Na shetani nae anae da motoni...Kuna watu wanakiri kwamba wamepata utajiri baada ya kupewa "dawa" na waganga wa kienyeji au wachawi. Kulingana na Maandiko, inawezekana shetani akakupa mali lakini lazima ukubali kumsujudia. Katika Luka 4:5–7 imeandikwa:
"Akampandisha juu, akamwonesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa yeyote kama nipendavyo. Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako. Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake."
Hii inaonyesha kuwa Shetani ana uwezo fulani wa kutoa "fahari" na "enzi" ya kidunia — mali, mapesa, heshima — lakini kwa masharti kwamba lazima umsujudie na kumwabudu — kwa kushiriki mambo ya uchawi/ushirikina.
Shetani anajulikana kama baba wa uongo na muuaji.(Yohana 8:44). Akikupa mapesa au fahari ya dunia hii, ujue amekutega. Amekutega umwabudu mungu mwingine kinyume na agizo la Mungu. Mungu alisema: “Usiwe na miungu mingine ila mimi.” (Kutoka 20:3)
Ukiabudu miungu mingine maana yake unajitakia laana(Kum 28:15). Hivyo mali yoyote itakayokupeleka kwenye ibada nyingine ni laana hata kama inaonekana kama "baraka."
Hivyo ndugu yangu, kama unawaza kwenda kwa waganga ili upate utajiri, futilia mbali mawazo hayo. Shetani anakutega umsujudie halafu siku ya mwisho uangamie pamoja na yeye motoni.
cc: Nomadix
Sasa mbona bible inatuchanganya tena.....tusipende fedha na nsio chanzo cha mambo mabaya. Lakini wakati huo huo inasema pesa ni ulinzi.Hakuna pesa zinazopatikana kwa waganga, au njia za kishirikina, na kama zipo mwisho wake ni mbaya sana unatisha! Tamaa ndio imefanya watu kuamini kuna utajiri wa njia hio. Tamaa ya pesa ni mbaya sana, ndio chanzo cha mabaya.
1 Tim 6:10
Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na imani, na kujichoma kwa maumivu mengi
Tufanyeje basi:
1 Tim 6:11
Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, saburi, upole.
Kiukweli nimesikitika sana kuona shetani ana ukwasi kiasi hicho cha kutajirisha watu na kuwapa maisha bora, tofauti na mungu tunaye hubiriwa kila siku ambapo waamini huombwa pesa kwaajili ya kuchangia kufanikisha kazi za huyo mungu.Kuna watu wanakiri kwamba wamepata utajiri baada ya kupewa "dawa" na waganga wa kienyeji au wachawi. Kulingana na Maandiko, inawezekana shetani akakupa mali lakini lazima ukubali kumsujudia. Katika Luka 4:5–7 imeandikwa:
"Akampandisha juu, akamwonesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa yeyote kama nipendavyo. Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako. Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake."
Hii inaonyesha kuwa Shetani ana uwezo fulani wa kutoa "fahari" na "enzi" ya kidunia — mali, mapesa, heshima — lakini kwa masharti kwamba lazima umsujudie na kumwabudu — kwa kushiriki mambo ya uchawi/ushirikina.
Shetani anajulikana kama baba wa uongo na muuaji.(Yohana 8:44). Akikupa mapesa au fahari ya dunia hii, ujue amekutega. Amekutega umwabudu mungu mwingine kinyume na agizo la Mungu. Mungu alisema: “Usiwe na miungu mingine ila mimi.” (Kutoka 20:3)
Ukiabudu miungu mingine maana yake unajitakia laana(Kum 28:15). Hivyo mali yoyote itakayokupeleka kwenye ibada nyingine ni laana hata kama inaonekana kama "baraka."
Hivyo ndugu yangu, kama unawaza kwenda kwa waganga ili upate utajiri, futilia mbali mawazo hayo. Shetani anakutega umsujudie halafu siku ya mwisho uangamie pamoja na yeye motoni.
cc: Nomadix
Uliwahi kumuona shetani?Shetani akikupa mapesa ujue pia yataambatana na hofu, mateso, na huzuni.
Katika Mithali 10:22 tunaambiwa: "Baraka ya BWANA hutajirisha, wala haichanganyi na huzuni.”
Ikiwa baraka za Mungu hazina huzuni, basi ni wazi kuna "baraka" nyingine ambazo huja na huzuni — hizo ni zile zisizotoka kwa Mungu, yaani za kishetani. Hivyo ukipata “mapesa” kutoka kwa shetani ujue yatakuja na kifurushi cha huzuni, hofu, ndoto mbaya na mateso. Unaweza usione mateso kwa sasa, lakini usisahau siku ile ya mwisho utatupwa jehanam na kuteseka milele na milele, motoni.
Weee bwege nini unaniuliza mie wakati wee ndio unajua bible kuliko mie 🤣🤣🤣🤣Pesa ni ulinzi imeandikwa wapi, mkuu?