Je, unatamani Kufanikiwa katika Kuitangaza na Kukuza Biashara yako Mtandaoni? Soma hapa

Joined
Aug 22, 2022
Posts
9
Reaction score
8
Siri 3 Usizozijua za Social Media Marketing[emoji33]

Je,Unatamani Kufanikiwa Ktk Kutangaza na Kuikuza Biashara yako Mtandaoni?

Basi Tumia Siri hizi 3 ambazo Wafanya Biashara wengi Wanazipuuzia.. Ili uweze Kufanikiwa

(Siri #3 ni ya Muhimu zaidi)

Anza hapa na Siri #1 [emoji1427]

1. Market Research

Na mwisho wa siku Wanahangaika ktk Kuvutia Wateja na kuuza, especially Mtandaoni

[emoji1428] Faida ya kufanya Research kwanza,

Itakusaidia kuona sokoni kuna magepu gani, fursa zipi na mwisho Utaona uingie ktk Angle ipi na Ujiposition vipi ili uvutie zaidi Wateja

[emoji1428] Ruge alikuwa na kauli yake anasema "Anzia Sokoni" .. Anza na Research ya Soko lako na Uwafahamu vizuri Wateja wako Watarajiwa.

2.Quality Matters (Business & Brand)

[emoji1428] Hapa tunaongelea Bidhaa/Huduma unayotoa.. Lazima iwe na Ubora

[emoji1428] Na pia Account yako iwe na Muonekano wa Kiprofessional, Pamoja na Contents zenye Ubora

[emoji1428] Kama ambavyo Unalipamba duka lako liwe kali na la Kuvutia,

[emoji1428] Hakikisha Quality hiyo hiyo unaileta Mtandaoni ktk account yako, iwe na Mpangilio mzuri na wa Kuvutia

[emoji1428] Kuna Jamaa ni YouTuber wa Tech, Marekani, Anaitwa MKBHD,...

Moja kati ya vitu vilivyosaidia kukuza brand yake ni Quality ya Videos zake, kwani Jamaa Anashutia A very Professional camera ya Netflix Movie Standard (RED Camera)

[emoji1428] Usiridhike na Mpangilio mbovu wa contents ktk account yako, au posts za kucopy kila mtu anaweka izo izo kiasi kwamba huwezi tofautisha account flani na flani

[emoji1428] Think BIG, Think QUALITY

3.Build An Audience

[emoji1428] Kama Umefatilia watu Mbalimbali Wanaofundisha Mambo ya Biashara Mtandaoni, basi tayari ushaskia neno CONTENT

[emoji1428] Content ni kitu chochote Unachoposti ktk account yako, mfano picha, Videos etc

[emoji1428] Na kazi ya Content ni Kuelimisha, Kuburudisha na Kuuza

[emoji1428] Lakini Majority ya Contents za wafanya Biashara ni za kuuza, yaani sell, sell, sell..

Hakuna ambae anatoa Contents za Kuelimisha.. Ni wachache sana

[emoji1428] Kama unataka kuuza Continuously, yaani Leo kesho na Keshokutwa..

Jifunze kuwa na Contents Zako, Na ukiweza ziwe Branded kabisa with your Logo & Colors

So that mtu yeyote Anayepitia, na Kujifunza.. Anaifahamu Brand yako pia

Kwanini?

[emoji1428] Kwa sababu Content ndizo zinabuild Audience,

Na ukiwa na Audience kubwa ya watu Wanaokufuatilia.. Utauza Bila Wasiwasi

Utauza kwa Kutumia Brand yako

Na utaweza kujitofautisha na WafanyaBiashara wenzio hata kama mnauza Bidhaa au Kutoa Huduma ile ile

[emoji1428] Hiyo ndiyo nguvu ya Kujenga Brand, watu Wakakufahamu na Kukuamini

Utajuaje Unaposti Content zipi? Anza na Research

BONUS TIP

[emoji1428] Jipe Muda wa Kujenga Brand yako Mtandaoni, watu wote unaowaona ni wakubwa.. 99% yao hawajafika hapo kwa siku moja

[emoji1428] Tumewaona miaka na miaka wanaposti, na kujitangaza na kuboresha Brand zao.. Mpaka Leo ukiwaona Unatamani kuwa kama wao

[emoji1428] Anza kuchukua hatua Leo, Think Long term.. Na Boresha Biashara yako Mtandaoni
Kama una Swali au Mchango ktk Mada, Karibu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…