JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Gharama za Intaneti zimekuwa zikikwamisha na kuathiri shughuli za Watumiaji wa Mitandao, Wabunifu wa Teknolojia na Wazalishaji wa Maudhui
Je, unaridhishwa na mikakati ya Serikali katika udhibiti wa Bei za Intaneti? Unaathirika vipi na Gharama za Intaneti nchini?
Ungana nasi katika Mjadala kuhusu Hatma ya Tanzania ya Kidigitali kwa kutazama Sera, Sheria, Matamko ya Viongozi na Kodi zinavyoathiri Ukuaji wa Sekta ya Digitali nchini
Ni leo Alhamisi Juni 20, 2024 kuanzia Saa 12 Jioni hadi saa 2 Usiku kupitia XSpaces ya JamiiForums
Kusikiliza mjadala na kushikiriki kupitia XSpaces bofya x.com
--
Rachel Magege (Pollicy):
Nimekuwa nafuatilia sana sera na Sheria za Masuala ya Digitali. Kuna sera kama tano muhimu zimetungwa hivi karibuni na Wizara inaendelea kutoa muda kwa Wadau kutoa maoni yao. Mara nyingi Sera na matamko huwa yanawasilishwa kwa Lugha ngumu lakini tuko hapa kwa ajili ya kuelewesha Umma ili wapate kuzielewa.
Sera Digital Economic Framework ni ya Miaka 10. Sera hii imegusia mambo kama kutengeneza 'system' itakayoruhusu mwingiliano wa Mifumo ya Kidijitali mfano Elimu, Utalii. Aidha, kwenye Sera hii kuna Jamii Namba. Namba hii moja itamtambulisha Mtanzania.
Pia, Sera hii imegusia AI, tayari Tanzania imeanza kutunga Sheria ya Akili Mnemba na muda si mrefu itakuwa kwa matumizi ya Jamii.
Changamoto ya Sera hii ni kukosa ujumuishwaji. Watanzania wengi wa Vijijini watashindwa kunufaika kwasababu wengi hawana hata NIDA na hawatumii Simu Janja. Pia, Sera zimeandikwa kwa lugha ya Kiingereza ambayo haieleweki na wengi.
Kuna wakati tulifuatilia Akaunti za Mitandao ya Kijamii za Madiwani hasa wakati wa uchaguzi, tulibaini kulikuwa na mazingira makubwa ya udhalilishaji hasa kwa Wanawake
Kuna haja kubwa ya kutoa elimu kwa Watumiaji wote kuhusu matumizi ya Mitandao kwa kuwa kumekuwa na watu wengi wanaotumia kuumiza wengine
KENNEDY MMARI (Mkurugenzi Mtendaji - Serengeti Bytes):
Kuna vitu kadhaa vya kuangalia, kwamba vitu vikoje katika mazingira ya kidijitali ya Tanzania. Tanzania kama nchi nyingine ina Sheria, Sera na Matamko yanayowezesha Uchumi wa Kidigitali.
Nitaanza kwa kugusia sheria ambazo zina impact kwenye Uchumi wa Kidigitali
Sera ya ICT ya 2016 hadi sasa tunaweza kuipa credit kwa kusaidia kuchagiza maendeleo ya Miundombinu ya kidigitali. Sera hii iliweka msingi ambao ulisababisha uwekezaji mkubwa.
Pia, mfumo wa Serikali wa E-Government una 'impact' kubwa sana kwa sababu umerahisha mambo mengi na 'kusave' muda ambao umetumika kwenye Shughuli nyingine za uzalishaji.
Finance act ya 2022 ambayo inaregulate masuala ya kodi katika mambo ya kidigitali kama online content creation
Tunavyafanya taxation ni vizuri kuangalia hali halisi ya mazingira ya uchumi wa kidigitali Nchini.
Sheria ya EPOCA imekuja na changamoto nyingi ikiwemo kupunguza uhuru wa kuweka maudhui mtandaoni, hivyo imeminya Uhuru wa kujieleza.
Pia imepunguza idadi ya Waandaa maudhui wa Mtandaoni kutokana na kulazimika kulipia vitu kama Youtube na Blogs.
Tunapaswa kuhakikisha Sera na Sheria zetu zinapaswa kuwa na Consistence. Kama tunataka na tunakusudia kukuza sekta ya Digitali ni lazima Sera na Sheria ziakisi hivyo tupunguze na tuondoe over regulation ya Uchumi wa kidigitali. Tuwe na regime inayo-facilitate na sio ku-over regulate.
