapulizia hiyo majani yanakufa.Nahitaji kujua kwa bei ya jumla maana nataka nyingi kariakoo naona bei ziko juu sana na mm nataka kwa wingi
 
Asante Kiogwe
Round Up ipo katika majina na bei tofauti kulingana na kampuni. Mfano Monsanto inaitwa hivo hivo Round Up, Twiga Chemical wanaita Gugusate, TCC wanaitwa Glyceri na Zaidi. Makampuni ninayoyajua yanauza bei ya jumla kuanzia (8500 mpaka 9500) kwa lita.

Round Up inaua majani yoooote shambani yaani haichagui (Non selective) ni vema ipigwe kabla ya kupanda na usubiri kwa muda wa kama week tatu.

Kuna dawa ambazo tunatumia kuua kwekwe baada ya kupanda na hizo hutofautiana kufuatana na aina ya mazao na majani unayokusudia kuua.
Mfano Kuna dawa za kuua magugu yenye majani mapana hivyo mazao yako yakiwa pia na majani mapana kama maharage nayo yanakauka. Hivyo hii dawa itumike kwenye mazao kama Mpunga.

Pia kuna dawa za kuua magugu yenye majani membamba (nyasi) hivo hii dawa kama mazao yako yana majani membamba na ukapiga hii dawa utajikuta na mazao yamekauka.
Natumaini nimekujibu.

Safi sana hii kitu ila samahani mkuu naomba nisaidie nahitaji kujua duka au maeneo gani ntapata dawa ya kuua maguu inaitwa ROUNDUP na pia nasikia kuna dawa nayo naweza kuitumia wakati wa majani ya palizi nikapulizia hiyo majani yanakufa.Nahitaji kujua kwa bei ya jumla maana nataka nyingi kariakoo naona bei ziko juu sana na mm nataka kwa wingi
 
Naomba kujua bei ya mbegu ya nyanya izi highbrid zikoje?
 
Kibila
Bei inarange kuanzia TZS 127 mpaka 250 kwa mbegu moja na inakupatia kuanzia kilo 15 na kuendelea kwa mche mmoja kwa msimu.
 
bwana geogrge hivi letttuce naweza kulima mikoa kama ya lindi au mtwara?
 
Kwa Mwanza ofisi / duka lenu liko sehemu gani? Pia nambie ni dawa gani ninyunyizie nyanya zikishaweka matunda lakini hayajakommaa ??
 
Habari ndugu. Ninaishi mitaa ya kia. Ninamchakato wa kupata kibali cha kutumia maji ya kisima fulani kilichimba muda na hakitumiki kwa sasa na kuna eneo lisilopungua ekari 7. Napenda kulima mbogamboga lakini sina utaalam wala mtaji wa uhakika. Naweza kupata udhamini au mkopo hapo kwenu kwa marejesho ya baadae? Nashukuru sana.
 
Back
Top Bottom