Leo nimeshangazwa na jambo nililoliona pale ubungo stand ya mkoa. Usafiri wa kutoka kibamba, mbezi, kimara na ubungo kuelekea posta siku zote nyakati za asubuhi na jioni huwa niwa tabu sana. Kumetokea kawaida ya watu wenye magari binafsi wanaoelekea posta kusaidia watu kwa kuwataka wachangie mafuta kidogo. its real sh. 4,000 au 6,000 huwezi kusema ni profit kwa mtu anayetumia gari kwenye follen kutoka ubungo kwenda posta.
Kitu kilichonishangaza leo nikiwa nasubiri hizo gari ilitokea gari moja na kupaki kisha watu wakawa wanagombania kuingia. cha ajabu walitokea watu 3 mmoja akaingiza mkono kwa dreva na kutaka kuchomoa funguo wa gari kwa maana kuwa anachokifanya yule mwenye gari ni kuvunja sheria.
Jamani hivi kweli ni sawa? ni bora watu waendelea kusota kituoni na wenye magari waende posta wakiwa tupu kwa vile tu gari yake haijasajiliwa kubeba abiria? Je kama takakuwa amebeba familia yake hao watu (labda askari au whatever maana mimi siwaelewi kwakweli) watashusha ile familia ya dreva wa gari? je sasa hivi private car haziruhusiwi kutoa lift kwa watu.
Naomba mwenye ufahamu wa hili anieleweshe maana hadi sasa niko kwenye mshangao!