Tunabeba matatizo yetu mengi kwenda kwenye Uchumi wa Digitali. Kwasababu hatujawawezesha makundi mbalimbali kustrive katika Uchumi wa Kidigitali.
Gender devide inaendelea kuwa kubwa katika uchumi wa kidigitali, pia tofauti ya Watu wa Mjini na Vijijini.
Tuna Sheria zetu zinakuwa reactive na sio kwaajili ya kuongoza. Mfano, Dunia inazungumzia zaidi kuhusu Akili Mnemba, itakapoanza kutumia kwetu Sheria zetu zinaweza kueelekea kwenye kudhibiti na sio kuongoza.
Uelewa wa Kidigitali bado upo chini sana Nchini, mfano hadi leo nikitangaza ajira, kuna Watu hawajui kuambatanisha, wengine hawajui misingi ya muhimu ya kufanya maombi. Hiyo inaturudisha nyuma kuwa kuna msingi unakosekana kuanzia kwenye elimu ya chini.
Kama Mtu hawezi kuandika barua pepe inamaanisha kuwa kuna changamoto ambayo inakabili Nchi kwenye suala la Digitali ili tufikie kiwango cha kuanza kuwalipisha au kupata kodi Serikali inatakiwa kutengeneza na kuwaandaa Wadau wa Digitali.
GODLISTEN MALISA (Mtetezi wa Haki za Kijamii):
Mimi nitazungumzia Changamoto ambazo watumiaji wa Mitandao Nchini Tanzania wanakabiliana nazo kutokana na Sera na Matamko ya Serikali
Sera, Sheria na Matamko ya kwenye karatasi yana matumaini lakini changamoto ni kwenye utekelezaji hasa Viongozi wanaopaswa kutekeleza wakikosa utashi (Political Will).
Ni bahati kwamba katika Nchi yetu tunafikiri kwamba Mwanasiasa ana akili kuliko wengine, yaani kila linalosemwa na Wanasiasa ni sahihi. Ukweli ni kwamba tunapaswa kwenda sawa na ulimwengu wa Kidigitali, na uvumbuzi unaotokea kila siku. Kwasababu viongozi wanapotuambia kuna maudhui yasiyofaa mtandaoni na namna ya kukabiliana ni kufungia mtandao fulani na tunapiga makofi, hio sio sawa.
Swali la msingi ni je, kuifunga ni suluhusho?
Watumiaji wa Mitandao ni walewale. Sasa mtu akiweka maudhui X ukaifungia, ataenda kuweka Facebook, Instagram au YouTube, je, utafungia na huko?
Kwa hiyo mimi naona kufungia mtandao sio sawa, na pia kama kiongozi anasema ifungiwe basi tubishane nae kwa hoja.
Ni bahati mbaya katika Nchi yetu tuna utamaduni wa kufikiri kuwa Mtu mwenye nafasi ya Kisiasa ana akili kuliko watu wengine na kila linalosemwa na Viongozi wa kisiasa ni jambo sahihi. Ulimwengu wa Kidigitali na maboresho yanayofanyika kila siku tunatapaswa kwenda nayo inayovyotakiwa. Viongozi wakituambia kuna maudhui yasiyofaa basi tunapiga makofi, sio sawa
Tokea Sheria ya Cyber crime ianzishwe ni watu wangapi wameshafikishwa mahakamani kwa kupost picha za utupu au kutukana watu mtandaoni? Mpaka unaweza kusema Sheria hiyo ilitungwa kwa ajili ya Wakosoaji wa Mitandaoni. Kuna wadada na wakaka wanaocheza picha za utupu huko mtandaoni lakini hawachukuliwi hatua. Victims ni Mimi, Mdude, Yericko, Bob Wangwe na Wengine.
Tusipokuwa na Sera nzuri tukaishia kuendelea kuamini katika matakwa ya Kiongozi na tutakuwa hatusongi mbele, mambo ya Mitandao yanatakiwa kuwekwa kwenye Sera. Mambo kama ya ubaguzi yamezungumzwa kwenye Sheria zetu, mfano Kifungu cha 18 cha Makosa ya Mtandao kipo
Hivi karibuni kuna kiongozi wa CCM alizungumza kuonesha anataka Watu fulani wauawe kwa kuwa walikuwa kinyume na kile alichokuwa akiamini yeye lakini hakukuwa na hatua zilizochukuliwa.
