JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Mtu anaweza kwenda Mahakamani na Kumshitaki mtu mwingine ambaye anamsababishia usumbufu katika Eneo lake la Makazi au la Kazi.
Usumbufu huo unaweza kuwa Kelele, Harufu, takataka, au aina nyingine yoyote ya usumbufu itakayomfanya mtu asiweze kufurahia eneo lake.
Ili mtu aweze kufanikiwa Katika Kumshitaki mtu mwingine kwa Usumbufu lazima aweze kuthibitisha vitu viwili:-
1. Uwepo wa usumbufu uliokuwa kinyume na sheria au usiokuwa na sababu za msingi.
2. Kupata Hasara kutokana na Usumbufu uliofanywa.
Upvote
2