Je, unaweza kumruhusu partner wako asome sms zako hivi?

Kuna wale wengine wameweka pin number
wana maana gani

Kama mimi vimeo vyangu viwili vimepigwa pin masaa 24. Ila wife ya kwake iko free. Siku akii lock hiyo kesi itaamuliwa kwa baba mkwe.
 
mi once in a while lazima nichungulie chungulie simu yake just for "curiosity", na yeye mara kadhaa nimeshamuona aki pitia inbox kwenye simu yangu tena mbele yangu wala hajifichi..!
 
Kama mimi vimeo vyangu viwili vimepigwa pin masaa 24. Ila wife ya kwake iko free. Siku akii lock hiyo kesi itaamuliwa kwa baba mkwe.

hahahaaaa, mkuu bana!,
mi mai waifu huwa hana taimu kabisaaaaa na simu yangu, na hana longolongo na simu yake nikiishika wala hakuna cha kwenda kupokelea simu pembeni na tukiwa wote humuoni yuko anabofyabofya simu!.
ukiona demu anapokelea simu pembeni ujue unaibiwa, stuka mpwa!.
 
kama una vimeo huwezi kuthubutu.....
 
Je, unaweza kumruhusu partner wako asome sms zako hivi? NDIO
 
Mobile are private entities, naruhusiwa kusoma zake ila simu yangu hairuhusiwi asije pata pressure bure! Akikuta picha za akina Joketi Mwengelo akiwa watupu itakuwaje?
 
Kama mimi vimeo vyangu viwili vimepigwa pin masaa 24. Ila wife ya kwake iko free. Siku akii lock hiyo kesi itaamuliwa kwa baba mkwe.

mhhh halafu mnasema wake zenu wagomvi, kwa hapo mie tungeongea vizuri, kwanini ya mwenzio uwe na mamlaka nayo?...
 
Namtahadharisha sana maihanei wangu hata kusogelea nusu mita simu yangu, hii kwa sababu za usalama wake mwenye. Ya kwake hata sitamani kuiona kila ikiita huwa mapigo ya moya wangu yanazidi sasa nikiishika si nita burst kabisa?
 
Kwenye blue mnaweza msiwe na malumbano lakini unaweza kuta unaliwa na we unakula nini bana tuelezee

Tizama vizuri. Nimesema hatuna malumbano yasiyo na msingi! Hayo ya kula au kuliwa hayawezi kuzuiwa kwa kusoma sms za mumeo/mkeo. Unajua mwanzo tulikuwa tunaweza kugombana kwa vitu vidogo tu. Inaweza kuanzia kwenye phonebook tu akiona majina ya kike inabidi ujiandae kujustfy uwepo wake kwenye phonebook yako!
 
Namtahadharisha sana maihanei wangu hata kusogelea nusu mita simu yangu, hii kwa sababu za usalama wake mwenye. Ya kwake hata sitamani kuiona kila ikiita huwa mapigo ya moya wangu yanazidi sasa nikiishika si nita burst kabisa?

Mpwa umenena jambo. Kabatan ka senks kamepotea ningekugongea. By the way how was your vekesheni at Segerea. Nilitaka kukuwekea dhamana mafisadi wakaniwekea uzibe.
 
ki ujumla mkianza kuchokonoleana fone, hakutakosa vimalumbano fulani, najiachiaga anasoma sms weeee akichoka ndo utackia hivi SMU ni nani? namwambiaga ni SMU... mana cjamtuma asome sms zangu....
 
Kama mwezi mmoja uliopita jamaa mmoja best wa miaka mingi aliniandikia kwamba alimpa kipigo mkewe cha hali ya juu. Kisa jamaa alitaka kujua email addresses zote za mkewe na pia ampe password ili awe na access nazo na kusoma kila kinachoingia. Mke akagoma kabisa kutoa passwords basi ndiyo kipigo kibaya sana kikamkuta. Na hii issue sidhani kama imekwisha hivyo ama Mume aamue kuacha kufuatilia au Mke aamue kuzitoa hizo passwords, vinginevyo ndoa iko kwenye matata makubwa.

Kama hakuna kibaya chochote cha kumficha mkeo/mumeo basi hakuna madhara ya kupeana ruhusa kuziangalia SMS zenu, lakini kwenye ndoa nyingi hali haiko hivyo. Kwenye ndoa nyingine hata cell phones zinafichwa kabisa Mke hajui mume kama ana mobile phone na vice versa.
 
Mpwa umenena jambo. Kabatan ka senks kamepotea ningekugongea. By the way how was your vekesheni at Segerea. Nilitaka kukuwekea dhamana mafisadi wakaniwekea uzibe.

Vekesheni ilikuwa poa sana, hata sikuchungulia nje kunani, nilikaa natafakari maisha.Ungenipa dhamana siku ile ningekuja kuua mtu bora nilipumzika nilikuwa na hasira sana.
 
mi nafkiri heri kukaa ukijua sasa yeyote mwenzako anawezashika simu yako na kuifanyia chochote, na ujue kuwa ukikataa tu ndo unamuhamasisha kuisoma zaidi=ugomvi lazima unyanyuke kama utaamua kuwa kichwa ngumu.
Be free.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…