Watengeneza Maudhui wanatakiwa kukatwa kodi lakini Serikali inafanya hivyo bila kuwatengenezea mazingira ya wao kuingiza kipato. Wapo (Watengeneza Maudhui) mbao wanafanya hivyo kwa fedha zao wenyewe kisha Serikali inataka kuja kuwakata kodi.
Kuna Watengeneza Maudhui ambao wanaweza kutangaza bidhaa ambazo tayari zimeshalipiwa kodi, wao wakikatwa inamaanisha malipo yatakuwa yanafanyika mara mbili.
Baadhi ya Watengeneza Maudhui wanapoenda kurekodi maudhui yao mfano pale Ukumbi wa Makumbusho watakutana na mzingira magumu ya urasimu, sio hapo tu, zipo sehemu nyingi ambazo sio rafiki kwao.
Hivi karibuni, Dunia ilikutana Kidigitali Nchini kulikuwa na Wadau wengi lakini Serikali ya Tanzania haikuwa na uwakilishi, walikuwepo Watu wachache kutoka kwenye sekta binafsi. Sasa Waziri au Serikali hawapo kwenye matukio muhimu kama hayo inawezaje kuwalipisha Watu wa Digitali ambao pia hawana mazingira ya kuingiza kipato.
Ikitokea Serikali yenyewe ikatumia taarifa zetu isivyofaa, nani ataichukulia hatua Serikali?
Miaka kadhaa iliyopita JamiiForums walipata changamoto wakatakiwa kutoa taarifa za Wateja wao, walisimama kidete hawakutoa taarifa lakini Serikali ilisisitiza kutaka taarifa hizo. Tunamshuku Mkurugenzi wa JamiiForums, Maxence Melo hakuwa tayari kutoa hizo taarifa kwa kuwa kama angetoa pengine leo tusingkuwa hapa. Tunashukuru tumevuka hizo zama lakini tunatakiwa kujiuliza kuwa Serikali ikifanya uhalifu, sisi tutaenda kushtaki kwa nani?
Mimi ni Mtumiaji wa Mtandao wa X, maudhui ya ngono huwa siyaoni, kwa kawaida unapoingia Mtandaoni yale mambo ambayo unapendelea kuyaangalia ndiyo ambayo ukifungua yanakuja kwako pia mara kwa mara. Sasa inakuwaje mambo ambayo wewe ni kipaumbele chako unayopenda kuyafuatilia yanakutokea unataka usababishe Watu wote wafungiwe?
WARDA MANSOUR (Mtayarishaji Maudhui Mtandaoni):
Tunaona wenzetu kwa haraharaka Digital Content Creators wanalipwa vizuri. Kwa mtu ambaye anapata watazamaji wengi wa Maudhui wanapata hela nzuri kwa Mwezi. Creators wa Tiktok wa Tanzania hawajawekwa kwenye plan ya malipo kwasababu watu wetu hawalipii matangazo huko Tiktok.
Jamii ya Watanzania inashindwa kuwatambua Digital Creators. Kawaida ukisema wewe ni Content creator unaonekana hauko serious na maisha. Pia juzijuzi BASATA ilisema haiwatambui hawa creators, lakini ikija kwenye tax wanatutambua. Sasa kama hawatutambui tukiwa na changamoto tunasema wapi?
ANDRO (Mdau):
Ninavyoona Serikali inaendesha masuala ya Mitandao kama kitu cha ziada na siyo cha lazima, hiyo inachangia kuwa na uzito katika kurasimisha shughuli za Mtandao. Hiyo inachangia matishio ya Mitandao kufungwa au kufanywa vile kitu ambacho sio cha kweli.
Nasisitiza kuwa fikra ya Serikali kufikiria Mtandao ni kitu ambacho si cha lazima iondoke, tuliona hivi karibuni Mtandao ulivyosumbua, Watu wengi walipata wakati mgumu na ilikuwa changamoto pia hata kwa Serikali
Dunia ipo kwenye Digitali sisi pia hatutakiwi kuwa nyuma ya kile kinachoendelea kwa wenzetu
KAMALA DICKSON
Nimeona Bunge, leo limetoa nafasi kwa Wadau wanaoweza kutoa maoni katika Finance Bill, nadhani hiyo ni nafasi nzuri kwa Wadau kushiriki na kufikisha ujumbe ambao tunataka uifikie Serikali.
