Je, unamjua Louis P Sazia, aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro na mbunge wa Kahama?

Je, unamjua Louis P Sazia, aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro na mbunge wa Kahama?

Yopinto

Member
Joined
Jul 27, 2021
Posts
61
Reaction score
62
Ee bwana wanyamwezi walikuwa na huyu mzee ambaye kwa sasa ni MarehemU, alikuwa jembe na nusu.

Huyu mzee alikuwa awe chief baada ya baba yake Andrea Sazia, lakini uhuru ndipo ulipatikana na hivyo uchief ukawekwa pembeni, huyu mzee alitokea familia ya kitawala huko kwa Wanyamwezi walioshi Shinyanga.

Baba wa taifa alimpa kuwa waziri wa kazi kama sio wa ardhi miaka ya 60 hivi, jamaa alikuwa kichwa kwelikweli.
Baada ya hapo alikuja kuwa mkuu wa mkoa huko Kilimanjaro, ukifatilia vizuri unaambiwa jamaa alikuwa polite na mpenda haki.

Elimu yake haijawekwa wazi ila unajua watoto wa machief walivyokuwa wanapewa kipaumbele kwenye elimu basi ni wazi jamaa alikipiga sana.

Cha ajabu sijaona mtoto wake ama mjukuu wake kwenye tasnia ya politics tena, na pia familia yake ni kama haijakaa wazi sana, au ni watu wa mifumo nini?

Nilisikia alikuwa na mtoto wake pale kilimanjaro ambaye hawakuwahi kuonana mpaka mzee alipoaga dunia.

Na pia nilipata Habari kuwa kifo chake kina utata fulani hivi, si unajua wapenda haki wanavyokutanishwa, ni tetesi tu wazee.

Na pia nilisikia ana mjukuu wake alikuwa anapenda usanii pia amefanya kazi media tofauti tofauti hapa tz anaitwa Mapembe, kitu kama Aloy Mapembe.

Huyu mzee niliposikia historia yake imenishangaza sana 😢 maana hakuna hata ndugu anayeendelea na masuala ya siasa tena. So sad.
 
Back
Top Bottom