Je, unaweza kunionesha Tanzania chama cha siasa kinachoweza kupigania uhuru wa kiuchumi na kufanya mapinduzi ya kiuchumi?

Blackafrica

Senior Member
Joined
Jun 26, 2021
Posts
141
Reaction score
401
Naandika kwa uchungu sana, vyama vyote kwa wakati huu havina maono wala ajenda ya kuisimamia, wanachama wake na viongozi wake, wamejaa unafiki na uwongo wa hali ya juu, nadhani ifike mahari tuwe na mgombea au wagombea binafsi katika nyanja mbali mbali za kisiasa, kijamii, na kiuchumi.

Msaada pekee tulionao na mabadiliko ya katika mpya, ewe Mtz amka na uwaamshe waliolala, nchi inahitaji katiba mpya ili tufike kaanani eeh! Mwenyezi Mungu utusaidie tuweze kujisaidia hapa tulipokwama.
 
Tatizo la Tanzania sio vyama vya siasa, bali ni aina ya watu(raia) wa nchi hii. Ikumbukwe viongozi ni Raia waliopewa madaraka, yaani wanatokea kwenye sample ya raia/wananchi.
Sifa za watanzania ni unafiki, roho mbaya, wizi, upigaji, kutokuwajibika, wabinafsi.. etc, huku wakijifanya wanampenda sana Mungu. Sasa jiulize kati ya hizo sifa hapo juu kuna yoyote inaendana na Mungu? ( Kumpenda Mungu bila kumtii ni kuthibiti mioyoni mwetu upenzi wetu kwa shetani badala ya huyo Mungu "tunayempenda").
Angalia miradi ya maendeleo, ni upigaji kila kona, hawa ndio Watanzania.
Haijalishi wametokea chama gani tabia zao ni hizihizi, Upigaji.
Ukiisoma ilani ya CCM, imejaa madini matupu na mipango mizuri ya maendeleo, ila tatizo sio ilani wala chama, bali tatizo ni watu wenyewe.
Hivyo usitegemee miujiza hata chama gani kiingie madarakani sababu watanzania ni walewale na tabia zao ni zilezile hivyo tegemea mambo yaleyale.
..
.
 
Naandika kwa uchungu sana, vyama vyote kwa wakati huu havina maono wala ajenda ya kuisimamia, wanachama wake na viongozi wake, wamejaa unafiki na uwongo wa hali ya juu, nadhani ifike mahari tuwe na mgombea au wagombea binafsi katika nyanja mbali mbali za kisiasa, kijamii, na kiuchumi.

Msaada pekee tulionao na mabadiliko ya katika mpya, ewe Mtz amka na uwaamshe waliolala, nchi inahitaji katiba mpya ili tufike kaanani eeh! Mwenyezi Mungu utusaidie tuweze kujisaidia hapa tulipokwama.
Mkuu nadhani umetoa maoni yako bila ya kupima ni kwa jinsi gani viongozi wa kisiasa wanatakiwa kuwasilisha kwetu hoja hizo.

Katiba ya nchi(ingawa ina mapungufu mengi) katika marekebisho yake wakati mfumo wa vyama vingi ulipopitishwa ikatoa haki na mizania sawa kwa vyama vyote vya siasa kufanya mikutano ya hadhara na maandamano yenye lengo la kustawisha demokrasia na kukosoa uzembe wa aina yoyote ule.

Angalia sasa kinachotokea, je, katiba inafuatwa? Ni chama kimoja tu hadi sasa kinaruhusiwa kufanya mikutano ya siasa na maandamano(kinyume cha katiba). Unategemea hao viongozi wa kisiasa kwa sasa watasimama wapi watoe sera mbadala yenye mwelekeo chanya kwa uchumi na ustawi wa nchi.?

Tulibakiwa kidogo na nafasi hiyo pale bungeni. Hebu angalia kilichotokea. Watanzania wenzetu wenye mawazo mbadala waliishia kupigwa risasi na kufukuzwa bungeni na mbaya zaidi kunyimwa tena nafasi ya uwakilishi wa bunge. Hivi sasa bunge ni la chama kimoja na kamwe usitegemee mawazo chanya yenye kuleta mapinduzi ya kiuchumi na kijamii nchini kwa bunge kama lile.

Kwa hiyo wakati ukifikiria kuwa viongozi wa vyama vya siasa hawana tena uthubutu wa kuliunganisha taifa kiuchumi, hebu angalia scenario hizo hapo juu halafu ndio u-draw conclusion yako.
 
Katiba ni ya hovyo ya chama kimoja,hata chama chako kikiingia madarakani kitayafanya hayo, kwani katiba hiyo hiyo inawapa nguvu, dawa ni kuwa na katiba nzuri inayoendana na wakati, vyama vimejaa ubinafsi na unafiki hakuna kitakachokuwa na afadhali kwa katiba hii
 
Tutafute katiba mpya kweli
 
Back
Top Bottom