Je, unamfahamu Rashid Ally Meri?

Je, unamfahamu Rashid Ally Meri?

Omari Makoo

Member
Joined
Sep 6, 2016
Posts
78
Reaction score
39
Je, unamjua Rashid Ally Meri?

Na Mwl Omari A. Makoo


Huyu ni kijana wa zamani ambaye alifanya kazi katika ofisi za Dar es salam municipal council akiwa kama mweka hazina.

Huyu alikuwa ni mmoja ya wajumbe 20 waliohudhuria mkutano wa mwanzo wa TANU wa mwaka 1955 wakiwa pamoja na kina mzee Chaurembo,Said Chamwenyewe,Abdul wahid Sykes,Dosa Aziz,L.Seat on,Clement Mtamila na wengine wengi.

Wakati TANU wanapanga safari ya Mwl Nyerere kwenda UNO pesa hazikutosha hivyo changisha changisha ikaanza,Mzee rupia akachangia theluthi ya gharama,kisha Iddi faizi mafongo akatoa pesa za jamiatul muslim kuongezea gharama za nauli na chakula cha safarini kwa Mwl Nyerere.

Lakini hazikutosha hivyo Mwl kahere Kule Tanga akaagiza TANU waende Tanga kuchukua mchango wao.
Wakati ule nauli ya kwenda marekani ilikuwa 12000.

Iddi faizi Mafongo alipoenda Tanga kuifuata pesa Special branch wakapata taarifa(usalama wa taifa wa enzi hizo)
Hivyo wakakusudia kumkamata njiani akiwa anarudi kutokea Tanga.

Walifanikiwa kusimamisha basi alilopanda pale Turiani lakini walipomkagua hawakumkuta hata na senti.Iddi faizi Mafongo pesa ile alimpa binti yake mdogo ambaye special branch hawakumkagua.Hivyo pesa ikawafikia TANU kama ilivyokusudiwa.

Turudi kwa mlengwa wetu Rashid Ally Meri ambaye nae baada ya kuona pesa hazitoshi alikwenda kubeba pesa za Dar es salaam municipal council na kuwapa TANU kwa sharti warejeshe pale tu watakapopata Kabla haijagundulika.

Chaajabu kesho yake tu special branch wakapata taarifa na kupekeleka auditors ofisini kwake na kuomba kukagua mapato na matumizi.

Siku ile ile jioni Rashid Ally Meri akawaona viongozi wa TANU na kuwahadithia. Kilichotokea. TANU wakajichanga ili kumuokoa Rashid Ally Meri asije akafungwa.

Pesa ikapatikana akafanikiwa kuirejesha kabla mambo hayajaharibika. Huyo ndio Rashid Ally Meri mmoja ya wapigania uhuru wa Tanganyika.

c050a1_a5596107b6824f52903b4a34ec50c6c2.jpg

Kushoto: Rashid Sisso, Robert Makange, Zuberi Mtemvu, Iddi Faiz Mafongo, Julius Nyerere, John Rupia na Bi. Titi Mohamed Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam Kumsindikiza Nyerere Akienda Umoja wa Mataifa New York, 1955
 
Daaah asantee kwa historia adhimu, inaonekana kuna mambo mengi sana kuhusu Uhuru wa nchi yetu hatuyajui. Mungu awabariki wote waliojitolea kwa moyo, hali na Mali kwa ajili ya Uhuru wetu. I love them all.
 
Mbona hao watu hawakuwekwa kwenye historia ya kupigania uhuru wetu kwenye vitabu vya Elimu ya msingi?
Ndio utambue kuwa ulilishwa matango from primary to secondary schools.

Ni jambo la ajabu na aibu kwa nchi kuficha Historia yake kwa sababu ya kutimiza matakwa ya kikundi flani cha watu.
 
Mbona hao watu hawakuwekwa kwenye historia ya kupigania uhuru wetu kwenye vitabu vya Elimu ya msingi?
kumekuwa na changamoto katika hilo,historia nyingi zimejikita kwenye shujaa mmoja.Hivyo na Tz shujaa aliyeinuliwa ni Nyerere pekee yake
 
Historia ya taifa inafichwa ni vema kuanza sasa kuitengeneza wazi historia ya nchi yetu, hapa serikali isifumbie macho.
 
Mohamedi said amafanya kazi kubwa sana maana asilimia zaida ya sabini ya maelezo ya uhuru wa tanganyika source ni mohamed said huyu jamaa mungu ampe maisha marefu hapa duniani ili aweze kutujuza.

Tunashukuru mtoa post kwa kutukumbusha
 
Hayo yote itayapata kwenye kitabu cha mohamed said sykes hao ndio wapambanaji wa kweli
 
Back
Top Bottom