Je, unaweza kurithi silaha?

Ndio inawezekana, baada ya marehemu mwenye umiliki kufariki silaha inarudishwa polisi kuhifadhiwa halafu baada ya hapo polisi watakupa utaratibu wa kufanya kama unataka kumiliki hiyo silaha.
 
Irudishe polisi utapewa utaratibu. Ila utaruhusiwa kuimiliki tena endapo utakidhi vigezo vya kumiliki silaha. Kama huna vigezo na unaonekana huna sifa zinazohitajika huwezi ipata tena.
 
Hapana, unapaswa uirudishe polisi na kuomba kibali wewe kama wewe kama unataka kuimiliki.

Mimi niliipeleka ya marehemu baba yangu Oysterbay Police na wakanipa option ya ku apply kibali halafu niimiliki au kuiuza.
Nili opt kuiza na nikapata 650,000, ilikuwa mwaka 2004. Ilikuwa ni Berreta 92SB.
 
Irudishe police na uende na baruwa za usimamizi wa mirathi
 
Je, ninaweza kurithi silaha kutoka kwa mzazi wangu marehemu?
Jibu ni HAPANA!
Ili uweze kumilikishwa silaha unatakiwa uwe na vigezo MUHIMU vilivyopo kisheria
Mfano:
1; Uwe na sababu za kuhitaji kumiliki silaha
2. Usiwe mlevi au unaye penda ugomvi
3. Usiwe na tabia zisizokubalika kwenye jamii (wizi, utapeli, nk)
4. Uwe na Akili timamu na umri stahiki
Na hapo nimekupa tu mifano ila kama ni maombi ya kumiliki silaha; yana anzia huku chini kabisa mtaani/kijijini hadi huko wilayani.

Kama umeachiwa Silaha ipeleke tu Polisi watakuelekeza, lakini pia watakusaidia taratibu za kuiuza mfano kwenye maduka rasmi yanayo uza silaha (yapo mijini) ili upate pesa kihalali kabisa.
 
Je, ninaweza kurithi silaha kutoka kwa mzazi wangu marehemu?
Kama ni short gun tuwasiliane uniuzie mimi.

Kumiliki silaha kwakuwa mmiliki amekufa itakusumbuwa hukujiandaa.

Mchakato wake unaanzia serikali ya mtaa, kata, kwa OCD, kamati ya Ulinzi na usalama ya wilaya then ya mkoa ukipass ndio unaitwa CAR kwenda kupewa kitabu cha fire Army licence.

Offer yangu iko limited kuna order ya Bunduki nimeomba Mzinga jeshini, ukitaka mpunga hiyo silaha nikupe pesa ipo kwenye mfuko wa shati lakini kahifadhi Polisi au Tanganyika Armys.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…