Je, ungefanya nini kama ungekuwa na rasilimali zisizo na kikomo?

Je, ungefanya nini kama ungekuwa na rasilimali zisizo na kikomo?

ChatGPT

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2019
Posts
532
Reaction score
1,011
Fikiria kwa muda kwamba una rasilimali zisizo na kikomo - muda usio na kikomo, pesa zisizo na kikomo kumzidi hata Elon Musk, maarifa yasiyo na kikomo zaidi ya watu maarafu kama kina Isaac Newton, na uwezo usio na kikomo. Ungefanya nini na wingi huu? Ungesafiri kwenda sehemu zote duniani? Kuanzisha biashara? Kuanzisha mradi wa ndoto yako? Kusaidia wale wenye uhitaji? Au ungefanya kitu tofauti kabisa?

Najua kuna wale watakaosema issue za kuwa na wapenzi wengi, wakali, na kila masihara wanayofanya itick (iwe kweli)😂😂 rikiboy 😉, nk… yote ni sawa katika kueleza fikra zao.

Hakuna jibu baya, na hakuna wazo kubwa au dogo sana. Tujifunze kuwa wabunifu na kudream big pamoja! Twende kazi!!
 
Mimi ningesafiri kila nchi duniani napenda adventure ndoto yangu itatimia siku moja
 
Mimi ningesafiri kila nchi duniani napenda adventure ndoto yangu itatimia siku moja
Big up sana. Hiyo safari yako ushaianza kwa kuanzia maeneo ya hapa Tanzania kama Mlima Kilimanjaro, mbuga, Kilimanjaro marathon, nk
Ama bado bado 😉
 
Big up sana. Hiyo safari yako ushaianza kwa kuanzia maeneo ya hapa Tanzania kama Mlima Kilimanjaro, mbuga, Kilimanjaro marathon, nk
Ama bado bado [emoji6]
Bado najipanga mkuu mdogo mdogo
 
Aisee ningekua na vyote ivyo nisingefurahia Maisha hata kidogo. Ningefanya kila niwezalo nipoteze na kusahau kila nilichonacho.

Wakati mwingine hili maisha Ya-make sense inabidi kuwe na Ups and Downs

Ndomana Mapambano siku zote hayaishi.
 
Me ningegawa tu rasilimali zote..nikawapa watu Kwan hii dunia niyetu?😂😂
 
Back
Top Bottom