Je unamjua mtu wa kwanza aliyegundua simu ?

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564

mgunduzi wa simu aliye keti: Alexander Graham Bell.

Mnamo mwaka 1876 tarehe 11 mwezi march bwana Alexander Graham Bell alifanikiwa kutengeneza simu ya kwanza kabisa. alizaliwa mnamo mwezi March tarehe 3, mwaka 1847 na kufariki dunia –mwezi August tarehe 2, mwaka 1922. Baba yake babu yake na kaka yake wote walikua wakijihusisha na maswala ya namna ya uzungumzaji pamoja matamshi yanii (elocution and speech).

Wakati mkewe ndiye aliye mvutia na kumshawishi Alexander Graham Bell aweze kuzama ndani zaidi ki uchunguzi kwa kufanya uchunguzi katika matamshi na usikilizaji baadae alikwenda zaidi kuchunguza ni jinsi gani vifaa vya kusikilizia sauti hufanya kazi hapo ndipo alipo weza kuibuka na simu yakwanza yenye kufanya kazi.

Alizawadiwa tuzo iliyo fahamika kama first U.S patent mnamo mwaka 1847 pamoja na hayo alikataa kutumia simu kwa matumizi yake binafsi katika kipindi chake chote pamoja na kua alikuwa akiendelea na masomo.
 
Pamoja na kwamba simu zimerahisisha mambo mengi, lakini pia zimeleta madhara makubwa sana kwa familia, mahusiano, na afya za watumiaji.
Kiukweli sipendi kabisa sim, ingawa nalazimika kuitumia ili niendane na wakati na hasa utandawazi
 
Usisahau hilo neno Heloo limetokana na jina la mke wake Grahmbell aliyeitwa Magreth Helloo baada ya kufanikiwa kutengeneza simu akajaribu kumpigia mkewe akasema Heloooooo hapo anamwita jina lake. Ndipo ikapitishwa kabisa
 
Kwa kuongezea tu huyo mkewe magreth inasemekana alikuwa kiziwi sasa jiulize jamaa alitaka kuwasiliana na nani
 
mgunduzi wa simu aliye keti: Alexander Graham Bell.

Mnamo mwaka 1876 tarehe 11 mwezi march bwana Alexander Graham Bell alifanikiwa kutengeneza simu ya kwanza kabisa. alizaliwa mnamo mwezi March tarehe 3, mwaka 1847 na kufariki dunia –mwezi August tarehe 2, mwaka 1922. Baba yake babu yake na kaka yake wote walikua wakijihusisha na maswala ya namna ya uzungumzaji pamoja matamshi yanii (elocution and speech).

Wakati mkewe ndiye aliye mvutia na kumshawishi Alexander Graham Bell aweze kuzama ndani zaidi ki uchunguzi kwa kufanya uchunguzi katika matamshi na usikilizaji baadae alikwenda zaidi kuchunguza ni jinsi gani vifaa vya kusikilizia sauti hufanya kazi hapo ndipo alipo weza kuibuka na simu yakwanza yenye kufanya kazi.

Alizawadiwa tuzo iliyo fahamika kama first U.S patent mnamo mwaka 1847 pamoja na hayo alikataa kutumia simu kwa matumizi yake binafsi katika kipindi chake chote pamoja na kua alikuwa akiendelea na masomo.
Ila we jamaa muongo muongo. Ina maana Bell alizaliwa mwaka 1847 akagundua simu mwaka 1876 alafu akapewa tuzo ya First US Patent mwaka 1847??

Ebu tueleweshe kidogo hapo naona sijaelewa. Au alipewa tuzo in advance?
 
Mbona mimi ni mgunduzi wa noti za 700 na 1200 zinazotumika Bongo ila siandikwi au wanahitajika wazingu tu
 
Simu hiyo aliwasiliana na nani, au ilichezewa game tuu?
 
Back
Top Bottom