Je, unaweza kumruhusu partner wako asome sms zako hivi?

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
Je, unaweza kumruhusu partner wako asome sms zako hivi????Kama kuna neno moja la msingi ambalo ni msingi wa ndoa yoyote neon hili ni Uangavu (transparency).

Kamusiinafafanua kwamba neno uangavu maana yake ni kuona kitu moja kwa moja hadi ndani, ni kuwa wazi, kuwa huru kimawasiliano na zaidi ni kuwajibika.
Uangavu katika ndoa maana yake kumuona mpenzi wako hadi ndani na kumfahamu vizuri bila shaka maeneo yote ya maisha yenu.

uangavu katika ndoa ni mwanaume au mwanamke kuweza kusoma sms na kupokea simu za mwenzake bila mashaka wala wasiwasi, kusoma emails zilizomo kwenye inbox yake bila wasiwasi wala hofu, Kufahamu akaunti yake benki ina kiasi gani, kuongea siri zako kwake bila mashaka na zaidi kuwa huru kuhakikisha mwenzako anajisikia vizuri kihisia.
Uangavu ni kuwa wewe bila kuwa na aina yoyote ya unafiki.

wanadamu tuliumbwa na uwezo au hamu ya kutaka kumfahamu mwenzako kwa undani hadi usiwe na shaka wala wasiwasi.
Transparency ni process na haiwezi kutokea usiku mmoja tangu umefahamiana na mpenzi wako ingawa wapo watu ambao hata akiwa kwenye mahusiano hataki mwenzake afahamu mambo yake kitu ambacho si lengo la mahusiano.

Uangavu ni kugundua au kupata uvumbuzi wa mambo mbalimbali mapya kwa mume wako au mke wako kwa sababu ya kuwekana wazi.

Bila kuwa na mawasiliano ambayo ni wazi mahusiano yanaweza kukwama.
Jambo la msingi ni wewe kuwa wazi kueleza kilichondani yako au siri zako kwa mwenzi wako (sincerely & straightfowawrd) na zaidi kushirikiana kupeana habari za kila kitu kinachohusu maisha yenu ili kuondoa wasiwasi, hofu na mashaka kwa mwenzako.

Kuficha vitu si jambo la busara na unapokuwa wazi na mwenzako naye anakuwa wazi kwako kwani kuwa wazi ni kufahamiana na kufahamiana ni mahusiano na binadamu tuliumbwa kuwa na mahusiano.

Je, upo wazi kwa mke wako au mume, au mchumba wako kiasi kwamba chake ni chako na chako ni chake?
 
wengine wake zao wakisoma sms zao wanabaki wanasmile kama hiyo avator kushoto..shocked,
 
kwangu ni kitu cha kawaida sana, nikiwa hm wife mara nyingi hutumia simu yangu ku make calls zake na sms kwa sababu simu huwa na pesa nyingi so anaitumia wala hatufichani yeye yuko huru na mie niko huru na ya kwake tena maisha yanakuwa very simple
 
Endelea hivyo hivyo baba.Inapendeza sana!
 
Hakuna ubaya wowote mpenzi wako kusoma sms yako.Kama hujiamini hapo ndio itakuwa kasheshe.
 
mie nadhani ni vyema tu akasoma

please note :-kuna message huwa zinakosea njia lakini
 
Hahaha! Mi kama anataka kufa kwa presha asome msg zangu. Manake nyingi sana huwa zinakosea njia! Hahaha! Ndio maana mtoto wa watu wala hana taim na simu yake. Na mimi huwa sina time na simu yake. Ila akichomoka kidogo akaisahau, dakika tano nakuwa nimeshakariri namba zote nazozitilia mashaka halafu upelelezi unaendelea. Mi kuisahau simu yangu ni MWIKO. Haijawahi kutokea na wala haitatokea. Hahaha!
 
