Safari_ni_Safari
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 23,265
- 17,120
Watu wengi wanapenda ulaji wa kuku waliopikwa kwa staili hii pasi na kujua asili yake.
Mzee Robert Makange (1928-1999)
Mzee huyu wengi hawamfahamu ila wanafahamu chakula chake alichokiasisi kilichopewa jina la Makange. Mzee Makange alikiasisi chakula hicho katika Bar yake ya Tropicana Club aliyokuwa akimiliki mtaa wa Nkrumah, jirani na Bustani ya Mnazi Mmoja upande wa chini. Katika eneo hilo zamani palikuwa ni Makao Makuu ya chama cha Umoja wa madereva teksi cha Co-Cabs. Umaarufu wa "Kuku wa Makange" ulijulikana kiasi kwamba hadi hii leo jina hilo limekuwa likitumika ama kujulikana na karibu kila mtu nchini kama aina fulani ya mlo mtamu wa Kuku wa kukaanga, hatua iliyopelekea hadi kuzaliwa kwa vyakula vingine vya Makange kama Samaki Makange au Mbuzi/Ng'ombe Makange.
Lakini ni wachache wanaojua kwamba Mzee Makange alikuwa mmoja wa Wanaharakati Wafanyabiashara wakubwa waliopigania Uhuru. Mzee Makange alikuwa mwandishi na Mhariri wa gazeti la "Mwafrika" kati ya mwaka 1957 hadi 1961. Gazeti hilo lilikuwa likichapishwa kwenye kiwanda cha Pan African Publishing House walichokuwa wakiiendeesha yeye, pamoja na Mzee Chiume na Mzee Kheri Rashidi Baghelleh hapo hapo Tropicana Club kwa nyuma.
Gazeti hilo lilifanya kazi kubwa ya kueneza siasa ya TANU ya kudai Uhuru. Mwaka 1958, Marehemu Mzee Makange pamoja na mmiliki mwenzake, Kheri Rashidi Baghelleh, walifungwa miezi 6 na Serikali ya mkoloni kwa tuhuma za uchochezi.

Maandiko ambayo yaliwapeleka jela ni haya hapa:
"Sisi wote tunajua kuwa Mwingereza yupo hapa kwetu kwa sababu ya kutunyonya damu na kujipatia manufaa yake mwenyewe, na wala asitudanganye kwamba yupo hapa kwakuwa anatuonea huruma na kutaka kutufundisha ustaarabu au kuleta maendeleo ya nchi. Maneno haya ni kigeugeu cha kutaka kutufunika macho; na kwa kadri atakavyozidi kuwa hapa ndivyo madini na fedha zitakavyozidi kutolewa katika nchi hii kupelekwa kwao, ambako bila ya sisi hawawezi kuishi sawasawa.“
(Mwafrika [weekly edition], No. 19, June 1st 1958, p. 5)
Mzee Makange pia alikuwa ni mtunzi wa vitabu mbali mbali kupitia kampuni ya uandishi na uchapaji ya Pan-African Publishing Company aliyoiongoza kwa miaka mingi pamoja na rafiki yake wa karibu, Mzee Kanyama Chiume.

Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari wa zamani Marehemu Kanyama Chiume (kushoto) na Marehemu Robert Makange(kulia) katika viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam mwaka 1985 siku chache kabla ya Baba wa Taifa kustaafu Urais.