Je, unajua kutotoa au kutodai risiti ni kosa kisheria?

Je, unajua kutotoa au kutodai risiti ni kosa kisheria?

Gini

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2018
Posts
398
Reaction score
385
KUTOTOA & KUTODAI RISITI NI KOSA KISHERIA

Na Mwl. Sylvester,

Je, unajua kutotoa au kutodai risiti ni kosa kisheria?
Kutodai risiti au kushindwa kuripoti kuwa umenyimwa risiti, au ankara ya malipo wakati wa kununua bidhaa na huduma ni kosa kisheria. Hili linawekwa bayana na Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya 2015 (THE TAX ADMINISTRATION ACT, 2015)
Kifungu cha 50, 51, 55 (1) & (2) kwa pamoja vinaeleza makosa na adhabu itakayotolewa endapo utashindwa kudai risiti. Na endapo umenunua bidhaa na kuomba risiti ukanyimwa, sheria inakutaka kuripoti haraka sana kwa Kamishna Mkuu wa TRA ili kuweza kuchukua hatua zaidi.

Wapo wafanyabiashara walioruhusiwa kisheria kuwa na matumizi ya Mashine (EFD) ambao hutakiwa kutoa risiti ya kielektonic na wale wafanyabiashara walio na mitaji isiyovuka Tshs Milioni 4 ambao hupewa vitambulisho maalumu ambavyo huvilipia Tshs 20,000/=. Adhabu ya kutotoa risiti kwa kutumia mashine inaweza ikawa Tshs milioni 3-4.5 au kifungo au vyote kwa pamoja na mteja ambaye hatadai risiti inaweza kuwa kuanzia Tshs 30,000 - 3,000,000 au kifungo kisichozidi miezi mitatu au vyote kwa pamoja.

Mtu ambaye atashindwa kudai risiti ya kieletroniki au kushindwa kutoa taarifa ya kutoa risiti ya kieletroniki au Ankara ya kieletroniki punde atakuwa amefanya malipo ya bidhaa au huduma atakuwa amefanya kosa na ikithibitika atalipa faini isiyopungua pointi za sarafu 2 au isiyopungua pointi za sarafu 100. (kutoka katika mtandao wa TRA).

Watanzania tumezoea kutokuona umuhimu wa kuchangia pato la Taifa kupitia kulipa kodi hasa kodi ya ongezeko la thamani (VAT), kwa Wafanyabiashara na wateja. NI muhimu sasa kila mtanzania hasa wateja wa bidhaa kuzingatia umuhimu wa kudai risiti ili kodi yako unayolipa ikusanywe kihalali na kutowaachia wafanyabiashara ambao machache wao sio waaminifu na kuisababishia Serikali hasara.

Unaponunua bidhaa KWA mfano ya thamani ya Tshs 30,000/= Serikali inatakiwa kukusanya kodi ya 18% ya pesa hiyo ambayo ni Tshs 5,400/=. SASA, unaposhindwa kudai risiti ya kielectonic maana yake ni kwamba Tshs 5,400/= itabaki kwa mfanyabiashara na Serikali haitapata chochote. Kuna mtindo wanautumia wafanyabiasha waku bargain na wateja, mfano unanunua Laptop ya thamani ya laki saba (700,000), badala ya kutoa pesa hiyo atakwambia anakuuzia kwa 660,000/= bila risiti ya kielekroniki au ulipe laki 7 akupe risiti ya kielekroniki. Ukikubali kutoa 660,000/= maana yake umeiingizia Serikali hasara ya Tshs 126,000/= ambayo ni 18% yaani kodi ya VAT ya thamani ya laki 7 ambayo ungelipa.

Tunapoilalamikia serikali kutowajibika kwenye kufanikisha huduma kwa Wananchi ni lazima tuanze kujilaumu sisi wenyewe, jiulize unatimiza wajibu wako ipasavyo, unalipa kodi ipasavyo, ulipofanya manunuzi ya bidhaa ulidai risiti itokanayo na mashine au ulipewa risiti ya kuandika kwa mkono? Mashine zinazotoa risiti (EFD) zina mfumo maalumu uliounganishwa na TRA wenye taarifa ya mfanyabiashara. Mfanyabiashara anapotoa risiti kwa njia ya mashine taarifa hiyo itasomeka TRA na wakati wa makusanyo ya kodi itaiwia wepesi TRA kuchukua kodi halisi kwa mfanyabiashara huyo kutokana na biashara halisi aliyofanya.

Akikupa risiti ya kuandika kwa mkono tafsiri yake ni kwamba mashine haitapeleka taarifa ya mauzo yake kwa Mamlaka ya Mapato (TRA) na kwa mantiki hiyo mfanyabiashara atakuwa amekwepa kulipa kodi na wewe mnunuzi utakuwa umeibiwa kwa kuwa kodi inayotakiwa kwenye TRA atabaki nayo mfanyabiashara. Kwa kutambua hilo, sisi kama Wananchi tunatakiwa tupeane elimu hii ya kulipa kodi kwa kudai risiti itokanayo na mashine na uidai maana ni wajibu wake akupe na ni haki yako. Kwa pamoja tutakuwa tumeisaidia Tanzania kujenga uchumi wa Taifa letu na huduma zitaboreka zaidi.
ENDAPO mfanyabiashara hajakupa risiti ya kielektroniki unaweza muda huo huo kuwasiliana na TRA kwa msaada zaidi na isipite siku baada ya tukio hilo. Unaweza kuwasiliana na TRA kwa namba 0800 750 075 au 0800 780 078 kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 1 usiku, kila siku Jumatatu - Ijumaa, isipokuwa siku za sikukuu.

Ni wajibu wetu kama watanzania kuhakikisha Serikali inakusanya kodi kwa lengo la kukuhudumia. Unapolipa kodi unakuwa umeiwezesha Serikali kutekeleza miradi yake ambayo ndiyo mahitaji ya mwananchi katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kiujuma. Huduma zote za kijamii zinafanikiwa kupitia kodi, iwr VAT, INCOME TAX n.k. Yafuatayo ni baadhi ya maeneo yaliyotekelezwa kupitia uwajibikaji wa mlipa kodi,

å Ujenzi wa SGR ambao kwa sasa umefikia 70% kwa sehemu ya Dar es Salaam
– Morogoro (km 300) na 20% sehemu ya Morogoro – Makutupora (km 422);
å Ujenzi wa Mradi wa kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere;
å Ujenzi wa barabara na madaraja ikiwemo Ubungo Interchange ambayo ujenzi
wake umefikia 55%; daraja la Selander (12%); barabara ya njia nane kutoka
Kimara hadi Kibaha (asilimia 41%); na ujenzi wa barabara za lami katika
maeneo mbalimbali nchini unaoendelea;
å Ugharamiaji wa miradi ya kimkakati 22 ya kuongeza mapato na kupunguza
utegemezi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa;
å Miradi ya Maji ya Kitaifa;
å Kupeleka umeme vijijini kupitia REA;
å Kuboresha Shirika la Ndege Tanzania.
å Mishahara ya watumishi;
å Utekelezaji wa miradi ya miundombinu (barabara, reli, nishati);
å Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu na elimumsingi bila ada;
å Miradi ya maji mijini na vijijini; na
å Huduma za afya (dawa, miundombinu, vitendanishi, vifaa na vifaa tiba)
MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom