Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,713
- 6,121
Huwa ninaamini kwamba Humu JF wamo Mabilione hata hivyo napenda zaidi kuzungumzia uhalisia;
Ukiwa katika Jiji la Dar es salaam ukabahatika kutembea katika maeneo ya watu matajiri kama Masaki,Mikocheni,Mbezi Beach na baadhi ya maeneo mengine ya watu wenye ukwasi unaweza kufikiri kwamba wewe hutakaa uwe katika orodha ya matajiri.Kati ya matajiri wengi ambao ninawafahamu ni wachache sana ambao walifahamu kwamba siku moja na wao watakuja kuwa matajiri.Utajiri ninaouzungumzia hapa sio huu utajiri wa kawaida wa kupata mahitaji yako ya msingi na kumiliki assets ambazo haziwezi kukufanya usurvive kwa miezi sita bila kipato chako cha sasa.Hapa ninazungumzi utajiri ambao unweza kukufanya usurvive kwa maisha yako yote yaliyosalia bila kuendelea kufanya shughuli yoyote ya kiuchumi.
Aina au kiwango cha utajiri ninaozungumzia hapa ni ule ambao unakuwezesha wewe kufanyiwa kazi na pesa yako badala ya wewe kuifanyia kazi PESA yako.Katika lugha ya kisasa tunasema unakuwa BILIONEA katika thamani ya DOLA.Nakwepa kutumia thamani ya shilingi kwa sababu Kigezo hicho kinakuondoa katika nafasi ya kuitwa BILIONEA.
Katika upambanaji wa kutafuta RIZIKI unaweza kujikuta unakuwa BILIONEA sio kwa KUBET wala kwa dhuluma bali ni kwa kuweza kutumia Fursa adhimu za kuweza kuwa Bilionea.Ili uweze kuwa BILIONE ni lazima utambue kwamba kuwa Bilionea lazima uanze mwanzo kabisa na unaze chini huku ukiwa na malengo makubwa.Ni lazima utambue kwamba wewe kama mwanadamu umepewa karama nyingi sana na uwe na utayari na ujasiri wa kuzitumia karama hizo ili kuwafanyawatu wengine wawe na furaha.Leo hii nitawashirikisha baadhi ya mbinu tunduizi ambazo ukizizingatia unaweza kuwa Bilionea Baada ya miaka 3.Sisemi kwamba ni rahisi maana ingekuwa rahisi nisingeandika bali ningekuwa busy natengeneza PESA so unaposoma ni lazima uamue kwamba kweli unataka kuwa BILIONEA ili uweze kuelewa hasa kile unachopaswa kufanywa.
Karibuni tujadili mbinu ambazo unaweza kuzitumia kuanza safari yako ya kuwa BILIONEA cha muhimu ni kuamini kile unachotamani kiwe katika maisha yako.

- Anza na ulicho nacho hapo ulipo.
- Je unaposoma andiko hili upo wapi?una nini?Unawezaje kutumia hicho ulicho nacho hapo ulipo kuanza safari yako ya kuusaka ubilionea?Ili kwenda level tuseme hapo ulipo una shilingi 10,000 cash.Una GB 2 za bando,una simu ya mkononi smart ambayo ndo unasomea andiko hili,Uko katika jiji la dar e salaam mitaa ya Tandale na unaishi kwenye chumba cha kupanga ambacho kodi inaisha tarehe 30 na hujui pesa ya kulipa utatoa wapi.SO in short uko chini kabisa.Hata hivyo kwenye simu yako una namba za simu za ndugu,jamaa,marafiki na mademu ambao umewahi kuwala kimasihara na ukachukua muda na kuandika kwenye ule uzi wetu pendwa ili kuonesha jinsi unavoweza kuwala kimasihara.Huenda huna ajira nyingine na hata hio 10,000 uliwapiga vilaza masela wako wenye ajira za kima cha chini.
- Kwa upande wa elimu unaweza kuwa ni mhitimu wa chuo kikuu cha dar es salaam na umesoma zile kozi ambazo huwa tunaulizanaga huku kwamba zina ajira na mishahara minono.Nyingine huwa ni nondo sana kiasi kwamba ukiamua kuzisoma unakula supp na carry za kutosha.Unaweza pia ukawa na elimu ya form six isyokuwa na cheti au ukawa naelimu ya form four isyokuwa na cheti au ukawa na elimu ya la saba hawaulizagi cheti.Unaweza pia ukawa una elimu ya ufundi au kadiploma flani au kacertificate flani.Namaanisha kwamba unaweza ukawa na kaujuzi fulani au maarifa fulani au cheti fulani au vyote kwa pamoja.In short unaweza kuwa na kitu fulani ambacho unaweza kukifanya kwa ajili ya watu wengine.Unaweza kuwa na sura au misuli iliyojaa(Nguvu) Inshort kwenye ubongo wako kuna kitu fulani ambacho unaweza kukitoa pembeni ya ule utaalamu wa kuchambua mgogoro Russia na UKRAINE
- Kuhusu mazingira yako hapo kwa mtogole najua panakuwaga na kaharufu fulani na pia huwa kuna mateja wanazagaaga sana hio mitaa kiasi kwamba ukiwa mgeni ukishuka hapoa unaweza hisi kukimbia bila kukimbizwa.Sijapia mida sana hilo eneo so panaweza kuwa pako poa maana nimeishi hio mitaa sana.Vyovyote vile palivyo najua hapo mtaani kuna masela zako wengi ambao wengine ni choka mbaya kuliko wewe na wengine ni wajanha kuliko wewe lakini najua kwamba hapo mtaani kwenu wapo vijana wa rika lako,wengine wakubwa na wako wazee ambao ni wakongwe wa hilo eneo na wapo pia ambao ni wageni kabisa au wadogo ndo wanaibukia.Hayo ndio mazingira yako.
