Je unajua ubatizo unaua na vile vile unaokoa?

Je unajua ubatizo unaua na vile vile unaokoa?

Bado natafuta

Senior Member
Joined
Oct 3, 2021
Posts
126
Reaction score
138
Je unajua ubatizo unaua na vile vile unaokoa?.

Ipo siri kubwa sana katika ubatizo ambayo laiti watu wengi wangeijua wangeutafuta kwa bidii zote.

Hebu tusome mistari ifuatayo,

1 Petro 3:20 “watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, WALIOKOKA KWA MAJI.

21 MFANO WA MAMBO HAYO NI UBATIZO, UNAOWAOKOA NINYI PIA SIKU HIZI; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo

Hapo kuna vitu 3 vya kuzingatia katika mistari hiyo..na tutatazama kipengele kimoja baada ya kingine.

1. WATU WANANE WALIOKOKA KWA MAJI.

Hapa tunachoweza kuonajumla nafsi 8, waliokoka kwa ni kwamba..“kumbe maji ni njia ya wokovu?”. Nuhu pamoja na mkewe na wanawe watatu na wake zao,

Wakati wengine wasioamini wanaangamia kwa maji, Nuhu aliyeamini, maji hayo hayo yanamwokoa na ghadhabu ya Mungu. Hili ni jambo la kwanza la kuzingatia…hebu tulitazame jambo la pili.

2. MFANO WA MAMBO HAYO NI UBATIZO, UNAOWAOKOA NINYI PIA SIKU HIZI.

Kumbe kama Nuhu alivyookoka kwa Maji zamani hizo, na sisi siku hizi hatuna budi kuokoka kwa kupitia maji hayo hayo? Yaani kwa Kubatizwa. Si ajabu Bwana Yesu alisema katika Marko 16:16 kuwa..“Aaminiye na kubatizwa ataokoka”..na si “atakayeamini tu peke yake”

Huu ni ufunuo mkubwa sana ambao Mtume Petro alifunuliwa na Roho Mtakatifu..

Kumbe wakati sisi tunasoma habari za gharika ya Nuhu kama gazeti, kumbe nyuma yake kuna ufunuo wa ubatizo..

Si ajabu na Yohana Mbatizaji pengine naye alitolea ufunuo wa ubatizo humu humu.
Unapomwamini Yesu (Ni sawa na umeingia ndani ya safina kama Nuhu)..unapobatizwa kwa kuzamishwa katika maji mengi na kuibuka juu (Ni sawa na umeingia kwenye gharika ukiwa ndani ya safina na umetoka salama).

Na kama vile baada ya gharika Mambo yote yakawa mapya kwa Nuhu, akaingia katika ulimwengu mpya na kuanza maisha mapya, yale ya kwanza yenye shida na dhuluma na maasi yamepita. (Kwa ufupi uchafu wote wa kwanza ukaondoka).

Vivyo hiyo na sisi tunapobatizwa katika roho tunaondoa uchafu wote unaozunguka maisha yetu ya kiroho… Yale maisha ya kale yanazikwa, zile dhambi za kale zinaisha nguvu, kile kiburi cha kale kinafifia n.k
Faida hii kuu inatupeleka katika kipengele cha tatu na cha mwisho

3. SIYO KUWEKEA MBALI UCHAFU WA MWILI, BALI JIBU LA DHAMIRI SAFI MBELE ZA MUNGU.

Kumbe lengo la ubatizo sio kuondoa uchafu wa mwilini kama JASHO au VUMBI..bali ni kuondoa uchafu wa rohoni ambao huo ndio jibu la Dhamiri zetu safi mbele za Mungu.

Swali ni Je! umebatizwa ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Bwana Yesu kulingana na Matendo 2:38?.

