Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi? Karibu tushauriane hapa

Naomba kuuliza msimu mzuri wa kulima vitunguu maji na soko linakuwa la uhakiki ni upi? Asante.
 
Kwa nchi nzima msimu wenye pesa kwa kitunguu, ni ukivune na ukiuze mwezi novemba hadi april. Kwa mfano mpaka jana gunia la kilo 140, lilikuwa tsh 140,000. Last week lililkuwa tsh 120,000

naomba kuuliza msimu mzuri wa kulima vitunguu maji na soko linakuwa la uhakiki ni upi? Asante.
 
kilimomaarifa.tajiri Mungu akubariki hapa tunajifunza mengi mno na unajibu kila unachoulizwa kwa ufasaha na kwa moyo mkuu tofauti na wengine wanaouza ushauri huku JF ilhali hata unapomuuliza kitu hajibu kwa ufanisi.
 
Last edited by a moderator:
Asante,je nitahitaji mbegu gram ngapi kwa nusu eka na mbolea mifuko mingapi? Mapato yatakuwa kiasi gani kwa nusu eka,pia je ni mbegu gani nzuri yenxe pato?.
 
Asante sana Kiongozi kwa ushauri na elimu hii adimu. Nimevutiwa na kilimo cha matikiti maji. Napenda kujua miezi ipi kilimo hiki kinaweza kufanyika. Na pia miezi ipi tunda ili linakuwa adimu sana ili niweze kujipanga. Na kama nitahitaji usaidizi wako wa karibu wakati naanza kilimo huko naweza kukupata? Asante sana.
 
Asante kilimomaarifa.tajiri naomba muongozo wako mimi nina miche ya nyanya aina ya eden kama 400 ndio ina kama wiki na nusu,nini cha kufanya miche ikiwa bado kwenye kitalu kwa wakati huu? Pia ninakusudia kupandia mbolea aina ya samadi,je kwa kila shimo nitaweka kiasi gani ili isiunguze mche? Asante mengine nitauliza baadae.
 
Last edited by a moderator:
Asante sana kilimomaarifa.tajiri, kabla ya kuweka mbegu kitaluni nilitanguliza mbolea ya samadi na majivu kidogo na baada ya hapo nikanyunyiza DAP kulingana na maelezo yako ya nyuma. Ukweli si kwamba samadi nimenunua hivyo sina hakika ni ya lini ila kuna ambayo inaonekana ni ya zamani maana imeshakuwa kama udongo, kuna ambayo bado iko kwenye mifuko na nyingine iko tu chini wala sijaifunika duh! Nirudi kwenye kupiga dawa ya kanitangaze,je inapigwa juu ya majani au ni chini kwenye shina? Barikiwa
 
Last edited by a moderator:
Samahani naomba kuuliza eti ridomil ikipigwa ni baada ya muda gani itakuwa imekolea vizuri kwenye mmea, kwani nilipiga kwenye viazi baada ya saa 2 ikanyesha mvua, lakini kuna mtu aliniambia kuwa ridomil ikikaa nusu saa tangia kupigwa itakuwa imeshafanya kazi yake.
 
Asante sana kilimomaarifa.tajiri tunashukuru kuwa huchoki na maswali yetu. Sasa nimetafakari ulichoniambia kuhusu mbolea ni cha msingi sana naona nisipandie samadi nipandie za dukani tu ili niwe na hakika wa ninachokifanya,sasa naomba tena kipimo kipya kwa kila shimo,pili nikishaweka niichanganye kwanza na udongo ama niiache tu ikutane na mizizi direct?
 
Last edited by a moderator:
 
Niliweka mbolea shambani aina ya dap wakati napandikiza miche ya nyanya, sasa nikaishiwa miche na mistari kadhaa ikabaki ikiwa na mbolea. Naomba kuuliza je nikienda kupandikiza miche mingine baada ya wiki mbili ,ile mbolea itakuwa bado na nguvu au itatakiwa niongeze nyingine? Asante.
 

Asante kwa somo hili la tikiti maji.Mkuu ni mara yangu ya kwanza kulima tikiti maji, nimelima aina ya SUKARI F1 yana wiki tatu sasa,niseme tu kwamba sikupanda na mbolea yeyote na wala sijatumia dawa ya kuuwa wadudu hizo ulizotaja hapo kutokana na aliyenishauri kutumia Dawa ya AGRI FOS 400 kwamba inaua pia wadudu japo haifanyi kazi maana wadudu wanakata majani na pia kuna miche inakauka kutoka chini nikashauriwa kutumia AGRI- FOS 400 lakini tatizo bado linaendelea.baada ya kusoma maelezo yako sijaona hii dawa,naomba kujua kuhusu hii dawa isije ikawa inamadhara kwenye miche hii ya tikiti maana nimepiga mara tatu sasa. Na pia naomba kuuliza je kuna booster ya kupiga kwenye miche ambazo bado hazijatambaa ili zitambae haraka?.,Asante
 
Agri fos 400 kutoka kampuni ya balton ni kiboko sana na magonjwa ya mnyauko hasa kwenye nyanya, hoho na mazao mengine ile dawa inaiingia moja kwa moja kwenye mizizi na kutibu, nimepiga kwenye nyanya zangu hivi karibun zilizokua na late bright nimeanza kuona mabadiliko
 
Mkuu EMoj kwa ushauri zaidi ingia google then tafuta iyo dawa ina maelezo yalijitisheleza uku ukimsubiri ndugu yetu Kilimo maaarifa kujibu maswali yako
 
Naomba kuuliza ,je hiyo aqua stiker naweza kuichanganya ninapopiga booster? Asante.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…