Sidhani kama Tanzania tuna Mmalaka ambayo inaweza kusimamia Watengeneza Maudhui wa Mitandaoni
Kwa tafsiri ilivyo je, hawa Watengeneza Maudhui wa Mitandaoni ni kina nani na wanasimamiwa na Sera ipi? Kuna haja ya kuipa muda Serikali kufuatilia na kuja na majibu hayo kabla ya kupitisha masuala mengine ya Kodi
Kuna shida kubwa katika kuelewa suala hilo la kuratibu Watengeneza Maudhui Mtandaoni katika masuala ya kodi na makato mengine
Mfano, Mtengeneza Maudhui anapopata nafasi ya kufanya kazi na Kampuni fulani, je malipo yake yanatakiwa kukata kodi pia au tunaweza kuwa tunakata kodi mara mbili
Hilo jambo la kulipisha Watengeneza Maudhui ni nzuri lakini tunahitaji muda kuwa na majibu sahihi, mfano changamoto ya sasa ni kuhusu wahusika hao wanaingizaje kipato? Je, Mamlaka zimechunguza kipato chao kinatoka wapi na kinaingiaje?
Serikali inatakiwa kuwekeza katika sekta hiyo kabla ya kufanya maamuzi bila kujua vijana wanatumia nguvu kiasi gani kuingiza kipato wanachoingiza
Nitoe Mfano, kabla ya kuaza kuwabana Vijanao waliopo kwenye Mitandao, wanaweza kutumiwa na Serikali kwanza
Wizara ya Afya imekuwa na kampeni mbalimbali, kwanini wasiwatumie Watengeneza Maudhui hao ili wapime nguvu yao kuona inaweza kufika wapi na wanaingizaje kipato kabla ya kuchukua hatua bila kujua uhalisia wa kile wnachopitia wahusika
NAUMANGA JR (Mdau):
Nitoe elimu kidogo, ninavyoelewa ipo Sheria ya Mwaka 2020 inayowaongoza Watengeneza Maudhui na wanasimamiwa na TCRA, pia Sheria inaeleza kuwa watengeneza maudhui wanatakiwa kuwa na leseni
Pamoja na uwezo wa Sheria kuna mazingira ambayo yanaweza kubana Watu wanaotumia, hasa katika zile zinazozungumzia maudhui yanayozuiwa
Sheria ya kuzuia mahudhui ya ngono Mitandaoni ipo, hivyo haina haja ya kufungia Mtandao wakati Sheria ipo na wo wanaweza kuhusika wanaoweka maudhui hayo
Sheria zilizopo isijekuwa zinataka kutumika kuwalenga Watu fulani na sio kwa nia ya kweli ya kuondoa maudhui ya picha chafu
DIGITAL NOMAD (Mdau):
Kuna baadhi ya Sera zinatakiwa kubadilika, ya kwanza ni namna ya kuandaa Vipaji vyetu hasa wanaotoka Vyuoni, kuna ushindani mkubwa kwenye Soko la Ajira kwa kuwa kazi anayoomba Kijana wa Kitanzania pia anaomba na Kijana kutoka nje kwa njia ya Mtandao.
Sijaona Kiongozi wa Tanzania akizungumzia au akihamasisha suala la ajira za Mtandao, kama ipo basi itakuwa imenipita. Viongozi wetu na Mamlaka wanatakiwa kuingia na kuwekeza huko kwenye kuwezesha elimu ya Digitali ili Vijana wa Tanzania waweza kuendana na soko la Kidigitali Duniani
Hapa Tanzania mtu anawea kuwa wa wafuasi zaidi ya Milioni 1 lakini akawa haingizi kipato, tofauti na Nchi kama Nigeria, mtu anaweza kuwa na wafuasi 200,000 Mtandaoni na akaingiza fedha
Kinachotaka kufanyika kwa Watengeneza Maudhui kulipishwa kodi na makato mengine kama hayo ni kama Serikali inataka kula kwa kitu ambacho haijakiandaa. Inatakiwa kuandaa Watengeneza Maudhui kwa kuwatengenezea maudhui mazingira mazuri