Je, ungependa baadhi ya taarifa zako mtandaoni zifutwe na kusahauliwa kabisa?

Je, ungependa baadhi ya taarifa zako mtandaoni zifutwe na kusahauliwa kabisa?

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
RTBF 1.jpeg

Katika zama hizi za kidigitali, taarifa zetu binafsi zimezagaa katika majukwaa mengi, na mara nyingi hatuna uwezo wa kuzifuta kabisa taarifa hizi zisionekane na umma. Taarifa hizi zinashikiliwa na taasisi na makampuni binafsi, n.k. Lakini je, ni lazima taarifa hizo kubaki hivyo daima?

Katika nchi za Ulaya, kwa mfano, Sheria ya Ulinzi wa Data – yaani General Data Protection Regulation (GDPR), inawapa watu haki ya kufutwa/kusahaulika ili kulinda faragha zao kwa kuhakikisha kwamba wanaweza kudhibiti ni taarifa gani zinapatikana kuhusu wao mtandaoni. Haki hii inaruhusu watumiaji kuomba kufutwa kabisa kwenye mtandao kwa mambo ambayo wanaona hayana umuhimu tena au yamepitwa na wakati.

Moja kati ya mambo yaliyoibua zaidi hisia kuhusu haki hii ni pale Mahakama ya Haki ya Umoja wa Ulaya ilipoamua mwaka 2015 kwamba kulikuwa na haki ya kisheria ya faragha kwa raia wa Uhispania, Mario Costeja kuilazimisha kampuni ya Google Spain kufuta kumbukumbu za mtandaoni zinazohusu madeni yake ya zamani ambayo yalikuwa yameshalipwa kitambo.

Mahakama hiyo ilisema kwamba watu katika Umoja wa Ulaya wanaweza kuondoa mtandaoni taarifa binafsi ambazo zinaonekana “kutokuwa na umuhimu tena".

Taarifa zinaonesha kuwa katika mataifa 27 ya Umoja wa Ulaya, mtu yeyote anaweza kutuma ombi moja kwa moja kwa wanaoshikilia taarifa zake kupitia Fomu ya Ombi la Haki ya Kufutwa (Right to Erasure Request Form) yenye kurasa tatu inayoomba mwandishi kuthibitisha utambulisho wake, na sababu za kutaka taarifa zake zifutwe. Baada ya maombi hayo Umoja wa Ulaya utatoa takriban siku 45 kwa mshikiliaji wa taarifa hizo kujibu. Hata hivyo, kwa sababu ambazo zitaonekana zina mashiko, mshikiliaji wa data anaweza kukataa kufuta kwa sababu zenye mashiko.

Nini faida yake?
Kwa kawaida kila mtu katika maisha anapitia vipindi tofauti. Na si kila tunalofanya leo tutajivunia baadaye – vitu tunavyovipenda/kuvichukia hubadilika. Akili nayo inaendelea kukomaa na kubadilika. Hivyo basi, kuwa na uwezo wa kufuta taarifa zetu ambazo hazina umuhimu kunaimarisha usalama wetu na amani ya akili. Ni jambo linaloweza kuboresha afya ya akili kwa kiasi kikubwa, na kuruhusu watu kusonga mbele bila kuishi kwenye kumbukumbu ya makosa ya zamani au taarifa potofu zinazowahusu.

Zaidi ya hayo, haki hii inasaidia kulinda heshima na sifa ya mtu binafsi katika jamii. Makosa ya zamani au taarifa potofu zinaweza kusababisha madhara makubwa kwa maisha ya mtu, ikiwemo kupoteza kazi, kudhalilishwa hadharani, au kuathirika katika mahusiano binafsi.

Pia, kwa wale ambao wamekuwa wahanga wa uhalifu wa mtandaoni kama vile udukuzi au unyanyasaji wa mtandaoni, haki ya kufutwa inatoa fursa ya kuondoa athari za matukio hayo. Hii inawapa nafasi ya kurejesha usalama wao wa kidigitali na kuanza upya kwa amani zaidi.

Katika ripoti yake ya Tafsiri ya Haki za Binadamu Kimataifa kwa Muktadha wa Kidigitali (Translating International Human Rights for the Digital Context), World Economic Forum inaeleza kwamba “…sisi sote tuna wajibu wa kusaidia kujenga dunia ya kidijitali yenye usalama, tija na uvumbuzi."

Haki ya Msingi
Haki ya Kufutwa si tu dhana ya kisheria—ni haki msingi ya kibinadamu. Ingawa nyaraka za Umoja wa Mataifa kama Azimio la Kimataifa juu ya Haki za Binadamu (Universal Declaration of Human Rights – UDHR) na Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (International Covenant on Civil and Political Rights - ICCPR) hazitaji moja kwa moja Haki ya Kufutwa/Kusahaulika, lakini zinajenga kanuni msingi ya faragha ambayo Haki ya Kufutwa inajengwa juu yake.
 
Zitafutika google lakin kwa allah, zitakutangulia kwenye kiama.
M/mungu mola wetu mlezi, aturuzuku matendo mema na mwisho mtukufu
Ah! 😀

Sema hapa FaizaFixy sikulenga MAOVU specifically. Zipo taarifa ambazo si MAOVU ambazo mtu fulani asingependa kuona zikiendelea kuwa wazi kwa umma baada ya muda fulani. Ukisoma vizuri utaona mfano wa Bwana Mario Costeja. Ahsante sana kwa mchango lakini. Nimeuheshimu.
 
A
Zitafutika google lakin kwa allah, zitakutangulia kwenye kiama.
M/mungu mola wetu mlezi, aturuzuku matendo mema na mwisho mtukufu

Zitafutika google lakin kwa allah, zitakutangulia kwenye kiama.
M/mungu mola wetu mlezi, aturuzuku matendo mema na mwisho mtukufu
Acha ushamba na ulimbukeni wa kujifanya ww ni mjomba na Mungu.

Kila taarifa anazoweka mtu mtandaoni ni za uovu?
 
Back
Top Bottom