KakaKiiza
JF-Expert Member
- Feb 16, 2010
- 11,794
- 9,075
Wadau najua wengi tunatumia sana Bodaboda,swali je unafahamuje kuwa boda boda niliyemchukua ni mharifu?
Basi ungana na mimi kujua ni jinsi gani walivyo na endapo ukiona yupo hivi jua huyo ni muharifu usipande bodaboda wake.
Kwa hayo machache hizo tips nimekupa kuwa makini!
Basi ungana na mimi kujua ni jinsi gani walivyo na endapo ukiona yupo hivi jua huyo ni muharifu usipande bodaboda wake.
- Kwanza chombo chake lazima kiwe kikukuu!
- Bodaboda yake lazima iwe ni Boxer 150 cc japo hata 120cc
- Bodaboda yake katiak Plate no yake inaweza kuwa imekatwa kipande kwa maana inaonekana imekatika.
- Bodaboda yake Plate No Imekunywa imesimama kama mabawa ya ndege kwa maana huwezi kusoma reg no ukiona hivyo huyo ni muharifu kuwa makini
- Kama usiku Ukiona amefunga taa za flashlight za kuumiza macho katika plate No jua huyo ni muharifu usipande.
- Ukiona boda boda pikipiki imefungwa vitambaa vyenye maua ya bange huyo ni muharifu usipande,
- Ukiona Bodaboda amevaa kandambili na ni mchafu na anavirasta vichafu huyo ni muharifu
- Ukiona bodaboda kavaa kijaket hakielezi kituo chake basi huyo ni muharifu usipande.