Nitajaribu kukupa baadhi ya majibu ya maswali yako, naamini watu wengine wenye uelewa kunizidi watakuja kuuongezea ujuzi wao juu ya haya:
Kumbuka nikisema mkongo au nikisema fibre namaanisha kitu kimoja. Maana kiurahisi Mkongo wa taifa ni Fibre optic cable: nyaya inayowezesha kutuma na kupokea data kwa uharaka mkubwa sana.
1. Swala la intaneti kuwa shida, hata kwenye jiji kubwa kama Dar-es-Salaam. Naamini swala hili linaweza kutokana na a) Idadi ya watumiaji wa mtandao kuwa kubwa sana katika eneo husika kuliko uwezo wa minara iliyopo ndani ya eneo hilo; b) Mtoa huduma kutofanya maboresho/marekebisho ya minara yake kuweza kuhudumia idadi hiyo kubwa ipasavyo; c) Watumiaji wa mtandao kuwa na simu zisizo sapoti "bands" ambazo mtoa huduma anazitumia na kusababisha wasipate spidi halisi za mtandao wake.
2. Issue ya kuunganishwa majumbani. Naona kwa sasa baadhi ya maeneo (DAR) mtandao kama TTCL wameshaanza kuweka sawa miundombinu ya fibre to home (utaona kuna waya waya fulani nyeusi kama zile za huduma ya cable zinapitishwa kila kona ya jiji) ili watu waweze kuvutiwa majumbani. Lakini tatizo lililokuwepo miaka yote ni swala la FAIDA, hususani, haya makampuni hayakutaka kuvuta miundombinu ya fibre kuja kwenye mitaa isiyokuwa ya kishua, kama vile: City Centre, Masaki, Oysterbay, Mikocheni n.k. Hawakutaka kuweka hela nyingi kutuleta huduma hii sisi walala hoi kutokana na idadi ndogo ya watu watakaojiunga na huduma hii.
Hali hii itabadilika kama sio mwisho wa mwaka huu, basi kabla ya katikati ya mwaka 2022 kwa maeneo mengi nchini.
3. Utajuaje kuwa sehemu unayoishi kuna Mkongo. Kama ulikuwepo katika eneo hilo tangia miaka ya 2015, basi ulishaona wakichimba chimba kupitisha waya wa rangi ya bluu. Kama umeamia; utaona bikoni zipo katika maeneo yaliyopishwa mkongo. Kama ninapoishi Vodacom na Halotel walipitisha hiyo waya mwaka 2016 kupeleka kwenye minara yao, na kuna bikoni zimeandikwa VODACOM juu yake.
4. Ukiwa na mkongo ni lazima ujenge minara? Ndiyo! Ilikuwezesha matumizi ya simu za mkononi (kupiga na kupokea jumbe, sauti na data nyingine) lazima minara iwepo, lakini pia ili minara ya simu iweze kutuma na kupokea taarifa baina yake kwa haraka inahitaji kutumia Mkongo. Japo inaweza kutumia mawasiliano kupita microwave, lakini mkongo ndio mzuri zaidi.