- Kila mahali kuna matatizo na changamoto na hapo kwenu yapo tena mengi.Tuanze na matatizo ya kawaida kama ya kiuchumi,kiafya,kielimu na kimazingira.Kiuchumi hapo kwenu umaskini upo tena wa hatari na wewe ni mmoja wa hao mafukara wa mtaani kwenu so katika hali ya kawaida wewe ni fukara wa kifedha pamoja na kwamba unajua kusoma na kuandika.Kwa upande wa afya mmejitahidi kulazimisha kinga zenu za mwili ziweze kustahimili hali ya magonjwa yaliyopo hapo kaisi kwamba ni wageni tu wakija ndo huugua ili nyie wenyeti haman shida yoyote.Kwa upande wa mazingira ndo kama hivyo nyumba nyingi ni kongwe na mazingira ni machafu kiasi cha kujikuta mkihisi manishi jehanamu.
- Tafuta suluhu ya matatizo(Gundua Fursa)
- Kila tatizo ni fursa.Kila Fursa ina matatizo yake.So hapo mtaani kwenu hapo hayo matatizo mliyo nayo ni fursa.Ili kuweza kuyatatua lazima kwanza uyatazame kama fursa.Ukishayatazama kama fursa jitazame juu ya uwezo wako wa kuzitumia fursa na watu ambao unaweza kushirikiana nao kwa namna moja ili kufanikisha kugeuza matatizo kuwa FURSA.Kwa mfano mnaweza kuamua kwamba sasa mnataka mboreshe makazi ya hapo kwenu.Mkaanza kujiongeza na kujipanga kwa blocks huku kila mmoja akiweka thamani ya eneo lake.Baada ya kuhakikisha kwamba mmefanya utahminishaji wa kina mkatafuta developers kama NHC au wa kutoka nje ya nchi wakaweka Low cost housing scheme hapo kwa mtogole na kisha mkamiliki kwa mfumo wa condominium/Appartment.Kwa Gharama za Ujenzi za siku hizi kujenga Ghorofa lenye residential Units 300 za kiwango cha chini zinaweza gharimu labda Bilioni 10(Huu ni mfano).So mkijiweka kwenye mtaa mmoja mkajiunga na kutafuta muwekezaji aje apaendeleze kisha awape units zenu za kuishi zinaitwa UNIT titles na nyingine mkawa mnakusanya kodi na yeye anakusanya kodi kwenye nyingine.Maisha yanaendelea na mji unazidi kupendeza badili ya kuishi ka raia wasotakiwa mkisubiri kuja kununuliwa na wajanja ambao husaini mikataa kama hiyo na developers.
- Unapotafuta suluhu ya tatzio unakuwa unalipwa premium kwa sababu unaweza kujikuata unapata fursa ambazo hukutarajia.So ni muhimu sana ukatafuta kutatua matatizo ya jamii na dunia kwa ni nia moja ya kupata utajiri wa juu.So usiweke akili yako kwenye hayo maghorofa bali unaweza angalia hata namna ya kutibu tatizo la harufu ya watu wanaozibua choo hapo mtaani kwenu kwani nayo ni fursa.
- Gonga Milango
- Hili ni eneo muhimu sana.Gonga milango ya viongozi wa mtaa wako,Gonga milango ya matajiri unaowafahamu na usio wafahamu,zungumza na viongozi wa kisiasa,kijamii na kidini na uhakikishe kwamba unawashawishi.Usiogope kukataliwa kwa ni katika watu mia utakao ongea nao 90 watakukataa so ni muhimu uhakikishe kwamba hawa 10 unawatumia vizuri .Usiogope kukataliwa kwani wanaokukataa iko sikua watakukubali wenyewe.Ni muhimu uhakikishe kwamba unajenga mtandao wako kikamilifu na watu sahhihi.Tembelea Makampuni na wafanya biashara,tembelea ofisi za serikali tembelea taasisi za kimataifa.Peruzi mitandao ya UN,blogs za habari uangalie namna ambavyo unaweza kuwatumia katika kufikia lengo lako la kuwatumia kutatua tatizo la hapo mtaani kwako.Uiswatafute kwa ajili ya kutatua tatizo la tanzania nzima bali tatizo la hapo kijiweni kwenu ahapo mnapovutia Ganja hapo mnapokunywa Gahawa na hapo mnapopiga stori zenu.Yale matatizo ya hapo ndio uwatafute ili washirikiane na wewe kuyatatua
- Usiogope
- Huwa ninaamini kwamba uoga wa mtu ndo umaskini wake.Usiogope kushindwa,kukataliwa,kudharaulika,kuzomewa kukataliwa kutokuelewa au hata kufukuzwa.Jitahidi tu uhakikishe kwamba unakuwa na confidence ya kutosha kwani uzoefu wangu unaonesha kwamba mtu anayejiamni huwa hakataliwi na mtu yeyote yule.Cha muhimu ni kusema tu kwamba IT IS NOT OVER until IT IS DONE
Karibuni tujadili mbinu ambazo unaweza kuzitumia kuanza safari yako ya kuwa BILIONEA cha muhimu ni kuamini kile unachotamani kiwe katika maisha yako.