Je, unaweza kumpunguza ndugu yako?

Je, unaweza kumpunguza ndugu yako?

BWANA WANGU

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2018
Posts
337
Reaction score
797
Habari zenu wakuu,

Ndugu sio kama marafiki, ndugu atuchagui ila tunajikuta wapo kwenye maisha yetu tu. Ndugu ni kiungo muhimu sana kwenye maisha ya kila mtu hasa pale anapokuwa chanya kwako.

Kwa upande mwengine kuna ndugu hasi hawa sio supportive, full majungu, uchawi, ubinafsi na mambo mengine mabaya yanayo fanana na hayo.

Unaweza ukamsaidia huyo ndugu hasi, kwa kusomesha watoto wake, kumnunulia nguo, kumpa mtaji. Lakini ikitokea anguko lako basi atacheka na kupiga makofi kwa nguvu huku akifurahi na tabasamu zito nyuma ya mgongo wako.

Je, unawezaje kuishi na ndugu ambaye ni hasi kama hautaki kuonyesha dalili zozote za kumkataa/ kumtenga.
 
Back
Top Bottom