Blackafrica
Senior Member
- Jun 26, 2021
- 141
- 401
Mkuu nadhani umetoa maoni yako bila ya kupima ni kwa jinsi gani viongozi wa kisiasa wanatakiwa kuwasilisha kwetu hoja hizo.Naandika kwa uchungu sana, vyama vyote kwa wakati huu havina maono wala ajenda ya kuisimamia, wanachama wake na viongozi wake, wamejaa unafiki na uwongo wa hali ya juu, nadhani ifike mahari tuwe na mgombea au wagombea binafsi katika nyanja mbali mbali za kisiasa, kijamii, na kiuchumi.
Msaada pekee tulionao na mabadiliko ya katika mpya, ewe Mtz amka na uwaamshe waliolala, nchi inahitaji katiba mpya ili tufike kaanani eeh! Mwenyezi Mungu utusaidie tuweze kujisaidia hapa tulipokwama.
Katiba ni ya hovyo ya chama kimoja,hata chama chako kikiingia madarakani kitayafanya hayo, kwani katiba hiyo hiyo inawapa nguvu, dawa ni kuwa na katiba nzuri inayoendana na wakati, vyama vimejaa ubinafsi na unafiki hakuna kitakachokuwa na afadhali kwa katiba hiiMkuu nadhani umetoa maoni yako bila ya kupima ni kwa jinsi gani viongozi wa kisiasa wanatakiwa kuwasilisha kwetu hoja hizo.
Katiba ya nchi(ingawa ina mapungufu mengi) katika marekebisho yake wakati mfumo wa vyama vingi ulipopitishwa ikatoa haki na mizania sawa kwa vyama vyote vya siasa kufanya mikutano ya hadhara na maandamano yenye lengo la kustawisha demokrasia na kukosoa uzembe wa aina yoyote ule.
Angalia sasa kinachotokea, je, katiba inafuatwa? Ni chama kimoja tu hadi sasa kinaruhusiwa kufanya mikutano ya siasa na maandamano(kinyume cha katiba). Unategemea hao viongozi wa kisiasa kwa sasa watasimama wapi watoe sera mbadala yenye mwelekeo chanya kwa uchumi na ustawi wa nchi.?
Tulibakiwa kidogo na nafasi hiyo pale bungeni. Hebu angalia kilichotokea. Watanzania wenzetu wenye mawazo mbadala waliishia kupigwa risasi na kufukuzwa bungeni na mbaya zaidi kunyimwa tena nafasi ya uwakilishi wa bunge. Hivi sasa bunge ni la chama kimoja na kamwe usitegemee mawazo chanya yenye kuleta mapinduzi ya kiuchumi na kijamii nchini kwa bunge kama lile.
Kwa hiyo wakati ukifikiria kuwa viongozi wa vyama vya siasa hawana tena uthubutu wa kuliunganisha taifa kiuchumi, hebu angalia scenario hizo hapo juu halafu ndio u-draw conclusion yako.
Tutafute katiba mpya kweliKatiba ni ya hovyo ya chama kimoja,hata chama chako kikiingia madarakani kitayafanya hayo, kwani katiba hiyo hiyo inawapa nguvu, dawa ni kuwa na katiba nzuri inayoendana na wakati, vyama vimejaa ubinafsi na unafiki hakuna kitakachokuwa na afadhali kwa katiba hii