Hahaha! Mi kama ZD anataka kufa kwa presha asome msg zangu. Manake nyingi sana huwa zinakosea njia! Hahaha! Ndio maana mtoto wa watu wala hana taim na simu yake. Na mimi huwa sina time na simu yake. Ila akichomoka kidogo akaisahau, dakika tano nakuwa nimeshakariri namba zote nazozitilia mashaka halafu upelelezi unaendelea. Mi kuisahau simu yangu ni MWIKO. Haijawahi kutokea na wala haitatokea. Hahaha!
😀😀
 
Bahati mbaya jamaa kakosea ksend SMS kwa demu wake ikaja to u, jamaa ako kaiona utamueleza nini?
 
Hahaha! Mi kama anataka kufa kwa presha asome msg zangu. Manake nyingi sana huwa zinakosea njia! Hahaha! Ndio maana mtoto wa watu wala hana taim na simu yake. Na mimi huwa sina time na simu yake. Ila akichomoka kidogo akaisahau, dakika tano nakuwa nimeshakariri namba zote nazozitilia mashaka halafu upelelezi unaendelea. Mi kuisahau simu yangu ni MWIKO. Haijawahi kutokea na wala haitatokea. Hahaha!

hahahah binamu kumbe na wewe una wivu unasemaga ooh FL1 mbona umezidi ka jelous kumbe na wewe hahahaha napata picha
 
Usiniambie na wewe muzee akiisahau foni yake unaifanyia u-FBI! Hahaha Binamu bana! Punguza wivu japo kiduchu!
 
Je, unaweza kumruhusu partner wako asome sms zako hivi????Kama kuna neno moja la msingi ambalo ni msingi wa ndoa yoyote neon hili ni Uangavu (transparency).

Kamusiinafafanua kwamba neno uangavu maana yake ni kuona kitu moja kwa moja hadi ndani, ni kuwa wazi, kuwa huru kimawasiliano na zaidi ni kuwajibika.
Uangavu katika ndoa maana yake kumuona mpenzi wako hadi ndani na kumfahamu vizuri bila shaka maeneo yote ya maisha yenu.​

uangavu katika ndoa ni mwanaume au mwanamke kuweza kusoma sms na kupokea simu za mwenzake bila mashaka wala wasiwasi, kusoma emails zilizomo kwenye inbox yake bila wasiwasi wala hofu, Kufahamu akaunti yake benki ina kiasi gani, kuongea siri zako kwake bila mashaka na zaidi kuwa huru kuhakikisha mwenzako anajisikia vizuri kihisia.
Uangavu ni kuwa wewe bila kuwa na aina yoyote ya unafiki.​

wanadamu tuliumbwa na uwezo au hamu ya kutaka kumfahamu mwenzako kwa undani hadi usiwe na shaka wala wasiwasi.
Transparency ni process na haiwezi kutokea usiku mmoja tangu umefahamiana na mpenzi wako ingawa wapo watu ambao hata akiwa kwenye mahusiano hataki mwenzake afahamu mambo yake kitu ambacho si lengo la mahusiano.​

Uangavu ni kugundua au kupata uvumbuzi wa mambo mbalimbali mapya kwa mume wako au mke wako kwa sababu ya kuwekana wazi.

Bila kuwa na mawasiliano ambayo ni wazi mahusiano yanaweza kukwama.
Jambo la msingi ni wewe kuwa wazi kueleza kilichondani yako au siri zako kwa mwenzi wako (sincerely & straightfowawrd) na zaidi kushirikiana kupeana habari za kila kitu kinachohusu maisha yenu ili kuondoa wasiwasi, hofu na mashaka kwa mwenzako.​

Kuficha vitu si jambo la busara na unapokuwa wazi na mwenzako naye anakuwa wazi kwako kwani kuwa wazi ni kufahamiana na kufahamiana ni mahusiano na binadamu tuliumbwa kuwa na mahusiano.​

Je, upo wazi kwa mke wako au mume, au mchumba wako kiasi kwamba chake ni chako na chako ni chake?

Hupana tatizo iwapo unamwamini
 
Usiniambie na wewe muzee akiisahau foni yake unaifanyia u-FBI! Hahaha Binamu bana! Punguza wivu japo kiduchu!

Xpin nilikuwa na hizo ila sasa nimekoma sitaki tena hata aisahau hapo mwezi sipekui kabisa labda anambie mwenyewe
 
Hahaha! Ulishaipekua ukakutana na ya kukutana nayo? Pole sana.
 
Back
Top Bottom