Je, Unajua utofauti wa vitu hivi viwili?

Je, Unajua utofauti wa vitu hivi viwili?

Reality of heaven

Senior Member
Joined
Nov 2, 2022
Posts
108
Reaction score
353
Leo nizungumzie vitu hivi viwili vinavyowachanganya watu, "DINI" na "WOKOVU, wengi hawajui utofauti, lakini huu ndo utofauti wake:

1: Dini imeletwa na wanadamu kwa lengo la kumkaribia Mungu lakini sio kufika kwake, wakati wokovu umeletwa na Yesu ili kuwafikisha mbinguni.

2: Dini haiondoi dhambi, lakini wokovu unaondoa dhambi.

3: Dini inatetewa na wanadamu wakati wokovu unatetewa na Bwana Yesu.

4: Kila mmoja ana dini yake, lakini sio kila mmoja aliye na wokovu.

5: Dini mtu anaweza kuipata kwa njia ya kurithi wakati wokovu unapatikana kwa njia ya kumwamini Yesu Kristo.

6: Dini huongozwa kwa taratibu za watu,na miongozo yao, wakati aliye na wokovu anaongozwa na Neno la Mungu chini ya uongozi wa Roho mtakatifu.

6: Bila dini utamuona Mungu, lakini bila wokovu huwezi kumuona Mungu.

7: Walio wa Mungu hawana dini, wakati kwenye swala la wokovu lazima uwe nao.

8: Mtu mwenye dini, ni mzinzi, ni mlevi, mla rushwa, mfisadi, mwasherati, muongo, mwizi, muuaji, mvuta sigara, msengenyaji, nk! Lakini aliye na wokovu hujilinda na vyitu hivyo, wala vyitu hivyo havina nafasi katika maisha yake!

FAIDA ZA WOKOVU
1: Unakuwa mtoto wa Mungu kwa njia Bwana Yesu
2: Unaoshwa dhambi zako zote
3: Unakuwa mtakatifu mwili na roho
4: Hutupwi jehannum ya moto, baada ya kifo
5: Huwezi kusumbuliwa na wachawi, waganga nk, unakuwa chin
 
Unakuwa chini ya ulinzi wa Mungu,

Namna ya kupata wokovu

Wokovu unapatikana kwa njia ya kumwamini Bwana Yesu kuwa Bwana na mwokozi wako, baada ya hapo unatafuta kanisa lolote la kiroho unadumu katika fundisho la Kristo,

Achana na dini ndugu yangu, mtu aliye na dini anaweza kufugq majini, wakati aliye na wokovu majini yapo mbali naye!

Aliye na dini anaamini kwamba hakuna mtakatifu duniani, wakati aliye na wokovu yeye ni mtakatifu , na kwa njia hiyo watakatifu wapo wengi duniani pia,

Aliye na dini anaamini akishakufa atafanyiwa maombi ya kuingia mbinguni wakati kwa njia ya wokovu, hakuna wokovu mwingine zaidi ya huu wa hapa duniqni, mtu baada ya kufa ni hukumu ya kwenda motoni au mbinguni

Mwamini Yesu ndugu yangu kabla haujachelewa!!!!baada ya kifo ni hukumu
 
Ndio maana ukristo sio dini kama uislam unavonenwa. Yesu Kristo hakuwahi kuleta dini duniani.
 
Back
Top Bottom