Kama bado unasubiri nini na tayari umeshajua faida zote hizi?..Haraka sana katafute ubatizo sahihi, kwa gharama zozote baada ya wewe kumwamini Bwana Yesu na kutubu dhambi zako.
 
naomba nipinge hoja yako ya pili unapodai mtu anaokolewa kwa imani na kubatizwa kwa hoja hizi mbili

1.hoja ya matumizi ya neno "kai"
kutokea katika Marko 16:16 tunaona neno linasema
16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.
sasa tujikite katika neno na lililotumika katika mstari huu.....neno hili katika biblia ya kiswahili na biblia ya kingereza limetumika kama kiunganishi ila katika lugha ya asili ambayo ni kigiriki neno kai limetumika sasa tukiangalia maana ya neno "kai" linaweza kutumika kama na kama ilivyotafsiriwa kiswahili na kingereza ila pia inatumika kuelezea vitu viwili vyenye maana moja ambapo ndipo hoja yangu ilipo kwa uchanga wa lugha ya kiswahili umesababisha matumizi ya k"ai" yaani "na" kama kiunganishi wakati ilitakiwa kuelezea kitu kimoja hivyo mstari huo unatafairiwa hivi
16 Aaminiye ambako ni kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.

2.kanuni ya kutafsiri biblia kwa kutumia maandiko mawili na kuendelea
ili kupata tafsiri sahihi ya mambo yaliyoandikwa kwenye biblia..biblia yenyewe imeelekeza kuwa kama neno limeandikwa zaidi ya mara moja basi neno hilo limethibitika na ni kweli lakini ukichukua kifungu ulichokitoa kwa tafsiri isiyo sahihi kuwa mtu anaokoka kwa kuamini na kubatizwa na siyo imani peke yake hakuna neno lingine "linaloback up" neno hilo hivyo tunaweza kusema kuwa tafsiri hiyo siyo sahihi lakini pia tukiangalia biblia hiyo hiyo ina sehemu nyingi(zaidi ya mbili) ambazo zimeonyesha kuwa watu wanaokolewa kwa imani peke yake

mistari kama

yohana 3:16
16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

efeso 2:8-9
8 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;
9 wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.

ebrania 11:6
6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.

warumi 3:28
Basi, twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria.
warumi 5:1
1 Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,

naweza kuorodhesha mistari 100inayoonyesha tunahesabiwa haki(tunaokolewa)kwa imani pekee na siyo imani na ubatizo

naomba kuwasilisha
 
Nashukuru ndugu kwa kuweka hoja yako hapa. Kwanza unatakiwa ufahamu ubatizo ni tendo linalofanyika baada ya kuamini. Na Imani bila matendo imekufa, hii maana yake kwamba ukiamini tuh halafu hakuna tendo linalothibitisha Ile Imani ni kazi bure.

Tuanze je Imani tupu inaweza kukuokoa. Yakobo 2:14 Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! Ile imani yaweza kumwokoa?
hilo ni swali je Imani bila matendo inakuokoa, sasa Mimi majibu yote yatatoka kwenye maandiko.

Yakobo 2:18 Lakini mtu atasema, Wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa njia ya matendo yangu.

sasa kama biblia inasema Imani na matendo. Je Imani pasipo tendo ni hiyo Imani ni nini?

Yakobo 2:17 Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake.
Na hii ndio maana biblia inasema shetani naye ana Imani ila Hana matendo
Yakobo 2:19 Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka.

Je Imani ndio ubatizo?
Waebrania 11:1 Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.

Tukija kwenye ubatizo ni dhamiri Safi mbele za Mungu ya kwamba umeipokea na kuikubali hiyo Imani.

Hebu tusome katika matendo ili tuwaone walioipokea Imani walifanyaje;

Matendo ya Mitume 2:40-41
40 Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi.

41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu ta
tu.

Unaona ilivyo tamu hiyo walioipokea Neno lake wakabatizwa.

SAsa twende katka vifungu ulivyovichukua ww
yohana 3:16
16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Sasa ona ....... Ili kila mtu amuaminiye asipotee.... Ina maana kwamba kila mtu amuaminiye asipotee . Je Yesu angekuja halafu asingesema chochote ktk maisha yake ungemuaminije? Kwa hiyo tunapata kwamba kuamini sio kuuamini mawili wake Tu Bali kila alichosema kwa sababu yeye ni Neno yohana 1:1. Hivyo kila Neno atakalolisema ulipokeee(uliamini) na baada ya kupoea unalitenda. Ili Ile Imani isife hiyo ndio sababu mitume walieleza vizuri kwamba baada ya kuamini unapaswa ubatizwe, tena kwa jina lake YESU KRISTO.
 
Back
Top Bottom