Je, Unaweza Kupeleka Copy Kama Ushahidi Mahakamani?

Je, Unaweza Kupeleka Copy Kama Ushahidi Mahakamani?

Joined
Apr 26, 2022
Posts
83
Reaction score
128
Leo tuangalie kama copy (nakala/vivuli) vinaweza kupokelewa na kutumika kama ushahidi Mahakamani. Au, je ni lazima upeleke original tu?

Kiujumla, ushahidi wa nyaraka (documents) unaweza kuthibitishwa Mahakamani kwa njia mbili: Kupitia “primary evidence” au “secondary evidence”. Soma section 63 ya Sheria ya Ushahidi ya Tanzania (Tanzania Evidence Act, kwa kifupi huwa tunaiita TEA).

“Primary evidence” ni nyaraka yenyewe halisi (original document itself) na “secondary evidence” ni copy (kivuli/nakala). Soma kifungu cha 64 na 65 TEA.

Lakini, sheria ya Ushahidi ya Tanzania (TEA), inataka kwanza upeleke Mahakamani primary evidence (original) na sio kopi (nakala/kivuli). Ni kweli kopi inaruhusiwa lakini kuna masharti. Usije ukafikri ukipeleka tu kopi itapokelewa automatic. Soma kifungu cha 66 cha TEA.

Sasa kama una kopi (nakala/kivuli) tu, labda original (halisi) imepotea au anayo mtu mwingine, mfano upande wa pili kwenye kesi, utafanyaje?

-You file a notice requiring the other party to produce original document before or during hearing. (Unatakiwa umpe notice (ilani) ya kumtaka huyo mwenye original (halisi) ailete Mahakamani kabla ya kesi au aje nayo Mahakamani wakati wa kusikiliza kesi). Section 68 ya TEA. (Kuna exception lakini, ila general rule toa notice).

Kwa hiyo ingawa, kifungu cha 67 cha TEA, kinaruhusu kuleta kopi lakini lazima uzingatie masharti ya kifungu cha 68 ambacho kinataka utoe notice. Upande wa pili usipoleta, basi Mahakama itapokea hiyo kopi yako.

Asanteni, kama una swali au nyongeza karibuni.

Mwandishi: zakariamaseke@gmail.com
(0754575246 - Advocate Candidate.)
 
Back
Top Bottom