Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Yaani hata kile cha kuombea maji au kusalimiana au kujitambulisha tu kwa walugha wenzio.
Haya ni matokeo ya fikra na falsafa chanya ya Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere katika kupiga vita na kutokomeza mipaka na ubaguzi wa kikabila nchini.
Kwa mafanikio na matokeo haya, nadhani nia yake hii njema, iliambatana na maombi kwa Mungu ili ifanikiwe..
Mawazo na maono ya mwalimu, yamefanya umoja, mshikamano, uhuru na amani miongoni mwa waTanzania, kua imara sana na wa uhakika mno licha ya changamoto kidogo za maoni na mitazamo tofauti ya kisiasa, ambayo ukabila hauna athari zozote ndani yake.
Na kadiri tunavyokwenda, katika muda usio kua mrefu wazaliwa wa dar kwa mfano, hawatakua wanajua hata kuongea lugha za makabila yao ispokua lugha ya Taifa na lugha nyingine za kibiashara na kimataifa pekee.
Sura na fikra za kikabila zitatoweka na kutokomea kabisa nchini.
Asanti mwenye heri, Baba wa Taifa Mwl.J.K.Nyerere🐒